Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Shida wahudumu wanajisahau sana , sijui kisa wamesoma ? Huyo malaika ameondoka lakini tumwachie Mungu.
 
Taja jina la hospitali ama sivyo ni chai kama chai nyingine humu,
 
Mwanangu aliumwa usiku ghafla tukalazimika kwenda hospitali ya karibu wakasema tumpeleke hospital ya ++++, kufika pale saa 8 usiku wanasema network hakuna hadi irudi wamekuja kumhudumia asubuhi saa 4 mtoto kashalegea anatapika damu nyeusi. Tumemlaza kitandani wakaniagiza mavitu mengi kumbe mtoto amekata roho kwa uzembe wa madaktari.

Naumia sana, mwanangu kachomwa chomwa kateseka kafariki kwenye maumivu makali sana kwa uzembe. Nisamehe mwanangu na ulale salama kama ningekuwa na pesa usingefariki maana masikini nimeganda na wewe masaa 7 hospitali bila msaada.

Kwanini wasingemhudumia mtoto jamani naumia sana mimi jamani
Pole sana kiongozi, pole sana.

Vv
 
nimempeleka rafiki yangu hospitali yuko taabani..kumuingiza kwa dokta hata ajachekiwa Dokta anapiga simu mochwar km kuna nafasi.
kweli bongo nyoso!!
unampeleka mgonjwa hospitali kweli dokta anakuelekeza sehemu majeneza bei rahis ilipo!!daahh hii nhi ngumu sana.

na lile rungu lenu kubwa kule mochwari maiti akipiga chafya mnaenda kumtwanga nalo kumalizia sio poa kabisa.

pole sana mfiwa
[emoji1][emoji1] wewe muongo hadi kwenye mambo seriously

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni sehemu ya huo uzembe pia. Baba wa mtoto yupo wapi? Hospitali ni moja tu hapo ulipo?
RIP chalii mdogo.
Kabla ya kulaumu kwa nini kwanza usimuulize hilo unalotaka kujua akufahamishe?.

Sasa taarifa huna na bado umebaki kumlaumu...Vipi kama Baba naye alishatangulia mbele ya haki, au anatumikia kifungo au yupo mbali kikazi n.k.
 
Mkuu pole sana. Sasa hapa si unatumia ID fake? Unaogopa nini tena kutaja jina la hiyo hospital kwa faida ya wengine??

Kwa mara nyingine pole sana ndugu.
 
Vifo tanzania ni uzembe hasa mahospitalini
Pole sana mungu akufanyie wepesi,uzembe plus madokta wetu kufanya kazi kwa mazoea,mgonjwa akifika hosp anatakiwa aanze matibabu mda huohuo...DK anamuweka mgonjwa bila matibabu toka saa 7 mpka saa 4 huyo sio DK ni muuaji yani kaka yake na shetani
 
Mkuu pole sana. Sasa hapa si unatumia ID fake? Unaogopa nini tena kutaja jina la hiyo hospital kwa faida ya wengine??

Kwa mara nyingine pole sana ndugu.
Hata akiitaja mara 100 haibadilishi lalamiko lake kuwa hakukuwa na network maana yake ili aweze kuhudumiwa aliitaji network means (Ni mnufaika wa BIMA?) Kama jibu ni ndio.....

Maana yake Taasisi ya BIMA husika ndio inatakiwa kujibu kwanini ukienda kuhudumiwa kama hakuna network au umeme hawakuhudumiii? Maana yake mfumo husika (Kampuni ya hiyo bima ijitafakari)
 
TAJA HIYO HOSPITAL MZEE UNAOGOPA NINI NA WAMETUULIA MTOTO WETU..?
All in all mimi naamini ktk KARMA au Malipizi hapahapa duniani... Wao au Watoto wao wafe kiroho mbaya AMEN 🙏
 
Poleni sana Mungu awatie nguvu. Madaktari wa bongo hata hivyo kanjanja nyingi sana. Hakikisha ugonjwa unaombiwa unao unaosoma tena pia mwenyewe kwenye internet na dawa unazopewa soma pia matumizi yake na side effects zake.

Niliwahi pewa dawa rufaa mbeya nilianza kuumwa sana kichwa bila kujua hadi nikapima sana vipimo kichwa hakipoi kila kitu kipo sawa nikaambiwa nifanyiwe city scan.

Kabla ya kwenda kama zari tu kusoma side effects za dawa inasema kichwa kikikuuma acha kunywa mara moja rudi kwa doctor akupe dawa nyingine. Niliacha kunywa kesho nikaamka mzima wa afya.
 
Sasa mzee wote hao wa nini mimi nimekuambia ukiwa na familia jitahid uwe na ukaribu na madoctor maana akiwa rafiki yako unaweza hata kutibiwa kwa mkopo au bure kama ni dereva muhimu uwe na ushoga na trafic ukikamatwa hata kwa kosa gan ni simu moja tu bia zenyewe buku jero tu ukipokea mshahata ukimtengea safar saba za buku jero hapo ni elfu kumi na mia tano tu ushamzimisha
Dah,we bana haya bana nimekusoma
 
MWANANGU AMEFARIKI AKIWA NA MIAKA 2.5 TAYARI ALIKUWA MKUBWA NAMTUMA NAMFUNDISHA ALIKUWA NA AKILI NA MTOTO MZURI SANA MSIBA UPO CHAMA KARIBUNI TUMPUMZISHE UHAI WAKE UMEDHULUMIWA MUNGU NASHITAKI KWAKO MIMI MASKINI NISIE NA SAUTI
 
Back
Top Bottom