Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Nilikuwa kwenye meli siku hiyo Mv Mapinduzi, nikitoka Mtwara kuelekea dsm, obviously sikuelewa kinachoendelea kwa kuwa nilikuwa bado mdogo na uwezo wa kuchambua mambo ulikuwa wa kiwango cha chini sana, ila nilishuhudia watu wakisema Tanzania haitakuwa salama mara baada ya kuondoka kwake!
 
young kid.....nikua nasari(vidudu)...... ckumbuki chochote zaidi ya nyimbo mfululizo radio tanzania dar es salaam.... kuulizwa naambiwa nyerere kafa, nyerere ni nani ? hapo sasa sielewi hata.... old memory thou
 
Doh naona aibu kusema...mi nimeskia ukubwani tuu, tena shuleni.
 
Nilikuwa nyumbani kwetu nacheza michezo ya kitoto
 
Dah! 1999 niko Form One, Makongo High School.
 
Ulikuwa wapi?,mimi nilikuwa darasa la pili shule moja maarufu jijini Mwanza, mwalim akapiga kengele akasema tunarudi nyumbani sababu Nyerere kafariki,nilikuwa hata sijui Nyerere ni nani, mimi nilikuwa namjua Ben Mkapa pekee,kurudi nyumbani jioni yake tunakuta Komba tayari ameshafanya yake (Jamaa alikuwa fasta sana) japo Tv tulikuwa tunaangalia kwa jirani.
Nyerere pumzika kwa amani
Kona baaa na mtoto rubby
 
Nilikuwa Fourth year UDSM, FoE, Electrical...
 
Muda wa kusema ukweli umefika sasa, nina miaka zaidi ya 30 lakini leo hii bado unaniita mtoto hv unafikiri matendo ya kitoto ndio yatakwisha? Tuheshimiane jamani hata katiba inanitambua, mpaka wimbo wa taifa pia unanitambua, nisipotajwa kwenye viongozi wote basi nipo kwenye wake na waume. Mtoto ni yule ambae ni below 18 na mtu mzima ni over18
Sijasahau, mada ni kuhusu kifo cha J.K.Nyerere.
Miaka minne nyumbani kijijin sielewi chochote
 
Kumbe huku % kubwa ni watoto ?,ushauri wangu ni huu,suala la umri lizingatiwe ili uweze kuwa member wa jf,pls wahusika walifanyie Kali
🙂🙂🙂 wengi wakubwa ila wezeee wengi ambao hawajasema walikuwa wapi
 
Muda wa kusema ukweli umefika sasa, nina miaka zaidi ya 30 lakini leo hii bado unaniita mtoto hv unafikiri matendo ya kitoto ndio yatakwisha? Tuheshimiane jamani hata katiba inanitambua, mpaka wimbo wa taifa pia unanitambua, nisipotajwa kwenye viongozi wote basi nipo kwenye wake na waume. Mtoto ni yule ambae ni below 18 na mtu mzima ni over18
Sijasahau, mada ni kuhusu kifo cha J.K.Nyerere.
kweli kiongozi
 
Back
Top Bottom