Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Interesting article: binafsi nilkuwa katika ajira ya serikali miaka 6 tayari,(nilianza ajira na age ya 18). Lakin siku ya tukio nilkuwa nafanyakaz part time Maili 2 dodoma kwa DR Chihoma dispensary km clinical.
Nakumbuka wiki nzima kabla ya kifo kulikuwa na updates za taarifa ya hali baba wa taifa inavoendelea, na ilkuwa inatolewa na rais mkapa, kwa maongezi ya kawaida watanzania tulikuwa tunajisemesha huyu mzee afi tu watangaze...ikawa kila siku siku watu tunaulizana na hali ya baba wa taifa ata tukikutana mtaani... na kuwa strong enough hata wakitangaza amekufa tulikuwa tayari......

Hali ilikuwa tofauti sana...mara Rais Mkapa kutanga kifo chake kili mtu aliduaaa, aliinamana chini...watu walishindwa kujizuia kulia....nakumbuka nilishnidwa kufanya kazi siku hyo maana tangazo lilitoka mchana....

R.I.P Mwalimu Nyerere
 

Umeona madhara ya utu uzima unaisahau hata keyboard yako baba angu
 
Nilikuwa chekechea mchana nimerudi nyumbani nikamsikia babu anamwambia baba mzee kafariki , ila mm sikujua ni nani ndo baadaye nikaanza kusikia wanaimba kwenye redio Tanzania!!
 
Nilikuwa kidato cha pili jitegemee secondary. Nilifika hadi kuaga mwili uwanja wa taifa kwani ni jirani sana na shule
 
Mi nilikua darasa la 5 s/m ilonga mazoezi ghafla ikapigwa kengele hao tukaruhusiwa kwenda zetu nyumbani
 
Ukiwa na miaka 24 ukawa unataka mwl Afe tu. Sasa una 41 unaionaje Tanzania hii?
 
Nilikua s/m Kiganza darasa la kwanza ilikua wenzetu wa darasa la saba wakifanya party yao kisha mziki ukazwa
 
Ulimwelekeza vizuri. You are good.
 
Lkn Jk Nyerere alikuwa na moyo wa pekee, muda wote wa kukaa madarakani ameondoka na kaunda zake tu!!
Leo mtu mkimpa hata uenyekiti wa mtaa atawaibia mpaka vijiko vya ofisi![HASHTAG]#Tunakukumbuka[/HASHTAG]
 
hahaha mkuu una hatari, ulifuta kanda bongomani ya mzee. Hukula bakora kweli?
 
hahaha mkuu una hatari, ulifuta kanda bongomani ya mzee. Hukula bakora kweli?

Ha ha ha, mzee alikuwa na kanda zake ambazo anazitunza mwenyewe, za Madilu System na Rwambo ukigusa umeumia.
 
Kumbe huku % kubwa ni watoto ?,ushauri wangu ni huu,suala la umri lizingatiwe ili uweze kuwa member wa jf,pls wahusika walifanyie Kali
Tangu Nyerere afariki ni miaka 17 sasa. Kama mtu alikuwa la pili labda alikuwa na 7 au 8 maana yake sasa ana 24 au 25 mtawalia.
Mtoto ni kabla ya 18.
 
14 Oktoba, kwani Darasa la Saba walikuwa bado hawajamaliza shule ndugu..? Au ndo umetuingiza mjini..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…