Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Alafu ndio mana tafiti zinaonyesha kuwa kati ya wanne mmoja ni kichaa
 
Me nilikuwa nasoma vidudu katika jengo moja hivi la duara lina gorofa moja lipo karibu na uwanja wa mpira wa kambarage........... nilikuwa naishi naishi majengo ya zamani karibu na buchosa bar mtaa wa maduka mengi
Tulikuwa majirani kiasi chake bro ila vidudu wewe ni mdogo wangu wa mwisho.
 
Kwani ukubwa ni mpaka ule tunda maana wengine toka tunacheza kibaba mama mizigo tunakula tena haina wivu?
 
Mnaoshangaa watoto,hamjui hii ndo generation mpya imacoverup wakati wale wazamani wakipukututika na kuachia nafasi,
haa sio watoto tena wameshakua wakubwa,waliokuwa la pili,la kwanza sasa wana miaka 24-25,hawa ni watu wazima tu,hata wewe wa miaka 35 ama 40 sasa unaweza kuoa bila tabu.


Mimi kipindi hicho niko dodoma nafuatilia pensheni ya kustaafu,kwakweli tulilia sana
 
Kuna mdogo wangu alikuwa na miaka kama 5 hivi, alipoona watu wanalia na yeye akaanza kulia huku hamjui hata huyo nyerere, siku zilipopita RTD wakaanzisha kile kipindi cha saa 2 na robo usiku Nyerere anaongea.

Dogo ndo kuniuliza kama mtu akifa anaongea tena, nikamwambia hizo wamezirekodi akawa hanielewi, ikabidi nimrekodi kwa kutumia casseti na zile kanda (music tape), baadae nikamwekea akajisikia akiwa anaongea, ndo kumwambia hata akifa ile tutaendelea kuisikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…