Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Hii nayo habari??Hawa waandishi jamani??lini mtaanza kufanya analysis za habari au matatizo ya wananchi??
 
mbona tumekosa vya kuandika au kuhoji? tuna hoji hadi gharama za makaburri? inasikitisha sana
 
Hii habari haina mashiko kwanza kaburi halijajengewa bado, kazi hiyo hufanywa baada ya mazishi hususani Arobaini yake au kumbukumbu ya mwaka
 
Wana jf tumieni akili kidogo na muache kumtupia lawama sana huyo lulu.. mngesema vipi km lulu ndio angekufa kwenye lile tukio kanumba akabaki hai???? Hiyo ni ajali km ilivyo ajali zingine waacheni upelelezi ukamilike kila kiti kitajulikana.. kwanza huyo kanumba mwenyew hakuwa desent as he pretended to be mbele ya jamii,, alidai hanywi pombe wala hatumii kilevi kifo kikamuumbua kafa kwa ulevi, hatembei na lulu na kafa akiwa na lulu tena kwenye wivu wa mapenzi,,, hii dunia wandugu tunapaswa kushukuru na kumtanguliza mungu atuepushe na mabalaa sio kujidai wajuaji na wasemaji wazuri wa mikasa ya watu
Hata angekuwa Lulu ndo kafa na kanumba anatendewa ndivyo sivyo watu wangehoji
 
mbona tumekosa vya kuandika au kuhoji? tuna hoji hadi gharama za makaburri? inasikitisha sana

Kama sio kakosea tarakimu basi sh. 1.55 millioni sio gharama za kuleta hapa watu wajadili. Sio lazima upost kitu hapa jamvini kama huna cha kupost. Gharama ndogo sana hiyo hata mikoani hizo gaharama za kawaida...
 
YOU ARE JOKING RIGHT?
Defence hiyo haisimami kwenye kesi kama hii ya kumtoa mtu roho kwa kukusudia au kwa bahati mbaya.
Ingesimama kwenye kesi za ubakaji and the like.
Thank God wakili wa Lulu anajua line of defence ya kumtetea angalau kumnasua na adhabu kali ( mitigation) au hata kuweka shaka kwenye kesi ya prosecution.
Ila sijui kama kuna aliyesema au kutujuza Lulu kashtakiwa na kosa gani maana hili nalo ni muhimu kujua.
ndugu yangu kwenye self defense hata ukiua is ok. tena kwa lulu msichana mdogo mwenye umbo dogo pengine nusu ya Kanumba(mwanaume) ndio usiseme kabisa na kitendo cha yeye kuvutwa kinguvu na kufungiwa chumbani ndio kabisaaa. watu watashangaa majaji watakavyoamua hii kesi maana waTz wengi ni washabiki tu. sidhani hata kama wanazifahamu hizo sheria. wanaangalia nini roho inapenda basi wanatetea tu.
Cha muhimu hapa ni kumuombea SK apumzike kwa amani.
 
Alijifunika mtandio, kwani mtandio na hijab ni kitu kimoja?Msipende kujipa ujiko hata mahala pasipo stahili; kama chama cha magamba kilivyofanya na mazishi ya Kanumba!!!!
 
Mmoja wa jambazi lilioiba fedha Ubungo NBC ni mwanamke alivaa hijabu na hiyo buibui so stara haiusian ni matendo ,ungemwambia aache tabia za kitoto lkn akitoka jela atakua above 25 so atakua ashapevuka vizuri.
 
Mmoja wa jambazi lilioiba fedha Ubungo NBC ni mwanamke alivaa hijabu na hiyo buibui so stara haiusian ni matendo ,ungemwambia aache tabia za kitoto lkn akitoka jela atakua above 25 so atakua ashapevuka vizuri.

Tukuiteje? Jaji Mihayo? ama huyu alomhukumu Lema?. Sababu naona ushakamisha ushahidi na kutoa hukumu.
Wabongo bana?
 
Wapi alipohukumiwa?

Jee, hujui kama kafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kifo cha Kanumba?

Ni kipi ulichokisoma hapo ambacho nimemhukumu Lulu? au ambacho ni cha kumzulia, si yeye si Kanumba, wote walikuwa hawana hijab ya moyoni. Kama hujui kusoma vizuri ni bora ungeuf



Toa boriti ndani ya jicho lako kwanza kabla hujaona kibanzi kwa mwenzio.
 
Toa boriti ndani ya jicho lako kwanza kabla hujaona kibanzi kwa mwenzio
 
Hii habari haina mashiko kwanza kaburi halijajengewa bado, kazi hiyo hufanywa baada ya mazishi hususani Arobaini yake au kumbukumbu ya mwaka

Kuna kujengewa ile sehemu ya nje,ambayo hufanya baadae.Pia kuna wanaojengea makaburi ile sehemu ya ndani kwa matofali kisha kuweka sakafu!Hebu tazama picha za lile kaburi!
 
Nilikua naipitia blog ya marehemu kanumba dakika chache zilizopita,nimekutana na hii post yenye picha mbuzi na kunguru pamoja na amneno mazito chini yake ambayo inaonyesha ilibandikwa na marehemu wiki mbili zilizopita,yaani tarehe 29 mwezi wa tatu mwaku huu 2012,je huu ujumbe ulimlenga nani na kwa nini?
B8.jpg

Look at this pic careful,,,moja ya vitu tulivyotofautishwa na wanyama na ndege ni Akili ya kujua mema na mabaya,tizama hao ndege na huyo mbuzi hawana akili kabisa lakini wanapendana ndio maana unaona wako pamoja ILA binadamu aliyepewa akili ana roho mbaya sana,katika mafundisho ya YESU KRISTO alisema neno kuu nawapeni PENDANENI.hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima kama huna upendo ni bure,mpende jirani yako kama unavojipenda,upendo haujivuni,hauhesabu mabaya,hautakabari,hauhusudu.....nk,1WAKORINTHO 13.Mungu ana akili sana kutuumba kwa mwili huu wa nyama laiti kama angetuumba kwa vioo au sightmirror ili uweze kuona mwenzako anakuwazia nini?anakufanyia nini?anapanga nini juu yako ungekuta ni heri ukaishi msituni na wanyama wakari kuliko kukaa na binadamu,katika tafiti zangu nimegundua kuna dawa mbalimbali mfano ya kichwa,homa,nk Lakini dawa ya Chuki na roho mbaya hakuna,,kama hiki kingekuwa kipindi kama kile cha zamani za Sodoma na Gomora au cha Nuhu ambacho Mungu alikuwa akiadhibu hapo hapo watu wengi sana wangeumbuka hasa wale wanaojifanya wasafi usoni lakini rohoni ni tofauti,Mungu atusaidie sana hasa sisi vijana tujue kusimama katika ukweli na uwazi,tuubebe upendo wa dhati toka rohoni huku mdomoni tukitamka amani ya kweli impendezayo Mungu ili watoto wetu waje watuenzi kwa mazuri na dunia ijivunie uwepo wetu.
 
Maneno mazuri sana, muda marehemu anaanguka angekuwa mfuasi wa aliyoandika angekuwa kwenye mkesha wa Ibada za Kufufuka Yesu Kristu.

RIP Kanumba
 
Back
Top Bottom