Kifo cha Sokoine: Watoto wake wataka mwili uchunguzwe kubaini kama alikufa kwa ajali au la!

View attachment 2967288

Angalia hii picha. Gari imegongwa pembeni, Sokoine alikuwa kiti cha nyuma. Hakuna mtu mwingine kwenye gari hii alikufa ila Sokoine tu

Ukiwa dereva maalum wa viongozi, ukaona gari inaingia barabarani bila tahadhari, hutagongwa squarely pembeni, utabalalizwa katika kuikwepa na labda mtaishia porini. Hii ni ajali ambayo Dube alipaswa kuwa anakatiza barabara sio anaingia barabarani. Labda walioitengeneza hawakufikiria hilo
Umesema sokoine alikuwa msukule😄😄😄😄😄miso misondo ulipigaje pale....
 
Huwa namwambia Max Mello watu kama wewe hawastahili kuwa humu JF, lakini najua hana la kufanya
Mimi huwa najua story za wavuta bangi jamii forum nazo zina haki ila zikishidisha uongo wa kitoto kam huo lazima tusema shida unahisi wote ni watu wa vijiweni

Eti nyerere akasema mkirudisha msukule dunia itanionaje .....hivi unafikir nyerere alikuwa pomole kama wewe eti aamini mambo ya misukule
 
Kuna sababu zilizofanya watu wamshuku Rashidi. Ni kweli Sokoine alimwona Rashidi kuwa nae ni fisadi tu. Inasemekana wakati kina Rashidi wanalalamika sana kwa Nyerere dhidi ya Sokoine kwamba anapita kiasi, Nyerere aliwaambia sasa nyie pia si viongozi, kama mnaona anapita kiasi mdhibitini. Watu wanasema Rashidi alikuja sema "uliposema tumdhibiti sie tulijua unamaanisha...." Sasa sijui kama ni kweli.

Ninachokumbuka ni kwamba, baada ya kifo cha Sokoine, Nyerere hakutaka kabisa kumwona Rashidi. Rashidi aliomba sana lakini ilichukua muda mrefu kabla ya Nyerere kukubali kukutana nae.
Kuna kijarida nilikikuta Library pale Nairobi Unv. hivyo yule mkwe wangu wa upareni Msuya alisingiziwa tu😂
 
Acha kupayuka. Nyerere hakuwa mkomunisti. Hujui hata maana ya mkomunist unakuja kupiga kelele hapa. Na kwa taarifa yako, kuna wakati wazee wa Dar es Salaam walimwambia Nyerere wampeleke Bagamoyo Mlingotini akafanyiwe "huduma" na wazee wa Bagamoyo, alikubali. Kwa hiyo Nyerere alikuwa na akili kuliko uwezo wako wa kufikiri
Na huko bagamoyo ndo alipopewa wazo la mwenge wa uhuru. Wewe mzee umeiva sana kwenye historia.
 
Mwaka huu kumekuwa na kumbikizi ya miaka 40 ya kifo cha Edward Sokoine, ambacho kiligubikwa na utata mkubwa, kukiwa na madai kwamba hakufa kwa ajali bali aliuwawa na watu ndani ya uongozi ambao walimwogopa sana.

Huenda ni kweli, kwa sababu wakati fulani Sokoine alitaka kumweka nguvuni kiongozi wa juu sana serikalini kwa kosa la ufisadi, na Nyerere ndio alimzuia akimwambia angesababisha mgogoro mkubwa wa kiuongozi. Sokoine alikubali, japo kwa shingo upande.

Hata hivyo, wakati Nyerere akiongelea kung'atuka na ikionekana wazi mrithi wa Nyerere angekuwa Sokoine, kuna viongozi walishikwa na uoga mkubwa juu ya hatima zao. Wengi waliona wazi kwamba siku Sokoine anaapishwa kuwa raisi basi milango ya jela ilikuwa wazi kwao, pamoja na wale ambao Sokoine alitaka kuwakamata na Nyerere akamzuia.

Kwa mfano, akihutubia Bunge pale Dodoma kabla ya kuanza safari ambayo ilimuua, Sokoine alikuwa ameweka ahadi kwamba akifika Dar es Salaam, alikuwa na list ya viongozi ambao walitakiwa kutupwa kikaangoni. Inaonekana Sokoine alitaka kwanza kuijadili ile list na Nyerere. Ndipo watu wanasema, akaliwa timing hata huko Dar es Saalam asifike.

Sasa katika mazingira ya ile ajali, ambayo kimsingi hayakuwa ya "head-on collision", Mercedes Benz walidai kwa maelezo yaliyotolewa juu ya ajali ilivyotokea, Sokoine hakupswa kufa. Na wakaenda mbali zaidi na kusema, wanataka walete wataalamu wao ili wachunguze, kama ni kweli Sokoine alikufa akiwa ndani ya gari yao ya Mercedes Benz, akiwa amekaa kiti cha nyuma, na kwa nini alikufa.

Sasa kumbuka gari aliyopata nayo ajali Sokoine ilikuwa customized na Mercedes Benz kwa ajili ya viongozi, yaani order za ikulu, kwa hiyo huwa zinatengenezwa maalumu kuwa na usalama zaidi kuliko gari ya kawaida. Kwa hiyo kwa Mercedes Benz hili la kusema Sokoine alikufa katika mazingira ya ajali kama ile, waliona ni kuchafua jina lao. Wakaomba waje kufanya uchunguzi, serikali ikawakatalia.

Sasa unajiuliza, kulikuwa na siri gani nyuma ya kifo cha Sokoine ambacho serikali ya Nyerere haikutaka zivuje? Kumbuka, Nyerere alikuwa ni aina ya kiongozi ambaye hata angejua Sokoine ameuwawa, asingetaka ulimwengu ujue hilo. Kwake hadhi na heshima ya Tanzania vilikuwa vitu muhimu sana, na alikuwa tayari kutotoa ukweli wa jambo kama hilo ambalo aliona lingelifedhehesha taifa la Tanzania.

Kwa mfano, kuna kikundi kilimfuata Nyerere na kumwambia Mwalimu, Sokoine ameuwawa katika mazingira ya ushirikina, kachukuliwa msukule na wanajua nani walifanya hivyo katika viongozi wa taifa. Wakasema wanaweza kabisa kumrudisha hai Sokoine ikiwa watamuwahi kabla hajamalizwa kabisa! Nyerere akasema, mie naamini kabisa haya mambo ya msukule na najua yanafanyika. Na huenda ni kweli Sokoine kafanyiwa hivyo. Lakini sasa niambieni, mie baada ya kuutangazia ulimwengu kwamba kijana wangu Sokoine amekufa, na nyie mkamrudisha, nitatoa tangazo gani jingine kwa ulimwengu, na huo ulimwengu utanionaje mimi na Tanzania kwa ujumla? Akasema kama mnataka kunisaidia, basi kama hajafa bado ni msukule, fanyeni afe kabisa ili hao waliomfanyia haya wasije wakamtesa.

Kwa kumkumbuka Sokoine, hebu jiulize, ikiwa leo Sokoine kwa muujiza fulani angefufuka na kuwa Raisi wa Tanzania, ni nani katika viongozi wetu waliopo madarakani milango ya jela ingefunguliwa kwa ajili yao?

View attachment 2967287
Wewe Mpumbavu unaleta mambo ya kufufua misukule hapa!
Wapi maiti alifufuka?
 
1713440635115.png

1713440776562.png
 
Na huko bagamoyo ndo alipopewa wazo la mwenge wa uhuru. Wewe mzee umeiva sana kwenye historia.
Asee wewe nchi nyingi dunia zina national torch mbona mnapenda habari za kufikirika sana national torch hadi uingereza wali wahi kuwa nao
 
Mwaka huu kumekuwa na kumbikizi ya miaka 40 ya kifo cha Edward Sokoine, ambacho kiligubikwa na utata mkubwa, kukiwa na madai kwamba hakufa kwa ajali bali aliuwawa na watu ndani ya uongozi ambao walimwogopa sana.

Huenda ni kweli, kwa sababu wakati fulani Sokoine alitaka kumweka nguvuni kiongozi wa juu sana serikalini kwa kosa la ufisadi, na Nyerere ndio alimzuia akimwambia angesababisha mgogoro mkubwa wa kiuongozi. Sokoine alikubali, japo kwa shingo upande.

Hata hivyo, wakati Nyerere akiongelea kung'atuka na ikionekana wazi mrithi wa Nyerere angekuwa Sokoine, kuna viongozi walishikwa na uoga mkubwa juu ya hatima zao. Wengi waliona wazi kwamba siku Sokoine anaapishwa kuwa raisi basi milango ya jela ilikuwa wazi kwao, pamoja na wale ambao Sokoine alitaka kuwakamata na Nyerere akamzuia.

Kwa mfano, akihutubia Bunge pale Dodoma kabla ya kuanza safari ambayo ilimuua, Sokoine alikuwa ameweka ahadi kwamba akifika Dar es Salaam, alikuwa na list ya viongozi ambao walitakiwa kutupwa kikaangoni. Inaonekana Sokoine alitaka kwanza kuijadili ile list na Nyerere. Ndipo watu wanasema, akaliwa timing hata huko Dar es Saalam asifike.

Sasa katika mazingira ya ile ajali, ambayo kimsingi hayakuwa ya "head-on collision", Mercedes Benz walidai kwa maelezo yaliyotolewa juu ya ajali ilivyotokea, Sokoine hakupswa kufa. Na wakaenda mbali zaidi na kusema, wanataka walete wataalamu wao ili wachunguze, kama ni kweli Sokoine alikufa akiwa ndani ya gari yao ya Mercedes Benz, akiwa amekaa kiti cha nyuma, na kwa nini alikufa.

Sasa kumbuka gari aliyopata nayo ajali Sokoine ilikuwa customized na Mercedes Benz kwa ajili ya viongozi, yaani order za ikulu, kwa hiyo huwa zinatengenezwa maalumu kuwa na usalama zaidi kuliko gari ya kawaida. Kwa hiyo kwa Mercedes Benz hili la kusema Sokoine alikufa katika mazingira ya ajali kama ile, waliona ni kuchafua jina lao. Wakaomba waje kufanya uchunguzi, serikali ikawakatalia.

Sasa unajiuliza, kulikuwa na siri gani nyuma ya kifo cha Sokoine ambacho serikali ya Nyerere haikutaka zivuje? Kumbuka, Nyerere alikuwa ni aina ya kiongozi ambaye hata angejua Sokoine ameuwawa, asingetaka ulimwengu ujue hilo. Kwake hadhi na heshima ya Tanzania vilikuwa vitu muhimu sana, na alikuwa tayari kutotoa ukweli wa jambo kama hilo ambalo aliona lingelifedhehesha taifa la Tanzania.

Kwa mfano, kuna kikundi kilimfuata Nyerere na kumwambia Mwalimu, Sokoine ameuwawa katika mazingira ya ushirikina, kachukuliwa msukule na wanajua nani walifanya hivyo katika viongozi wa taifa. Wakasema wanaweza kabisa kumrudisha hai Sokoine ikiwa watamuwahi kabla hajamalizwa kabisa! Nyerere akasema, mie naamini kabisa haya mambo ya msukule na najua yanafanyika. Na huenda ni kweli Sokoine kafanyiwa hivyo. Lakini sasa niambieni, mie baada ya kuutangazia ulimwengu kwamba kijana wangu Sokoine amekufa, na nyie mkamrudisha, nitatoa tangazo gani jingine kwa ulimwengu, na huo ulimwengu utanionaje mimi na Tanzania kwa ujumla? Akasema kama mnataka kunisaidia, basi kama hajafa bado ni msukule, fanyeni afe kabisa ili hao waliomfanyia haya wasije wakamtesa.

Kwa kumkumbuka Sokoine, hebu jiulize, ikiwa leo Sokoine kwa muujiza fulani angefufuka na kuwa Raisi wa Tanzania, ni nani katika viongozi wetu waliopo madarakani milango ya jela ingefunguliwa kwa ajili yao?

View attachment 2967287
Kwenye ajali,mtu anaweza kufa hata kwa mshtuko,asiguswe hata na machumachuma.
 
Nyie watoto wa 2000 hamuwezi kuelewa, hamkuwepo tatizo.
Shida yenu majinga sana nyie unaongea hapa na mtu wa mwaka 85 usijafanye watoto wa 2000.....

Majinga kama nyinyi ndo husambaza mila potofu taifa linaendelea kuwa masikini kwa kwa amini mambo ya kijinga jinga

Mbaya zaidi unakuta hadi wasomi na viongozi wanaamini kwenye ushirikina
 
Kwenye ajali,mtu anaweza kufa hata kwa mshtuko,asiguswe hata na machumachuma.
Kweli kabisa. Mshituko, na ukiwa na tatizo la BP na umri mkubwa ndio kabisa. Ila usisahau Sokoine alikuwa na miaka 45 tu, kijana bado si rahisi kufa kwa mshituko tu
 
Nyerere Aaamini misukule😄😄😄😄😄mcommunist na mambo ya mitaani wapi na wapi ......uzi una kamba huuu
Lete wewe ukweli wako,ingia kwenye kumbukumbu za Mercedes Benz,ni kweli walitaka kutuma wataalamu wao kuchunguza ajali hii maana iliharibu brand yao,angalia picha hiyo ya ajali,hapo dereva hakupata majeraha makubwa,na kweli huyu Dube a ignore kwanza yule traffic kwenye motorcycle anaye clear njia,then apuuzie leading car na aje agongane na gari iliyombeba main subject!,na wale tiss ya gari iliyokua nyuma ya main car hawakuchukua action yeyote ya ku defend main car!elewa msafara unakuaga sio wa straight line,LAZIMA main car iwe ndani ya curve,bodyguards car na leading car ndizo zinakua in a straight line,ukweli unatakiwa hapa....ule mchanganyuo wa mwenye heri umeishia wapi?
 
Mimi huwa najua story za wavuta bangi jamii forum nazo zina haki ila zikishidisha uongo wa kitoto kam huo lazima tusema shida unahisi wote ni watu wa vijiweni

Eti nyerere akasema mkirudisha msukule dunia itanionaje .....hivi unafikir nyerere alikuwa pomole kama wewe eti aamini mambo ya misukule
Acha kuonyesha upumbavu wako. Watafute watoto wa Nyerere watakuambia ukweli
 
Kuna kijarida nilikikuta Library pale Nairobi Unv. hivyo yule mkwe wangu wa upareni Msuya alisingiziwa tu😂
Mkwe wako Msuya alikuwa top adui wa Sokoine. In fact Sokoine alitaka awekwe ndani kwa ufisadi. Kama sio Nyerere mkwe wako angewekwa ndani. Nadhani kumridhisha Sokoine, Nyerere alikubali kumvua Msuya u-PM. Sasa hao ndio walikuwa aina ya watu Sokoine went after, kina Msuya, kina Kawawa, na Nyerere akawa anamwambia taratibu, utaleta mgongano mkubwa nchini! Na hao ndio watu walikuwa wanamwambia Nyerere Sokoine adhibitiwe, anavuka mipaka!

Na kama ni kweli kifo cha Sokoine kilichorwa, basi tutahisi hao ndio watu walikichora. Umeona hii hapa chini

1713442210057.png
 
Back
Top Bottom