Kifo cha Norah; aliyejifanya mwanaume ili ajue maisha ya wanaume yakoje

Kifo cha Norah; aliyejifanya mwanaume ili ajue maisha ya wanaume yakoje

Niliangalia mahojiano yake YOU-TUBE, na jinsi alivyokuwa anakaa Bar-Counter na kuanza kuwachombeza wanawake wenzake. Kuna madhara makubwa sana kiakili mtu huyapata kwa kuishi maisha yasiyo na uhalisia.

Feminists, Transsexual na Homosexuals hupata majanga ya kisaikolojia kama mgogoro wa kitaswira (Identity Crisis). Mwisho huwa mbaya sana, sema vyombo vya habari havipendi kutangaza hizi habari.
 
" lakini kaitka kizazi hiki kuwa mwanaume ni shida. Utafiti uliofanyika mwaka 2020, ulionyesha kuwa 70% ya watu wasio na makazi (homeless) ni wanaume. Pia hatari ya mwanaume kujiua ni mara 4 zaidi ya mwanamke. 90% ya ajali za sehemu ya kazi ni za wanaume"

NDIO MAANA TUNASEMA ZAMA HIZI KUOA NI KUJITAFUTIA MATATIZO
 
Ninapitia mengi sana kwasababu ya UANAUME WANGU.
Naam! wewe unapitia mengi mno na mpaka uje kutulia kiakili na kukomaa itachukua muda. Uko na mgogoro mkubwa kisaikolojia (You're highly conflicted).

Huna tatizo, ni sehemu ya makuzi ambayo wanaume wote tunapitia. Ndiyo maana unatukashifu majukwaani, halafu tukikujibu ambacho hupendi kukisikia unafuta nyuzi zetu haraka. Ulinichekesha na kunishangaza mno siku ile.

Lakini, huu ni mgogoro ambao naamini utaisha tu siku ukifikia kitu kiitwacho ukomavu (Maturity Curve). Binafsi nilikuwepo hukohuko ambapo upo wewe leo hii.
 
Naam! wewe unapitia mengi mno na mpaka uje kutulia kiakili na kukomaa itachukua muda. Uko na mgogoro mkubwa kisaikolojia (You're highly conflicted).

Huna tatizo, ni sehemu ya makuzi ambayo wanaume wote tunapitia. Ndiyo maana unatukashifu majukwaani, halafu tukikujibu ambacho hupendi kukisikia unafuta nyuzi zetu haraka. Ulinichekesha na kunishangaza mno siku ile.

Lakini, huu ni mgogoro ambao naamini utaisha tu siku ukifia kitu kiitwacho ukomavu (Maturity Curve). Binafsi nilikuwepo hukohuko ambapo upo wewe leo hii.
Nanii, una hakika umemkoti mtu uliwai jadiliana nae before ya huu uzi?.
 
View attachment 2500007

Kifo cha Norah Vicent kiliibua hisia kwa jamii kutokana na namna utafiti alioufanya ulivyommaliza yeye mwenyewe. Norah alitaka kujua maisha ya mwanaume yakoje..ni changamoto zipi anapitia? Mwaka 2003, bila kubadili jinsia yake, akaamua ajifanye kuwa mwanaume; akaajiri mtu wa make up,mtaalamu wa sauti, pamoja na mwalimu wa mazoezi ya viungo.

Kwa miezi 18 akawa na jina jipya, Ned. Akajiunga timu ya mpira wa wanaume, akaanzisha mahusiano na wanawake, na kufanya kazi kwenye ofisi ya wanaume pekee. Lakini Norah, sasa Ned, hakuona raha yoyote na bila kujijua akaanza kupata msongo wa mawazo...depression. Kwenye kitabu chake "Self-Made Man" akakiri kuwa wanawake, pamoja na wanaharakati, huwa wanaamini wanawake ndio wanapitia magumu mengi katika jamii lakini ukweli ni kwamba wanaume wana machungu mengi katika maisha yao.
Wanaume wanateseka, Wana matatizo tofauti na ya wanawake, lakini bora sisi, wao wanahitaji zaidi upendo, kuonewa huruma" alisema Norah.

Zamani ukizaliwa mwanaume ilionekana ni bahati na nafasi ya upendeleo; lakini kaitka kizazi hiki kuwa mwanaume ni shida. Utafiti uliofanyika mwaka 2020, ulionyesha kuwa 70% ya watu wasio na makazi (homeless) ni wanaume. Pia hatari ya mwanaume kujiua ni mara 4 zaidi ya mwanamke. 90% ya ajali za sehemu ya kazi ni za wanaume

kwa aliyokutana nayo Norah, alipata matatizo ya akili yaliyotesa kwa zaidi ya miaka 17, na mwishowe julai 6, 2022 akaamua kujiua huko Switzeland. Kuwa mwanaume ni kazi.

View attachment 2500010
Mm namwambiaga dem wangu nikikupa kichwa changu walau siku moja tu basi utakufa kabisa maana hataweza kuhimili yale niliyonayo kichwani..

Anabaki kucheka tu..😅anaona kama jokes asijue ndio ukweli wenyewe huo.
 
wanaume tumeumbwaaa matesooo!!! Matesooo!! Mahangaikooo!! [emoji445][emoji445]
 
Back
Top Bottom