Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kanumba alipewa sumu muda mrefu kabla, pengine jioni ile alipotoka matembezi (au kazini) na labda siku moja au mbili kabla.

Lulu kwa kuwa alikuwa na mahusiano ya karibu alitumwa kwenda kuangalia effect ya kilo alichopewa huyo mnayemuita 'the great,' maana jamaa aliyeleta hiyo kitu kutoka Nairobi si ajabu aliwaingiza mjini

Kwa kuwa kabinti ni kichwa hewa kalienda tu kama zuzu na kalipokuwa huku jamaa kwa mchecheto wakata kujua hali ya kanumba kupitia simu ambazo Lulu aliogopa kuzijibu akihofu mhusika kusikia kuwa alikuwa anaongea na mmoja wa maadui zake.

Na hakika Kanumba alipofanikiwa kuipokonya Simu ya Lulu akagundua kuwa binti alikuwa anateta na adui yake mkuu, yaani Mr X.

"Yaani huyu ndiye ......!" akakata kauli na kuanguka maana dawa ilikwisha kuchukua effect.
 
Polisi wetu sijui wanafundishwa kitu gani bwana?! Watu wa kuisaidia polisi wako wengi lakini anashikiliwa mmoja tu nini maanake? Mimi na ki-course changu cha advanced security in the field naona kabisa Seth anapaswa kuombolezea cell na Ray siyo wa kubaki mitaani! Lazima waisaidie polisi period!! Nîliwahi kufokeana na OCD mmoja shauri ya upelelezi wa kijinga kama huu unaotaka kufanyika kwa SCK! Nyamb..f kabisa hawa!
 
View attachment 51535

mapaparazi hawakosi kitu mkuu wangu.

kasomewa mashitaka leo kwa hisani ya blog ya issa michuzi kama kuna mtu anajua kuweka link saidia


BREAKING NYUZZZZZ........Elizabeth Michael a.k.a Lulu apandishwa kizimbani leo kusomewa mashtaka yake kufuatia kuhusika na kifo cha Kanumba

Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.



Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.



Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.



Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.



Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.
 
NN,

Anaonekana bado anang'aa eeh! na tulishazoea mtu akiingia rumande hata siku mbili tu akitoka hafai.

Ooh yeah....kanang'aa kweli kweli. Sasa najiuliza kama huko jela wanaruhusiwa kuwa na make-up, kutumia simu (manake kuna taarifa kuwa kuna watu walikuwa wanawasiliana naye kwa njia ya text messages), na kadhalika.

Hata nywele zake zipo freshi na sio tim tim kama za Wema enzi zile alipotoka Segerea
 
Anashtakiwa kwa kosa la Mauaji:
  1. Anatuhumiwa kwa Kumpiga Marehemu kwa kitu kizito kilichosababisha ubongo kutikisika na hatimaye kifo
  2. Anatuhumiwa kwa kosa la kukimbia baada ya kutekeleza mauaji ya Kanumba
 
RPC wa Kinondoni amenukuliwa na Daily News 10.April 2012 akieleza kuwa chupa ya whisky, sprite, na panga ni miongoni mwa vitu vilivyochukuliwa kutoka chumbani kwa kanumba ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa kifo cha msanii huyo nguli, lulu anauguza majeraha madogo aliyopata kutokana na panga hilo, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo sehemu za siri

Imekaaje hii wakuu, kanumba alitaka kuchinja mtu kwa wivu wa mapenzi?
 
Haya ni maswala ya 'kifamilia' ya kina kanumba.
Sisi wengine tuendelee na shughuli zetu...
 
View attachment 51534

Wadau kama kuna mwenye fununu kuwa Lulu alikuwa anoongea na nani kwenye simu amwage mambo pwaaaaaaaa hapa kuna tetesi mtaani kuwa alikuwa anazungumza na waziri fulani na alipobanwa na kanumba akamtaja...unaambiwa kanumba kusiia hilo jina hakaishiwa nguvu hapo hapo inawezekana huyo waziri ndo chanzo mtajeni jameni tumkamate.....

Mhhhhhhhhhhh! kama siyo Malima sijui
 
Alichoeleza Lulu polisi hiki hapa
Mwandishi Wetu
MSANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi
kuwa kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifanyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.

Habari zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa,Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumzana simu kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake.

"Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo Kanumba akamfokea nandiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje nakuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari waKanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali.

"Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha PolisiOysterbay kuchukua PF3," kilisema chanzo hicho.

Chanzo kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivuasiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi.

Katika hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baadaya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba,walioandamana wakidai wanamtaka Lulu.

"Tunataka jembe letu", waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokeaBarabara ya Ali Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askariwaliokuwapo kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaakutuliza ghasia kama zingezuka.

Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayarikupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Patricia Kimelemetaanaripoti kuwa,
Msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa mahakamanileo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba. Kamanda wa PolisiMkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili jana kuwa Luluatafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mara baada ya polisikupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa Serikali.

"Tunasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu kubaini chanzo cha kifo hicho kwa sababuwamechukua baadhi ya sampuli za marehemu kwenda kupima na kwamba tutakabidhiwaleo(jana). Kimsingi tukipata tu taarifa hiyo tutamfikisha mahakamani," alisemaKenyela.

Aliongeza ripoti hiyo itaweza kuwasaidia kuandika mashtaka ili yawezekufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.

Kamanda Kenyela alisema kuwa, ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwambaimeonyesha kuwa Kanumba amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.

Msanii Stephen Kanumba alifariki usiku wa Ijumaa Kuu.

- Chanzo: Mwananchi Aprili 11

Ni Nani Huyo?
 
rpc wa kinondoni amenukuliwa na daily news 10.april 2012 akieleza kuwa chupa ya whisky, sprite, na panga ni miongoni mwa vitu vilivyochukuliwa kutoka chumbani kwa kanumba ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa kifo cha msanii huyo nguli, lulu anauguza majeraha madogo aliyopata kutokana na panga hilo, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo sehemu za siri

imekaaje hii wakuu, kanumba alitaka kuchinja mtu kwa wivu wa mapenzi?

ukisikia umbea usiokua na kikomo ndiyo huu
 
"Elizabeth Hakutakiwa kujibu
chochote Mahakamani hapo kwani
mahakama hii haina mamlaka ya
kusikiliza kesi za mauaji"

Kwani hawakujua kwamba mahakama hii haisikilizi kesi za mauaji? Mis use of resources na time! Kwanin wasiipeleke moja kwa moja kwenye level husika?
 
Kwanini unasema muongo?una uhakika gan hana miaka 17?ww ndo mzazi wake?mama ake ametoa vyeti vinadhibitisha kua ana miaka 17 sasa mnabisha nini
 
Back
Top Bottom