Kifo cha Sokoine: Watoto wake wataka mwili uchunguzwe kubaini kama alikufa kwa ajali au la!

Kifo cha Sokoine: Watoto wake wataka mwili uchunguzwe kubaini kama alikufa kwa ajali au la!

tangu 1984 mpaka 2013 ndio uchunguzi uanze???? hata kama ni wabaya wake watakuwa wamenusurika katika kipindi hiki cha miaka 30 iliyopita wawe hai?
 
Acha kutokwa na povu uchunguzi marekani ulifanyika kwa Rais takribani miaka mia baada ya kifo chake, kama kifo ni cha utata inawezekana wakati huo watoto na ndugu hawakua na uelewa acha uchunguzi ufanyike watu wawajibike au serikali iwajibike unaogopa nn au na ww uko ktk mkondo huo?
Hii habari inanichanganya. Nakiri kwamba sikuwahi kusikia kabisa habari za mazishi ya pili ya Ndugu Edward Moringe Sokoine hapo mwaka jana (sijui ni tarehe zip za mwezi upi?). N'nachokumbuka tu ni kwamba Moringe tulimzika katikati ya zizi la ng'ombe kijijini kwao Monduli na zizi likaendelea kutumika kusetiri ng'ombe kama ilivyo desturi yetu. Nakumbuka mengi yalisemwa baada ya kifo cha Moringe; ya kishirikina na ya kimafya kinyume kabisa na "post mortem report" ya madaktari. Leo ninapopata habari kama hii najiuliza maswali yafuatayo:
  1. tangu Sokoine afariki tarehe 12 Aprili 1984 hao watoto wake walikuwa wapi?
  2. Post mortem investigation hufainyika ili kubaini sababu za kifo cha marehemu si kwa malengo ya maelezo na kumbu kumbu tu bali pia ili kuchukua hatua kama kuna ushaidi wa kutosha kwamba kifo kimesababishwa na uzembe au makusudi ya mtu yeyote. uchunguzi huu ukifanyika sasa na ikagundulika kuna mazingira ya kuwa kifo kilisababishwa na makusudi au uzembe wa yeyote itasaida nini iwapo wasabishaji walishakufa miaka mingi?
  3. Mazingira mazuri zaidi ya kufanya post mortem investigation ni wakatimwili bado mbichi kikemikali. Kwa hali ya kifo hiki cha takribani miaka 29 tangu kitokee na mazingira aliyozikwa (na kuzikwa tena baada ya tetemeko) huo uchunguzi utatumia sayansi ipi?
  4. Uchunguzi huu unachochewa na nini sasa hivi na una maslahi gani kwa taifa na familia (kwa hao watoto wa marehemu?)
 
siri kubwa kuhusiana na kifo cha sokoine anayo lowassa, kwa hili hata jkn alikuwa anamgwaya sana edo! Mnakumbuka jinsi ambvyo edo alimtaka jkn aende monduli kumsafisha baada ya kumtuhumu kuwa alimchafulia jina kwa kauli zake? Captain lowassa ana mambo mengi ambayo akiamua kuyaweka hadharani watu wengi sana watabadilika kimitazamo!

Sijui kwanini ameamua kukaa kimya hata pale ambapo huwa anaonewa wazi kabisa! Kuna watu ambao hofu haziwaishi kwa kuogopa kuwa ipo siku atalipiza kisasi kwa wanayomtendea hivyo kuzidisha kasi ya kuendelea kumchafua.

...moringe aliuawa na hili halina pingamizi! Kuna watu walikuwa hawako radhi kumuona mtu anambishia jkn...walikuwa wanauwezo wa kukupoteza faster then wanaenda kumpa taarifa! Wakati mwingine jkn alikuwa anaishia kusikitika tu maana hakuwa na uwezo wa kurejesha uhai!



.......fact!
 
Hivi kweli watu mnahoji Kama watoto wa sokoine wakijua ukweli itakuwaje? Nani asingependa kujua ukweli wa kifo cha mzazi wake? Kama itathibitika aliuawa Ina maana kutakuwa kuna watu walihusika, nani na kwasababu gani hivyo vitafuata baadae hatimaye wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria hata Kama watakuwa wazee kwa sasa! Leo tunashuhudia aliyekuwa mshindi wa nishani ya Nobel mtunzi wa mashaili Pablo Neruda wa chile inayesemekana aliuawa wakati wa utawala wa augusto Pinochet mwaka 1973 ukifukuliwa kwa uchunguzi! Lengo ni kukomesha watu wanaofikiri wanaweza kutoa roho za wenzao Kama wao ndio waliowaumba na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria na kuwapa Amani familia ya Marehemu kwa kujua kiini cha kifo cha mpendwa wao.
 
Hata watoto wa Mwalimu nyerere nao utasikia wanataka wa baba yao ufaniwe uchunguzi!waacheni wapumzike bhana
 
Kwanza niipongeze familia ya Sokoine kwa uamuzi huo, ccm umafia hawakuanza kwa akina mwangosi, ulimboka, kibanda, mwakyembe na mwandosya, wamefanya unyama mwingi, pia nawahimiza familia ya karume, kolimba na nyerere na waombe uchunguzi, yatagundulika mengi
 
tangu 1984 mpaka 2013 ndio uchunguzi uanze???? hata kama ni wabaya wake watakuwa wamenusurika katika kipindi hiki cha miaka 30 iliyopita wawe hai?

Aliyeamuru naye marehemu kwa sasa
 
Ndio maana MaCCM yanaogopa CHADEMA kushika dola wanajua uozo mwingi utajafichuka na hata msukule wa Balali waweza kuibuka akawa HAI tena.
 
haya, kama serikali itaridhia basi huo uchunguzi ufanyike ila sidhani kama Hao waliohusika watapelekwa mahakamani. ni wangapi wananaonewa, kupigwa, kuteswa na hats wengine kuuliwa Ila waliotenda hayo hawafungwi? Ila ngoja tuone
 
kupoteza muda na pesa bila xababu apo. je kama ikigundulika na wahusika hawapo duniani, kesi itakula kwa nani?
 
Katika hali ya kushangaza,watoto na baadhi ya ndugu wa aliekuwa waziri mkuu wa Tanzania,marehemu Sokoine, wanataka uchunguzi ufanyike wa mwili wa marehemu ili kubaini kama ni kweli kifo chake kilitokana na ajali au laa.

Uamuzu huo ulofikiwa mara baada ya mwili wa marhemu Sokoine kuzikwa upya mwishoni mwa mwaka jana baad ya kabuli la awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi katika milima ya Oldonyo Lengai.

Taarifa zinasema wanafamilia hao wanakusudia kuomba kibali serikalini ili wataalamu waufanyie uchunguzi mwili huo kubaini chanzo cha kifo chake.

Kulingana na taarifa za gazeti la Tanzanian Daima la tarehe 07/04/2013,ambapo habari hii imeelezwa kwa kirefu zinasema uamuzi huo ni kutokana na hofu kuwa huenda kifo chake kilitokana na hujuma za wale waliokuwa wakimpinga hayati Sokoine katika vita vyake vya kupambana na wahujumu uchumii wakati huo.

Imeelezwa mh.Lowassa ni miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi hayo yalifanyika saa saba za usiku mwishoni mwa mwaka jana.

CHANZO:TANZANIA DAIMA ONLINE.

Labda kama wana wasiwasi .kuwa uenda alipewa sumu .kama ni ajali ya kupangwa unafukua maiti ya nini ? Labda wadai uchunguzi upya wa ajali ulivyotokea .
 
Mwaka huu kumekuwa na kumbikizi ya miaka 40 ya kifo cha Edward Sokoine, ambacho kiligubikwa na utata mkubwa, kukiwa na madai kwamba hakufa kwa ajali bali aliuwawa na watu ndani ya uongozi ambao walimwogopa sana.

Huenda ni kweli, kwa sababu wakati fulani Sokoine alitaka kumweka nguvuni kiongozi wa juu sana serikalini kwa kosa la ufisadi, na Nyerere ndio alimzuia akimwambia angesababisha mgogoro mkubwa wa kiuongozi. Sokoine alikubali, japo kwa shingo upande.

Hata hivyo, wakati Nyerere akiongelea kung'atuka na ikionekana wazi mrithi wa Nyerere angekuwa Sokoine, kuna viongozi walishikwa na uoga mkubwa juu ya hatima zao. Wengi waliona wazi kwamba siku Sokoine anaapishwa kuwa raisi basi milango ya jela ilikuwa wazi kwao, pamoja na wale ambao Sokoine alitaka kuwakamata na Nyerere akamzuia.

Kwa mfano, akihutubia Bunge pale Dodoma kabla ya kuanza safari ambayo ilimuua, Sokoine alikuwa ameweka ahadi kwamba akifika Dar es Salaam, alikuwa na list ya viongozi ambao walitakiwa kutupwa kikaangoni. Inaonekana Sokoine alitaka kwanza kuijadili ile list na Nyerere. Ndipo watu wanasema, akaliwa timing hata huko Dar es Saalam asifike.

Sasa katika mazingira ya ile ajali, ambayo kimsingi hayakuwa ya "head-on collision", Mercedes Benz walidai kwa maelezo yaliyotolewa juu ya ajali ilivyotokea, Sokoine hakupswa kufa. Na wakaenda mbali zaidi na kusema, wanataka walete wataalamu wao ili wachunguze, kama ni kweli Sokoine alikufa akiwa ndani ya gari yao ya Mercedes Benz, akiwa amekaa kiti cha nyuma, na kwa nini alikufa.

Sasa kumbuka gari aliyopata nayo ajali Sokoine ilikuwa customized na Mercedes Benz kwa ajili ya viongozi, yaani order za ikulu, kwa hiyo huwa zinatengenezwa maalumu kuwa na usalama zaidi kuliko gari ya kawaida. Kwa hiyo kwa Mercedes Benz hili la kusema Sokoine alikufa katika mazingira ya ajali kama ile, waliona ni kuchafua jina lao. Wakaomba waje kufanya uchunguzi, serikali ikawakatalia.

Sasa unajiuliza, kulikuwa na siri gani nyuma ya kifo cha Sokoine ambacho serikali ya Nyerere haikutaka zivuje? Kumbuka, Nyerere alikuwa ni aina ya kiongozi ambaye hata angejua Sokoine ameuwawa, asingetaka ulimwengu ujue hilo. Kwake hadhi na heshima ya Tanzania vilikuwa vitu muhimu sana, na alikuwa tayari kutotoa ukweli wa jambo kama hilo ambalo aliona lingelifedhehesha taifa la Tanzania.

Kwa mfano, kuna kikundi kilimfuata Nyerere na kumwambia Mwalimu, Sokoine ameuwawa katika mazingira ya ushirikina, kachukuliwa msukule na wanajua nani walifanya hivyo katika viongozi wa taifa. Wakasema wanaweza kabisa kumrudisha hai Sokoine ikiwa watamuwahi kabla hajamalizwa kabisa! Nyerere akasema, mie naamini kabisa haya mambo ya msukule na najua yanafanyika. Na huenda ni kweli Sokoine kafanyiwa hivyo. Lakini sasa niambieni, mie baada ya kuutangazia ulimwengu kwamba kijana wangu Sokoine amekufa, na nyie mkamrudisha, nitatoa tangazo gani jingine kwa ulimwengu, na huo ulimwengu utanionaje mimi na Tanzania kwa ujumla? Akasema kama mnataka kunisaidia, basi kama hajafa bado ni msukule, fanyeni afe kabisa ili hao waliomfanyia haya wasije wakamtesa.

Kwa kumkumbuka Sokoine, hebu jiulize, ikiwa leo Sokoine kwa muujiza fulani angefufuka na kuwa Raisi wa Tanzania, ni nani katika viongozi wetu waliopo madarakani milango ya jela ingefunguliwa kwa ajili yao?

1713439207798.png
 
Back
Top Bottom