Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I am shocked kwa kweli... kila kukicha watu wanajisemea tu wanacho taka.
Anashtakiwa kwa kosa la Mauaji:
- Anatuhumiwa kwa Kumpiga Marehemu kwa kitu kizito kilichosababisha ubongo kutikisika na hatimaye kifo
- Anatuhumiwa kwa kosa la kukimbia baada ya kutekeleza mauaji ya Kanumba
kasomewa mashtaka ya mauaji ya kukusudia.Karudishwa segerea kesi itasikilizwa tena baada ya wiki 2.
Zamu ya Polisi sasa kula utamu...
My story baada ya kusikia stori tofauti tofauti za Lulu na Sethi, mdogo wake Kanumba, kwa mtazamo wangu inaonekana stori halisi iko hivi:
Kanumba alimpigia simu Lulu aje watoke out. Akamtaarifu na mdogo wake ajiandae. Mdogo wake akajiandaa. Lulu akaja. Akiwa hapo kwa Kanumba akapigiwa simu/ akatumiwa meseji na mwanaume mwingine (huyo mbongo fleva) akimtaka waonane. Lulu akaanza kutoa visingizio kuwa hataki kwenda tena 'club' bali anataka kurudi nyumbani.
Kanumba akawa na wasiwasi ni kwa nini atake tena kurudi nyumbani wakati ashafika kwake! Mzozo ukatokea. Wakati bado wakiwa katika mzozo Lulu akapigiwa simu tena na huyo mwanaume kumtaarifu kuwa kafika hapo kumpick. Lulu akapokea hiyo simu mbele ya Kanumba lakini akaanza kuongea huku akitoka nje.
Kanumba akawa ashaelewa nini kinaendelea. Akamfuata kwa hasira na kumrudisha ndani kisha kufunga mlango. Zikaanza purukushani za kugombania funguo kutoka nje. Katika hizi purukushani Kanumba akaanguka (maybe kwa kusukumwa au kuteleza). Lulu akapata chance ya kufungua mlango na kutoka.
Hapo nje akamwamwambia Sethi kuwa kakako yuko kadondoka huko chumbani, kwa sababu tayari alikuwa na wasiwasi kuwa Kanumba kaumia sana. Akapanda gari lililokuwa linamsubiri hapo nje akaondoka. Sethi akaenda kumcheki kaka yake akampigia daktari. ...........
we jamaa umenishtua,
nilijua utanitaja...
kasomewa mashitaka leo kwa hisani ya blog ya issa michuzi kama kuna mtu anajua kuweka link saidia
BREAKING NYUZZZZZ........Elizabeth Michael a.k.a Lulu apandishwa kizimbani leo kusomewa mashtaka yake kufuatia kuhusika na kifo cha Kanumba
Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.
Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.
Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.
Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.
The Public has formed an opinion, but opinion so formed can be overturned to the advantage of the accused.The substantial pretrial publicity of this case may prevent her from getting a fair trial.
Kanumba alipewa sumu muda mrefu kabla, pengine jioni ile alipotoka matembezi (au kazini) na labda siku moja au mbili kabla.
Lulu kwa kuwa alikuwa na mahusiano ya karibu alitumwa kwenda kuangalia effect ya kilo alichopewa huyo mnayemuita 'the great,' maana jamaa aliyeleta hiyo kitu kutoka Nairobi si ajabu aliwaingiza mjini
Kwa kuwa kabinti ni kichwa hewa kalienda tu kama zuzu na kalipokuwa huku jamaa kwa mchecheto wakata kujua hali ya kanumba kupitia simu ambazo Lulu aliogopa kuzijibu akihofu mhusika kusikia kuwa alikuwa anaongea na mmoja wa maadui zake.
Na hakika Kanumba alipofanikiwa kuipokonya Simu ya Lulu akagundua kuwa binti alikuwa anateta na adui yake mkuu, yaani Mr X.
"Yaani huyu ndiye ......!" akakata kauli na kuanguka maana dawa ilikwisha kuchukua effect.
Du mod wamelikubali jina lako? Nakumbuka best yako kifili walili-modify jina lake!
Ooh yeah....kanang'aa kweli kweli. Sasa najiuliza kama huko jela wanaruhusiwa kuwa na make-up, kutumia simu (manake kuna taarifa kuwa kuna watu walikuwa wanawasiliana naye kwa njia ya text messages), na kadhalika.
Hata nywele zake zipo freshi na sio tim tim kama za Wema enzi zile alipotoka Segerea