Kifo cha Tabibu Dkt. Buberwa wa Herbal Products utata mtupu

Kwa kweli nami nashangaa sana. Alikuwa mtu maarufu ndiyo leo nasikia kifo hiki. Wanaume muwe waangalifu katika hili kuna wanawake hawafuati mapenzi bali ni mali ni mbaya sana. Ni muhimum kuandika Mirathi. Kwa hili nawasifu sana dini ambayo ina utaratibu unaoeleweka. Maana wengine wanaona mali ni za mke na watoto tu hata Mama aliyye suffer kumsomehsa hapati kitu. Tunajidai kuwaiga wazungu ambao wenyewe wana majumba ya kuwatunza wazee wao. Maanda,ano yaanze ili kushughulikia hili suala la mirathi kuna watu ni majambazi!
 
Huo upande wa pili uta justfy kitu gani?! Mume anataabika mwenyewe , anadhulumiwa, kuna cha justfy hapo?! &
Hapo bosi tayari umesha jaji bila kusikiliza upande wa pili. Mpaka sasa tumesikia mume alitaabika na kudhulumiwa. Inasikitisha.

Watu walipendana wakaoana, tatizo lilianzaje? Hapo unaweza kuta marehemu naye ana yake yaliyosababisha haya. Usiangalie mwisho wa movie tu.
 
Inasikitisha sana,wanasema kosea vitu vyote lakini sio kukosea kuoa/kuolewa.It is a very touching story,anyway we learn through mistakes.Tamaa ya mali haijawahi kuleta amani kwenye maisha ya binadamu hata siku moja,na ukikuta mmoja wa wana ndoa anafikiria mali zaidi kuliko utu unatakiwa umuogope kama ukoma.....
 
Du hii habari naiscreen shot,
You nailed it,
Kongole zako
 



Mrejesho no 2
Maelezo ya Bi Riziki Buberwa yako wazi wakati akiongea na wawakilishi wa ndugu wa marehemu kwamba walianza kutafuta mali wote na walifunga ndoa na kupata watoto watatu .

Anasema kuwa hawakujua awali kama mumewe ana mtoto mkubwa.

Kwamba baada ya kutokea kutoelewana baina yao aliamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake kisheria na mahakama iligawa mali sawa kwa sawa. Hata ofisi ya huduma za kitabibu iligawanywa kila mmoja akabaki na ya kwake.

Hivyo kila mmoja alianzisha maisha yake huku wote wakiwa na jukumu la kulea watoto

Anasema miaka kadhaa baadaye alikuja kugundua kuwa mumewe huyo amefilisika na hajui zile mali zake alipeleka wapi au kufanyia nini maana hata mtoto wake mkubwa alikosa mwelekeo. Aliamua kumchukua na kukaa naye.

Anasema maisha ya mumewe waliyetengana bila kuvunja ndoa yalikuwa hayaeleweki na kila mmoja aliishi kivyake hadi hapo mauti ilipomkuta akiwa dodoma.

Anasema taratibu za kumzika alizifanya yeye akishirikiana na badhi ya ndugu wa marehemu hasa mdogo wake wa kiume,watoto wake wote wanne na yeye.

'Dr Buberwa hakuwa na mama wala baba ,amezikwa na mkewe,baadhi ya ndugu zake na watoto wake wote hata mwanamke aliyezaa naye huyo mtoto alikuwepo' sasa mtasemaje familia yake haikuhusika?. alijibu wakati akihojiwa .

Kuhusu kutopeleka msiba bukoba Riziki anasema kuwa kulitokea sintofahamu iliyotokana na maziko ya mumewe lakini kwa sasa anajinga kupeleka msiba na watoto huko Bukoba.

Alipoulizwa alipo yule mtoto wa kiume kwa sasa amesema kuwa amepelekwa Morogoro kwa mamake.

Kuwajua vema wapendao hawa waliotikiza na kuvunja historia ya harusi za kifahari Jijijini Dar. unaweza kutazama hapa chini


Husikose mrejesho no 3
 
Una magonjwa ya akili wewe si bure!

Maana unafoka kila mahali!

Are you sure you are not crazy?

Hauokoti makopo kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…