View attachment 1837507
View attachment 1837769
Wadau. Nafikiri mnamkumbuka huyu tatibu aliyekuwa maarufu Jijijini Dar Es salaam hasa miaka ya 2010 hadi 2017 .
Huyu mwamba amefariki dunia akiwa katika nyumba ya kulala wageni Jijijini Dodoma na tayari amezikwa Jijini Dar huku kukuiwa na utata wa familia ya mkewe aitwaye Riziki mwenyeji wa Kilimanjaro na ndugu wa marehemu. Mengine yatasemwa baadaye lakini tambua kuwa huyu mwamba amakwisha zikwa wiki mbili zimepita.
RIP DR Buberwa
Tazama video zake hapa.
Mrejesho no 1
Tukio lenyewe liko hivi.
Huyo Dr Buberwa aliingia msukosuko na mkewe huyo Riziki baada ya familia kuingilia kati juu ya mambo ya mali maana alikuwa na watoto 3 wa kike kwa huyo dada Riziki na mtoto mkubwa wa kiume mkubwa aliyekutwa wakati anaolewa.
Ilikuja kubainika kuwa huyo Dr buberwa mali zote ikiwemo maduka ya dawa, nyumba zote za Dar na huko kwao ukweni walikokuwa wamejenga zilkuwa kwa jina la mke huyo.
Tangu day one huyo mama anaolewa alikuwa na one mission ya mali na kumfilisi huyo dr.
Huyo mwanamke alikimbilia mahakamani kuonesha vielelezo baada ya ndugu kuchachamaa. Mahakama ilitoa hukumu na kuonesha Dr buberwa hakuwa na kitu chochote bali usajili wa kampuni ambaye naye huyo mama ana hisa ndani.
Hivyo Dr buberwa alifukuzwa hata kwa nyumba akaanza maisha mapya kupanga. Aliishi kwa msaada wa ndugu na akaanza kuzunguka mikoani kutoa huduma mbalimbali.
Alianza kubadili huduma ikiwemo kuuza bidhaa za ulinzi kama cctv camera nk pamoja na mambo ya unabii.
Baadaye alianza kuugua magonjwa mbalimbali hadi kukatwa mguu mmoja. sijui chanzo cha ugonjwa uliosababisha ukatwe ila inasemekana ni kansa.
Kutokana na kuangaika mikoa mbalimbali mauti yalimkuta akiwa guest dodoma ambapo haijulikani kama aliuawa,alijiua au alikufa kifo cha kawaida. wahudumu walikuja kushtukia mteja wao hafungui mwishowe ikabanika amekufa.
Sasa ndugu walipopata taarifa walimtafuta mkewe naye akasema anazo taarifa. Wakakubaliana kuwa kwa kuwa maiti iko dodoma basi wapitie maiti waipeleke Bukoba direct kuzika.
Dadake na marehemu aitwaye Jen na ndg wengine walianza safari kuelekea dodoma lakini walipofika wakaambiwa maiti imechukuliwa na mkewe kwenda Dar.
Mzozo ulianza lakini hawa ndg walipitiliza hadi Bukoba huku mke akisema ameipeleka kwake ili aagwe then watarudisha mwili bukoba.
Huyu dada alianza visa na visa na mwishowe akashirikiana na mdogo wake na marehemu wa kiume wakazika huko dar.
Kule Bukoba wakasubiri wapeleke udongo ( kulingana na taratibu za mila zao) pamoja na watoto lakini udongo ulitumwa lakini huyo mama na watoto hawakwenda.
Ilikuja kubainika kuwa hadi mauti yanamkuta marehemu alishakuwa maskini wa kutupwa na hata yule kijana mkubwa alikuwa anaishi kwa huyo riziki hana chochote kile kutoka kwa baba.
Hitimisho.
Tutumie tukio hili kuishi vema na wake zetu siyo kwa kuwa huyu alikuwa mchaga bali dunia ya tamaa za mali imeongezeka sana.
Asante