Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Pole Sana ndugu yetu na ninaomba uwasamehe wale wote ambao Kwa maana moja au nyingine wametumia lugha mbaya huenda ni stress tu za Maisha.
Sijajua wewe ni Imani gani lkn Kwa waislamu,tunaamini kwamba mtu au kiumbe chochote hakitakufa Ila wakati wake ikifikia,na wakati ukifika hata ungezungukwa na madaktar bingwa kiasi gani hawatoweza kukusaidia,hiyo ni mipango ya mungu,inatakiwa umshukuru mungu na umuombe akupe badala ya huyo uliyempoteza, ukiwa na Imani hii hautaweza kumkufuru mungu.

Huwezi jua mungu amekuepusha na nini au atakupatia nini kutokana na kifo cha huyo mtoto,najua kama mzazi itakuwa vigumu kunielewa lkn naomba umuombe mungu akupe faraja ktk kipindi hiki kigumu.
 
nimempeleka rafiki yangu hospitali yuko taabani..kumuingiza kwa dokta hata ajachekiwa Dokta anapiga simu mochwar km kuna nafasi.
kweli bongo nyoso!!
unampeleka mgonjwa hospitali kweli dokta anakuelekeza sehemu majeneza bei rahis ilipo!!daahh hii nhi ngumu sana.

na lile rungu lenu kubwa kule mochwari maiti akipiga chafya mnaenda kumtwanga nalo kumalizia sio poa kabisa.

pole sana mfiwa
 
Polee sana.
 
hii nchi ina viumbe vya ajabu mno. Yani kama ingekuwa mimi nimepeleka mgonjwa ningemtanguliza huyo daktari mochwari.
 
Dah!! Pole sana. Hakuna maumivu makali kwa binadamu kama haya ya kumpoteza mtu umpendaye.

Hata mimi nilimpoteza mke wangu miaka kadhaa iliyopita, kwa uzembe wa hawa jamaa. Natambua maumivu unayopitia. Mwenyezi Mungu akujalie wepesi katika kipindi hiki kigumu unachopitia.
 
Pole sna na Mungu akutie nguvu katika magumu yaliyokupata
 
NHIF ya Toto Afya Kadi ni 50400 kwa mwaka, mtoto anatibiwa hospital nyingi.
Wazazi wengi ni wazembe kwa makusudi hawakati hii bima wakati ni msaada sana
 
Pole mkuu I feel your pain!
mtoto alikuwa na umri gani
 
NHIF ya Toto Afya Kadi ni 50400 kwa mwaka, mtoto anatibiwa hospital nyingi.
Wazazi wengi ni wazembe kwa makusudi hawakati hii bima wakati ni msaada sana
Hio nilikata mapema sana ili siku lilitokea la kuhitaji uharaka wa huduma basi dogo apatiwe huduma chap hata kama sipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…