Na katika hii safari ya kuwa mwanaume Kuna wengi hasa kizazi Cha Sasa wameshindwa na kuishia kuwa binadamu jinsia ya tatu(mashoga) na wengine wakakwepa majukumu na kuishia kujiua.
Huo ni ukweli usiothubutu kusemwa. Wanaume wengi ukiwaona wanapokutana sehemu yoyote iwe bus stand, au bus stop, kwenye daladala, sokoni, barabarani, makanisani, misikitini, makazini na popote ambapo ni lazma ukutane na watu, utaona kama wanaumoja wanasalimiana kama wanajuana. Kisha kila mtu anaendelea na lililompeleka pale.
Lakin Trust my word. Huo uelewano wa haraka na mshikamano rahisi wanao-potray si halisi na huwa hauna uhalisia kivitendo. Hakuna hata mmoja mwenye nia thabit ya kumsaidia mwingine ama kumdokezea mwingine fursa ili aende mbele ama apate unafuu.
Ushirikiano ni salam. Tuu na si zaidi.
Inastahili ukiwa maeneo ya umma na ukaona kuna jambo unaweza ukashauri likaleta unafuu kwa mwingine umshauri amjulishe pale pale si lazma mpaka asiwe jinsia yako.