Mwaka huu kumekuwa na kumbikizi ya miaka 40 ya kifo cha Edward Sokoine, ambacho kiligubikwa na utata mkubwa, kukiwa na madai kwamba hakufa kwa ajali bali aliuwawa na watu ndani ya uongozi ambao walimwogopa sana.
Huenda ni kweli, kwa sababu wakati fulani Sokoine alitaka kumweka nguvuni kiongozi wa juu sana serikalini kwa kosa la ufisadi, na Nyerere ndio alimzuia akimwambia angesababisha mgogoro mkubwa wa kiuongozi. Sokoine alikubali, japo kwa shingo upande.
Hata hivyo, wakati Nyerere akiongelea kung'atuka na ikionekana wazi mrithi wa Nyerere angekuwa Sokoine, kuna viongozi walishikwa na uoga mkubwa juu ya hatima zao. Wengi waliona wazi kwamba siku Sokoine anaapishwa kuwa raisi basi milango ya jela ilikuwa wazi kwao, pamoja na wale ambao Sokoine alitaka kuwakamata na Nyerere akamzuia.
Kwa mfano, akihutubia Bunge pale Dodoma kabla ya kuanza safari ambayo ilimuua, Sokoine alikuwa ameweka ahadi kwamba akifika Dar es Salaam, alikuwa na list ya viongozi ambao walitakiwa kutupwa kikaangoni. Inaonekana Sokoine alitaka kwanza kuijadili ile list na Nyerere. Ndipo watu wanasema, akaliwa timing hata huko Dar es Saalam asifike.
Sasa katika mazingira ya ile ajali, ambayo kimsingi hayakuwa ya "head-on collision", Mercedes Benz walidai kwa maelezo yaliyotolewa juu ya ajali ilivyotokea, Sokoine hakupswa kufa. Na wakaenda mbali zaidi na kusema, wanataka walete wataalamu wao ili wachunguze, kama ni kweli Sokoine alikufa akiwa ndani ya gari yao ya Mercedes Benz, akiwa amekaa kiti cha nyuma, na kwa nini alikufa.
Sasa kumbuka gari aliyopata nayo ajali Sokoine ilikuwa customized na Mercedes Benz kwa ajili ya viongozi, yaani order za ikulu, kwa hiyo huwa zinatengenezwa maalumu kuwa na usalama zaidi kuliko gari ya kawaida. Kwa hiyo kwa Mercedes Benz hili la kusema Sokoine alikufa katika mazingira ya ajali kama ile, waliona ni kuchafua jina lao. Wakaomba waje kufanya uchunguzi, serikali ikawakatalia.
Sasa unajiuliza, kulikuwa na siri gani nyuma ya kifo cha Sokoine ambacho serikali ya Nyerere haikutaka zivuje? Kumbuka, Nyerere alikuwa ni aina ya kiongozi ambaye hata angejua Sokoine ameuwawa, asingetaka ulimwengu ujue hilo. Kwake hadhi na heshima ya Tanzania vilikuwa vitu muhimu sana, na alikuwa tayari kutotoa ukweli wa jambo kama hilo ambalo aliona lingelifedhehesha taifa la Tanzania.
Kwa mfano, kuna kikundi kilimfuata Nyerere na kumwambia Mwalimu, Sokoine ameuwawa katika mazingira ya ushirikina, kachukuliwa msukule na wanajua nani walifanya hivyo katika viongozi wa taifa. Wakasema wanaweza kabisa kumrudisha hai Sokoine ikiwa watamuwahi kabla hajamalizwa kabisa! Nyerere akasema, mie naamini kabisa haya mambo ya msukule na najua yanafanyika. Na huenda ni kweli Sokoine kafanyiwa hivyo. Lakini sasa niambieni, mie baada ya kuutangazia ulimwengu kwamba kijana wangu Sokoine amekufa, na nyie mkamrudisha, nitatoa tangazo gani jingine kwa ulimwengu, na huo ulimwengu utanionaje mimi na Tanzania kwa ujumla? Akasema kama mnataka kunisaidia, basi kama hajafa bado ni msukule, fanyeni afe kabisa ili hao waliomfanyia haya wasije wakamtesa.
Kwa kumkumbuka Sokoine, hebu jiulize, ikiwa leo Sokoine kwa muujiza fulani angefufuka na kuwa Raisi wa Tanzania, ni nani katika viongozi wetu waliopo madarakani milango ya jela ingefunguliwa kwa ajili yao?
View attachment 2967287