Kwanza kabisa naomba ku-declare interest..mimi siyo mpenzi wa Bongo Movies ila natambua kwamba Bongo movies imeshika katika vichwa vya watanzania wengi ambao kwa asilimia kubwa hawawezi kuangalia even Nigerian (tupa kule american) na wakaelewa..natambua kuwa kuna watu ambao haziwezi kupita walau siku mbili bila kuangalia hizi movie za nyumbani kwetu. Watu hawa wapo wengi kuliko unavyoweza kufikiri na ni kama ilivyo kwangu isivyowezekana kupita siku mbili bila kusoma kitabu chochote au kufuatilia politics!. Lengo la kusema haya awali ni kutaka kuonesha kwamba kama binadamu..kuna wanaopenda vitu fulani fulani il-hali vitu hivyo hivyo wengine hawataki kusikia..ndio maana kuna watu humu JF huwaambii kitu kwa CHADEMA,CCM or even CUF.Ndiyo maana vidole kwenye mikono,miguu ni vitano lakini havilingani..vikilingana.... you can imagine the situation!
Back to the topic, suala hili ambalo limeenea kwa 'the so called' wanaoweza kufikiri na kupambanua i.e great thinkers kwamba watu waliojitokeza kuhudhuria msiba wa Steve Kanumba (R.I.P) ni wajinga,punguani ambao hawana kazi za kufanya limenisikitisha sana.
Nataka kuwarudisha nyuma si chini ya miaka miwili iliyopita ya kifo kilichotokea cha Mtu Mweusi mwenye mbwembwe nyingi..Michael Jackson a.k.a Wacko Jacko. Wamarekani walilala nje ya Mjengo wa Wacko Jacko,ulaya,asia watu walikusanyika open spaces kote huko.. Watu walifunga barabara za mitaa mbali mbali marekani kwa ajili ya kuomboleza..CNN, BBC,Al-Jazeera etc etc walikatisha program zote za Ki-uchumi,kisiasa etc etc ili kucover tukio la kifo cha Wacko Jacko..Tena siyo kwa siku moja..ni kama wiki 2 mfululizo na zaidi na zaidi..! Ndugu zangu akina Masanilo and co., niwaulize hivi hawa hawataki maendeleo ya ki-uchumi?? Wao hawakuwa na kazi za kufanya?.
Je Nyerere alivyokufa watu wakajitokeza barabarani, shughuli za kiuchumi etc etc zikasimama, watu hawakuwa na kazi za kufanya?. Wanasiasa wanapokuwa mahali na kukusanya Lundo la watu (tumeona Zitto kirumba, Mbowe & co Arusha, Barack Obama alipoenda Ujerumani etc etc) wale wahudhuriaji wanakuwa hawana la kufanya?. Tofauti ya matukio haya ni kwamba moja ni msiba jingine ni politics..lakini uhudhuriaji waweza kushabihiana.
Guys, Funguka...usidhani kila unachokifikiri wewe ndio kila mtu afanye..! Kanumba was a celebrity, hata baadhi ya watu hapa wakifa na ikajulikana given the fact kwamba wao ndani ya JF ni Celebrities (I cant mention names,but I know even these guys amongst them ar celebrities within JF)..Quote my words,asilimia kubwa za Post zitawaongelea wa0, mara oh, tutengeneze t-shirt,tujitokeze msibani kwa wingi, alikuwa mtu mzuri etc etc!
Cha msingi ni kutambua kila mmoja ana uhuru wa kufanya yale anayotaka kuyafanya kwa muda wake yeye mwenyewe kadiri anavyoona inafaa. Ndio maana mimi hata sijaangalia wala kufuatilia popote hiyo Live coverage zaidi ya kuingia JF jioni hii na kupata news..it is enough for me! Lakini kuna watu leo ofisini, kwenye biashara zao, kwenye mashamba yao etc etc kulikuwa hakukaliki wakitaka kufuatilia Kanumba anazikwaje kwa kuhudhuria wao wenyewe,kupitia radio,TV au hata internet.
Everything is about Choices, and we must not envy others choices or even mock their choices because definitely they will mock ours, it is simple..they are not theirs. He was great to them, they chose him to be like that, it is not for you, you chose otherwise ..dont mock their choices!
Alamsyk.