Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Anashtakiwa kwa kosa la Mauaji:
  1. Anatuhumiwa kwa Kumpiga Marehemu kwa kitu kizito kilichosababisha ubongo kutikisika na hatimaye kifo
  2. Anatuhumiwa kwa kosa la kukimbia baada ya kutekeleza mauaji ya Kanumba

Mungi hayo ndio mashitaka yake? Kama ndio baaasiii jela maisha!
 
Mimi siongelei hatima ya hukumu. Ila huyo mtoto lulu amevuka mipaka ya maadili.

Ndege mjanja hunasa kwenye tope... Na asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na polisiii.....

Miaka 18 anachanganya wanaume kama kachumbari....duh
"Eti nilikua kwenye simu naongea na mpenzi wangu mwingine"

Huyo mtoto kila siku kwenye magazeti, anaongelea mapenzi... Hivi alikua anaenda shule kweli??? Au ndo u_super star huo????

Mimi naona iwe fundisho kwa watoto wote ambao wanaharakia maisha. Pia mi_baba mnaopenda toto dogo dogo, "muache"...wazazi pia, muwalee watoto katika mazingira na maadili ya kiTanzania... Haya ndo madhara ya kutoka kuishi kama Marekani...

Ni hayo tuuu
 
kasomewa mashtaka ya mauaji ya kukusudia.Karudishwa segerea kesi itasikilizwa tena baada ya wiki 2.
Zamu ya Polisi sasa kula utamu...

Du mod wamelikubali jina lako? Nakumbuka best yako kifili walili-modify jina lake!
 
My story baada ya kusikia stori tofauti tofauti za Lulu na Sethi, mdogo wake Kanumba, kwa mtazamo wangu inaonekana stori halisi iko hivi:

Kanumba alimpigia simu Lulu aje watoke out. Akamtaarifu na mdogo wake ajiandae. Mdogo wake akajiandaa. Lulu akaja. Akiwa hapo kwa Kanumba akapigiwa simu/ akatumiwa meseji na mwanaume mwingine (huyo mbongo fleva) akimtaka waonane. Lulu akaanza kutoa visingizio kuwa hataki kwenda tena 'club' bali anataka kurudi nyumbani.

Kanumba akawa na wasiwasi ni kwa nini atake tena kurudi nyumbani wakati ashafika kwake! Mzozo ukatokea. Wakati bado wakiwa katika mzozo Lulu akapigiwa simu tena na huyo mwanaume kumtaarifu kuwa kafika hapo kumpick. Lulu akapokea hiyo simu mbele ya Kanumba lakini akaanza kuongea huku akitoka nje.

Kanumba akawa ashaelewa nini kinaendelea. Akamfuata kwa hasira na kumrudisha ndani kisha kufunga mlango. Zikaanza purukushani za kugombania funguo kutoka nje. Katika hizi purukushani Kanumba akaanguka (maybe kwa kusukumwa au kuteleza). Lulu akapata chance ya kufungua mlango na kutoka.

Hapo nje akamwamwambia Sethi kuwa kakako yuko kadondoka huko chumbani, kwa sababu tayari alikuwa na wasiwasi kuwa Kanumba kaumia sana. Akapanda gari lililokuwa linamsubiri hapo nje akaondoka. Sethi akaenda kumcheki kaka yake akampigia daktari. ...........

Safi,this one is saleable
 
Mama yake jana alipeleka birth certificate pale kituoni inayoonesha mwezi wa 5 ndo anatimiza miaka 17
 
kasomewa mashitaka leo kwa hisani ya blog ya issa michuzi kama kuna mtu anajua kuweka link saidia


BREAKING NYUZZZZZ........Elizabeth Michael a.k.a Lulu apandishwa kizimbani leo kusomewa mashtaka yake kufuatia kuhusika na kifo cha Kanumba

Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.



Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.



Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.



Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.



Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

Hii siyo SIASA
 
ndu wankubwa kuna tetesi kuwa simu aliyopigwa usiku ule na kusababisha maafa ilikuwa ni ya waziri fulani...mwenye jina aliweka hapa tumjue inawezekana yeye ndo source ya kifo kwani hata mie mke wangu akinambia anatembea na waziri tena waziri wa mzee wetu wa kichwa cha nazi na jinsi walivyowafuksa na ufisadi lazima nipatwe na brain concusion...
 
The substantial pretrial publicity of this case may prevent her from getting a fair trial.
The Public has formed an opinion, but opinion so formed can be overturned to the advantage of the accused.
Fair trial in this case is doubled-edged.
Lets wait and see how it goes....
 
Mara hii miaka imepungua?Duh, hapo najua 'hukumu' mwaka 2015....
 
Kanumba alipewa sumu muda mrefu kabla, pengine jioni ile alipotoka matembezi (au kazini) na labda siku moja au mbili kabla.

Lulu kwa kuwa alikuwa na mahusiano ya karibu alitumwa kwenda kuangalia effect ya kilo alichopewa huyo mnayemuita 'the great,' maana jamaa aliyeleta hiyo kitu kutoka Nairobi si ajabu aliwaingiza mjini

Kwa kuwa kabinti ni kichwa hewa kalienda tu kama zuzu na kalipokuwa huku jamaa kwa mchecheto wakata kujua hali ya kanumba kupitia simu ambazo Lulu aliogopa kuzijibu akihofu mhusika kusikia kuwa alikuwa anaongea na mmoja wa maadui zake.

Na hakika Kanumba alipofanikiwa kuipokonya Simu ya Lulu akagundua kuwa binti alikuwa anateta na adui yake mkuu, yaani Mr X.

"Yaani huyu ndiye ......!" akakata kauli na kuanguka maana dawa ilikwisha kuchukua effect.

Unatizama movies sana! Ulikuwepo mkuu au na wewe ulishiriki japo indirect? Unasema kuna mtu kutoka nairobi, duh, itabidi na wewe ukamatwe ukaulizwe maswali kituoni, how did you get all the infos and not report them? Au magazeti ya udaku hayo?
 
ya dunia hii ni mengi sana.....ila mwishowe yote ni ubatili
 
Ooh yeah....kanang'aa kweli kweli. Sasa najiuliza kama huko jela wanaruhusiwa kuwa na make-up, kutumia simu (manake kuna taarifa kuwa kuna watu walikuwa wanawasiliana naye kwa njia ya text messages), na kadhalika.

Hata nywele zake zipo freshi na sio tim tim kama za Wema enzi zile alipotoka Segerea

Huenda kuna mjeda anatengeneza mazingira, si unajua tena bado kabichi!!:shock:

Nitamuuliza WP mmoja pale oysterbay kujua kama siku hizi kuna rumande za VIP.
 
Hii inamaanisha uchunguzi wa awali umeonekana kuna kesi ya mauaji! dear lord! hili si kulitegemea. . hata kama badae itaonekana hana hatia itanitisha hii! RIP kanumba!
 
Back
Top Bottom