Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Mimi nilikuwa moja ya maofisa wandamizi ngazi ya wilaya siku hiyo tulikuwa kwenye semina pande za Singida ile tunatoka break tunakuta kwenye ofisi za serikali bendera zipo nusu mlingoti na watu wapo kwenye vikundi vya watu wachache wakiongea kwa sauti za chini chini tukajua tu Nyerere ametutoka kipindi kile TV ni chache mpaka uende bar uagize kinywaji
 
Nilikua Kitanzini.. Ukumbi tuliokua tunautumia kusomea awali wa Olofea ulivamiwa kwan ndo ulikua una Tv kubwa karbu iringa yote
 
nilikuwa darasa la tano shule ya msingi Gungu kule mjini kigoma mwisho wa reli
 
Mtu aliyekuwa darasa la tatu make alikua na around 9-10 yrs, sasa ukijumlisha 17 unazungumzia mtu mwenye 26-27, huyu ni mtu mzima na wengine wana familia kubwa tu.
Ni kweli ni watu wazima but sio kwa makelele wanayopiga humu ndani na kutaka kutuambia they are omniscient
 

nlikua chekechea shule moja hv huko MOSHI
 
Mkuu sitakaa nisahau mi nilikuwa ndo niko darasa la saba ila kipindi anatangazwa kafariki tulikuwa migombani tunachuma kahawa na redio tulikuwa nayo tumening'iniza kwenye mkahawa!!tena umenikumbusha dedio ilikuwa aina ya national ile ya batery 4 kubwa[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…