Nimeponea chupuchupu kuuliwa na mpare hata sitaki kuwasikia,nimeishi nae 10yrs kumbe ananilia target nimalizie mjengo anirestishe in peace,mungu ni mkubwa na ahimidiwe kwa kweli.
Ingawaje si vizuri kuonyesha udhaifu wa kabila , lakini na mimi na rafiki yangu karibu turestishwe in peace na dada mmoja wa kipare.
Ilikuwa hivi.
Tulikuwa marafiki watatu ambao tulianzisha mradi kwa ubia na mradi uikuwa unaenda vizuri sana na unakaribia kukamilika kule Morogoro.
Mradi ulianza kuleta faida nzuri kabisa kabla hata ya kukamilika na ulitutoa familia zote tatu.
Kwa bahati mbaya yule mume wa dada wa kipare akakanyaga miwaya, na akaanza kuugua.
Ilipoonekana ni lazima atatangulia mbele za haki panic ikaingia kwa familia ya dada wa kipare.
Bahati nzuri tulijua kuwa yule dada wa kipare ana roho mbaya.
Lakini yaliyotokea ni funga kazi.
Kuna siku tumeenda kumjulia hali rafiki yetu ambaye sasa likuwa hoi bin taabani, tukatonywa na house girl wake ambaye tulimzoea maana tulikuwa kama marafiki tunaotembeleana sana.
Na yule house girl alikuwa wa kabila ya yule mwenzangu wa pili.
Yule house girl akatwambia tukiletewa juice tusinywe kwa hali yoyote.
Basi tumekaa sebule tunamsubiri mwezetu mgonjwa atoke toka chumbani , kweli tukaletewa juice .
Tukatazamana na mwenzangu na tukakaa kimya.
Mgonjwa alipotoka tukamjulia hali na tukaongea naye kwa muda kidogo.
Dakika kumi baadaye yule dada wa kipare kaja, kitu cha kwanza anatuuliza kwa nini hamywi juice?
Siye tukamwambia tumeshiba!!
Haraka akamwita house girl na akamwambia akaimwage!!
Asingeimwaga ile juice , kwa vile ana watoto alijua wanaweza kunywa
Tulishangaa na tukaondoka zetu.
Rafiki yetu aliaga dunia si muda mrefu.
Yule dada alijua mume angefariki, na ili apige bingo na hawa marafiki zake wakiondoka yeye angerithi mali zote.
Duniani kuna mambo!
(hii stori ni ya kweli, sio riwaya)