Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

MSANII Elizabeth Michael (Lulu) Leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashitaka ya mauwaji yanayomkabili dhidi ya Steven Kanumba.
Leo hakutakiwa kujibu lolote, kesi imeahirishwa hadi Aprili 24 mwaka huu, amerudishwa rumade kutokana na kesi za mauaji hazina dhamana. Ungana nasi baadaye kwa habari zaidi.

Kutoka Mwananchi website
 
lulu.jpgni kweli
 
Aulizwe mdogo wake nadhani na yeye alitakiwa kushikiliwa kwa wema ili kuisaidia polisi coz mkemia akisema ni sumu then itakuwaje na yeye ndiye aliyekuwa naye before?
May be na polisi wana clue muhimu hapa ndio maana wanamshikilia LULU pekee.
 
kesi ni ushahidi, upande utakaokuwa na strong evidence to defend their arguments utashinda, tusubiri
 
mmhh wanamuonea dogo coz unaweza kuta yeye hana makoza unaweza kuta ilikua ni mipango ya mungu au siku zake za kuishi hapa duniani zimeisha
 
Mbona wengi sana wanamshuku huyu mdogo wake?...mnakaribia kunipandikiza hisia za aina hiyo na mimi!

mkuu hapo ku question behind the curtain. Kama huyu ndiye aliyekuwa naye kabla LULU hajaja imekuwaje yeye asiwe na something to say or write down kule polisi?
Kwanini suspect awe mmoja wakati walikuwa watatu? Huo ndo wasiwasi kwa upande wangu halafu unagnisha na povu mdomoni na kinywaji je, mkemia akisema ni sumu tutamsuspect nani Lulu au huyu aliyekuwepo kabla?
 
kasomewa mashitaka leo kwa hisani ya blog ya issa michuzi kama kuna mtu anajua kuweka link saidia


BREAKING NYUZZZZZ........Elizabeth Michael a.k.a Lulu apandishwa kizimbani leo kusomewa mashtaka yake kufuatia kuhusika na kifo cha Kanumba

Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.



Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.



Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.



Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.



Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

Mkuu mbona michango mingine inasema kesi imeahirishwa hadi april 24, wewe unasema april 23? ipi ni sahihi?
 
Unafikiri watu wanaoharibikiwa wamekosa malezi ya baba na au mama? Si kweli. Usiwe na papara kutoa judgement kwa watoto wa wenzako ilhali na wewe unao au wanakuja. That is her destiny. Angekuwa na uwezo amgerudisha nyuma mkanda na kuanza upya. After all, life has to go on!
 
was just jokng,
kwanza hua siamin hayo mambo, ngoja 2subir atasemaje,
ila mi nimezoea 'mama ni mama'
baba ni baba am nt sure
 
MSANII Elizabeth Michael (Lulu) Leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashitaka ya mauwaji yanayomkabili dhidi ya Steven Kanumba.
Leo hakutakiwa kujibu lolote, kesi imeahirishwa hadi Aprili 24 mwaka huu, amerudishwa rumade kutokana na kesi za mauaji hazina dhamana. Ungana nasi baadaye kwa habari zaidi.

Kutoka Mwananchi website

kesi imeahirishwa hadi April 24 au 23?
 
Back
Top Bottom