Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Inavuta hisia-Unatoa pole
Ukitoa pole-Inaleta hasira
Ukikanda na kududumiza-Ahsante

...halafu
Dukuduku zao zinatoka bila ya kuhojiwa.
Zipo Uzi nyingi kama hii JamiiForums leo.

Aliyepiga simu na kufika Tandale, Chama watuletee picha za Tanga

Poleni Wafiwa
 
Sasa hivi ni kuomba sana usiugue maana hizo Hospital ni changamoto mnooo,

Nilienda hospital ya Amana rushwa inayotembea kwenye ile hospital hadi nilistaajabu, sasa imagine mtu hana pesa ya kutoa hiyo rushwa ndio anakufa kama mfugo,

Kingine wazazi mjitahidi sana kukata Bima ya Afya kwa Watoto wenu ni msaada mkubwa sana na ukiona sehemu huielewi basi unaenda pengine Bima si unayo bhana.

Mola amlaze mahala pema Mtoto.
Hamasisha watu ni 50400 tu ila watu bado uelewa mdogo, utasikia ni gharama
 
mkuu mimi pia natumia bima ya afya, ila hospitali zote za jirani wananijua. Wewe nikiona dalili ya kudharauliwa na vitoto vidogo sina uvumilivu.

nilimripoti mpumbavu mmoja alinijibu tu "leo watu wa bima hatutibu, mtandao hakuna", nami nikamjibu "leo unanitibu, mtandao utaupata tu, subiri dakika 3 zijazo uone".

Nikaongea na mkurugenzi mkuu wa NHIF moja kwa moja, zilipigwa simu dakika 20, alikuja kunitibu mganga mkuu mwenyewe, kwa samahani na pole nyingi sana.
Hayo ndo mambo sasa yanayotakiwa yafanywe na wananchi.

Tatizo hatujiamni pale unapo jibiwa jibu japesi na mtoa huduma na Upo katika hali mbaya au mgonjwa wako anahitaji huduma ya haraka.
Tunasubiri mpaka yatukute.

Take action pale in apo bidi tusilaze damu.
 
Mwenzako anataka rambirambi
Yaan baada ya kusoma nikapata majonzi, hasira na maswali mengi. Ila hili swali moja tu jepesi hataki kujibu na ndo swali la MSINGI. JINA LA HOSPITAL..
Hataki kujibu.

Hapo ndipo watu wanamwekea ????.
 
Pole sana, ina maana hospital ipo moja tu hilo eneo had unasubiri masaa saba mgonjwa ahudumiwe?yani network ndio ushindwe kuhudumiwa?Daktari anatumia network kujua ugonjwa wa mgonjwa?ulishindwa kuanzisha mtiti hadi mtoto ahudumiwe wakat wakisubiria network yao?Tuache kuwa wapole kwenye mambo ya msingi na tujifunze kutokana na hili.Sitak kukupa lawama ila wakat mwngne tuchukue hatua kabla mabaya hayajatokea na kutupa lawama kwa wengine ata yakitokea angalau kuna namna tumeenda mbele zaidi kuyazuia.
 
Binafsi naona kuna kitu hakijakaa sawa.... Naona kama unataka kutupiga kamba hivi?

1. Hutuambii mtoto alikuwa anaumwa nini..

2. Hutuambii kaanza kuumwa lini na imekuaje mpaka umauti ukamfika.

Kingine katika vitu ambavyo hospitali huwa wako makini navyo ni watoto na wajawazito.... Ni ngumu sana mtoto kukaa masaa 7 bila kuhudumiwa kama kweli alikuwa amezidiwa..

Hebu leta vithibitisho vya wewe kuhudhuria hospitali, tutumie hata picha ya risiti ya consultation tuu..
Hyu jamaa labda story katunga tu,maana ata hospitali kagoma kuitaja amebak analalama tu
 
Yaan baada ya kusoma nikapata majonzi, hasira na maswali mengi. Ila hili swali moja tu jepesi hataki kujibu na ndo swali la MSINGI. JINA LA HOSPITAL..
Hataki kujibu.

Hapo ndipo watu wanamwekea ????.
Niko radhi kukujibu yote ila sio kuandika hapa njoo inbox au namba yangu 0699574224
 
Naomba mwandishi mmoja mzuri aneweza kuandika anaitafute nimuelezee mwanzo mwisho yeye ndio aandike mimi sijaja kuomba au kumwambia mtu nimelia uchungu huishe lakini hauishi naitaji faraja hata ya maneno wana jf naumia sana jamani nafarijika nikisoma pole
 
Mwanangu aliumwa usiku ghafla tukalazimika kwenda hospitali ya karibu wakasema tumpeleke hospital ya ++++, kufika pale saa 8 usiku wanasema network hakuna hadi irudi wamekuja kumhudumia asubuhi saa 4 mtoto kashalegea anatapika damu nyeusi. Tumemlaza kitandani wakaniagiza mavitu mengi kumbe mtoto amekata roho kwa uzembe wa madaktari.

Naumia sana, mwanangu kachomwa chomwa kateseka kafariki kwenye maumivu makali sana kwa uzembe. Nisamehe mwanangu na ulale salama kama ningekuwa na pesa usingefariki maana masikini nimeganda na wewe masaa 7 hospitali bila msaada.

Kwanini wasingemhudumia mtoto jamani naumia sana mimi jamani
POLE SANA APUMZIKE KWA AMANI MTOTO WETU
 
Binafsi naona kuna kitu hakijakaa sawa.... Naona kama unataka kutupiga kamba hivi?

1. Hutuambii mtoto alikuwa anaumwa nini..

2. Hutuambii kaanza kuumwa lini na imekuaje mpaka umauti ukamfika.

Kingine katika vitu ambavyo hospitali huwa wako makini navyo ni watoto na wajawazito.... Ni ngumu sana mtoto kukaa masaa 7 bila kuhudumiwa kama kweli alikuwa amezidiwa..

Hebu leta vithibitisho vya wewe kuhudhuria hospitali, tutumie hata picha ya risiti ya consultation tuu..
Ni wachache sana wanaweza kuliona hili.
Jambo linalonishangaza amekataa kata kata kutaja hosipitali.
Naona pia amejiongeza...anaweka namba ya simu kimya kimya.
Anaachia waliozidiwa na huruma watume wenyewe.

Huyu mfiwa pole zake lakini umakini.
 
Naomba niulize nikitaja hospital itamrudisha mwanangu? Namba sihitaji mchango nahitaji msaada wa kiroho au mwana saikolojia nahisi roho yangu inatoka sijatumiwa na mtu hata 100 wala sijaomba pesa ya mtu punguza ujuaji kwenye masuala ya watu
 
Mtoto ama mtu mzee ni watu delicate sana when comes kwenye kuumwa, you can loose them any time - cha kufanya ni kujitahidi sana kuwa na bima ambayo unaweza kutibia hosp yoyote kubwa ambayo ina vipimo vyote.

With critical condition please wazazi jitahidi kufika hosp kubwa - hosp kubwa cha kwanza ni moja kwa moja kwenye chumba cha emergency wakati wewe unaendelea kujaza makaratasi ya bima.

Pole mzazi, its painful.
 
Naomba niulize nikitaja hospital itamrudisha mwanangu? Namba sihitaji mchango nahitaji msaada wa kiroho au mwana saikolojia nahisi roho yangu inatoka sijatumiwa na mtu hata 100 wala sijaomba pesa ya mtu punguza ujuaji kwenye masuala ya watu
Mfiwa huyo...ambaye hata mtoto hajazikwa!!
 
Itaje hospitali ikiwezekana kama unamjua huyo aliesema network hakuna mtaje pia. Hakuna kitu cha thamani zaidi ya uhai wa binadamu.

Wahudumu wa hospitali sijui ni wamezoea kuona watu wakifa, yaani kwao hilo huwa haliwastui kabisa.
Mtu yuko mahututi wala hawajali.
 
Back
Top Bottom