Sorry najua hichi kifo kimewauma watanzaznia wengi duniani na wapenzi wake huyo marehemu huko west africa (according to JF members). Lakini ukweli wenyewe hichi kifo kingekua kimetokea nchi za wenzetu marehemu sasa hivi ndio anaekula bad publicity Kutembea na mtoto mdogo.
Nchi za wenzetu kabla ya hata mwanasheria wa huyo dada hajafika huko polisi, child protection agencies wangekua wameshafika kuhakikisha hako katoto kako sawa mentally kutokana na mambo yaliyo mtokea na umri wake mdogo kwakuwa yeye ndio mtu wa mwisho kumuona, hayupo kwenye shock na hana akili zake timamu za kuweza kuongea etc.
Na wangeakikisha hawezi kuhojiwa bila ya psychiatrist, social worker na kuhakikisha polisi hawampi pressure kutoa majibu ya wanayowataka wao.
Sasa najiuliza na hili hitimisho la kuwa ni muhusika mkuu na kumbebesha zigo la she has something to do with it, personally i dont think it is right morally kwa sababu hata kama wengi wetu humu si wanasheria the case lucks all the motive of GBH from the outset.
Sielewi kwa nini magazeti yanaruhusiwa kumuhukumu huyu mtoto mapema hivi, if anybody needs to pick up the blame is Kanumba, what are you doing with a seventeen year old girl, tena unataka kumpeleka kwenye vilabu vya pombe na isitoshe umeanza kukajua haka katoto lini?
Nakwambia kwa wazungu hata kuzungumzia scenario ya kifo chenyewe hadharani ni aibu hili kumtunzia heshima marehemu kama alikuwa mtu wa watu hao polisi wenyewe wangesema yaishe tu. Maana huo moto wa child protection agencies and women rights ungekuwa tosha kabla ya hata mwanasheria wa huyo binti kufika.