Kifo hakipangwi na Mungu



"Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?"

Fafanua Kwa nini kisichopo hakithibitishwi? na unauthibitisho gani kisichopo hakithibitishiki?
 
Nyani Ngabu said:
Hayo chini ndo maswali niliyokuuliza.

Hujajibu hata moja!
Mkuu,naomba nijibu kwa niaba yake kama hutojali

1]Kama huyo mungu tayari una tajiriba/ uzoefu naye, iweje tena uamini kwamba yupo?
Labda niiweke hivi,unaweza kuwa na Direct au indirect experience

Hajawahi kumuona Mungu,yeye ana indirect experience

Ili ujue kama kitu kipo
lazima uki-experience directly,otherwise bado utaendelea kuamini

2]Sasa kama yupo kweli [kwa mujibu wa hiyo tajiriba/ uzoefu wako kwake na kwa maisha ya wengine], kwa nini unaamini, na si kujua, kwamba yupo?
Nafikiri nimekujibu vema hapo juu

3]Vilivyopo huwa vinaaminika au huwa vinajulikana kuwa vipo?

Vinaweza kuaminika au kujulikana pia
Theoretically,tunaamini kuwa ulimwengu unatii cosmological principles
Yaani sheria za asili ni sawa ulimwengu mzima

Lakini hakuna anayejua
Je ulimwengu huo haupo,kwasababu ni wa kuaminika tu?

4.Mwisho,kujua na kuamini ni vitu viwili tofauti
 
Bila shaka kama kuna mungu kama huyo, basi atakuwa mpumbavu sana
 
Haisaidii
 
Sasa wewe hapa sijui unataka nini. Mungu lazima angepanga tu. Na huo ndio mpango aliochagua.
Amepanga hivi unasema kwa nini hakupanga vile. Na angepanga vile ungesema kwa nini hakupanga hivi.

Kusema it's not all up to God namaanisha kwamba Mungu na mwanadamu wote wana role ya kuplay ktk kuhakikisha kuwa mwanadamu anakuwa ktk ukamilifu wake.

Unaposema kwa nini Mungu aliumba dunia ambayo kifo kinawezekana, u are being illogical and unfair.
Kwanza kifo ni kizuri....kifo ni kitu cha asili. Bila kifo hata wewe pengine usingekuwepo...

Pili, huwezi kuishi irresponsibly ili mwisho wa siku umtupie Mungu lawama zote.
 
Katika kukujibu naomba nikuulize tena....

Wewe unaamini au unajua kuwa kuna sayari inayoitwa jupiter?
 
"Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?"

Fafanua Kwa nini kisichopo hakithibitishwi? na unauthibitisho gani kisichopo hakithibitishiki?
Kisichopo hakithibitishiki kwa sababu hakipo ili kuthibitishwa.

Uthibitisho ni kwamba, hakuna kisichopo kinachothibitishika, kama kipo kitaje.
 
Hujajibu swali. Umeliepuka tu.

Kwa nini mungu kaumba dunia yenye mabaya, mateso, magonjwa, uonevu, ukatili etc wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wa kuumba dunia ambayo yote hayo hayawezekani bila kujipunguzia chochote?

Unaongeaje habari za "huwezi kuishi irresponsibly" kwa mtoto anayekufa wakati wa kuzaliwa?

Huyo mtoto kaishi vipi irresponsibly?
 
Umejuaje kwamba Mungu kaumba dunia yenye mabaya yote hayo? Nini kinakufanya usione kwamba Mungu kaumba dunia ambayo ni pure na hayo mabaya yametokana na complexity ya hii dunia?

Kwa mfano vita vinasababishwa na ubinafsi na uchu wa madaraka wa binadamu. Sasa unataka kuniambia Mungu aliumba vita?

Mtoto wa mtu akiwa changudoa utasema mzazi wake alizaa changudoa?

Ukihitimisha hivyo utakuwa hutendi haki na utakuwa kinyume na falsafa yako ya kutumia logical reasoning.
 
Mkuu,naomba nijibu kwa niaba yake kama hutojali

Wewe msaidie tu kama unaona kalemewa.

Labda niiweke hivi,unaweza kuwa na Direct au indirect experience

Sawa. Hivi hujui Kiswahili cha 'experience'?

Hajawahi kumuona Mungu,yeye ana indirect experience

Okay....hiyo unayoiita indirect experience ndo nini? Waweza kunipa mifano?

Ili ujue kama kitu kipo
lazima uki-experience directly,otherwise bado utaendelea kuamini

Anhaa....kwa hiyo hajui basi kwamba mungu yupo bali anaamini kwamba mungu yupo, siyo?

Nafikiri nimekujibu vema hapo juu

Sidhani kama umenijibu vema. Umejitahidi kwa kiasi chako.

Vinaweza kuaminika au kujulikana pia

Okay....

Theoretically,tunaamini kuwa ulimwengu unatii cosmological principles
Yaani sheria za asili ni sawa ulimwengu mzima

Wewe kidogo naona unajua unachokisema.

Lakini hakuna anayejua
Je ulimwengu huo haupo,kwasababu ni wa kuaminika tu?

Kama upo basi si wa kuaminika tena. Utakuwa ni wa kujulikana.

4.Mwisho,kujua na kuamini ni vitu viwili tofauti

Kidogo naanza kupata imani na wewe kwamba walau unajua unachokisema.

Sasa unaweza kunipa tofauti ya kujua na kuamini, kwa maneno yako mwenyewe?
 

Mungu hajaumba mabaya wala uovu
Bali uovu kauleta mwanadam baada ya kumuasi Mungu

Binadam kapewe fursa ya kuchagu[Free will]
Hivyo Mungu hawezi kuingilia uamuzi wake
 
Umejuaje kwamba Mungu kaumba dunia yenye mabaya yote hayo? Nini kinakufanya usione kwamba Mungu kaumba dunia ambayo ni pure na hayo mabaya yametokana na complexity ya hii dunia?.

Bado hujaelewa swali. Hiyo complexity imekuja bila mungu kuipanga? Au alipanga iwepo na baadaye ikaleta mabaya?

Kama imekuja bila mungu kuipanga, je ni kweli mungu anajua na kuweza yote? Mbona complexity imekuja bila kupangwa?

Kama aliipanga complexity iwepo na baadaye ikaleta mabaya, utasemaje kwamba hakuumba ulimwengu unaowezekana kuwa na mabaya?

In any case, ultimately your god is responsible for the world.Ukisema watu wamefanya dhambi ndiyo maana ulimwengu ukawa na mabaya, nitakuuliza, mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu hawawezi kufanya dhambi?

Kwa mfano vita vinasababishwa na ubinafsi na uchu wa madaraka wa binadamu. Sasa unataka kuniambia Mungu aliumba vita?.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao uchu wa madaraka hauwezekani?

Mtoto wa mtu akiwa changudoa utasema mzazi wake alizaa changudoa?.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao uchangudoa hauwezekani?

Kama alishindwa, ni kweli ana uwezo wote?

Kama hakushindwa ila aliamua tu kutouumba, je, ni kweli ana upendo wote?

Mfano wako wa mzazi na mtoto ni mfano fyongo. Mzazi hana control juu ya maisha ya mtoto kama mnavyosema mungu ana control juu ya ulimwengu. Unapotoa mfano, toa mfano wa vitu vinavyofanana ama kulingana kwa namna Fulani.

Ukihitimisha hivyo utakuwa hutendi haki na utakuwa kinyume na falsafa yako ya kutumia logical reasoning.

Mfano wako una mawaa na mtu anayetumia mantiki hawezi hata kuutumia.

Zaidi ya hapo, kama unajua kwamba huwezi kumlaumu mzazi kwa makosa ya mtoto, wala mtoto kwa makosa ya mzazi, ungejua kwamba habari ya mungu kumhukumu mtoto kuzaliwa mfu kwa sababu mama yake alikuwa mlevi ni habari isiyoyumkinika kwa mtu yeyote anayetumia ubongo wake kufikiri.
 
Katika kukujibu naomba nikuulize tena....

Wewe unaamini au unajua kuwa kuna sayari inayoitwa jupiter?

You are employing sidetracking tactics.

Hapa tupo tunaongelea uwepo na uwezo wa mungu halafu wewe unaleta habari za Jupita.

Maswali umeulizwa toka jana. Ukaahidi utarudi kuyajibu ukishakunywa chai.

Nasadiki chai ushakunywa na pengine hata chakula cha mchana ushakula. Sitashangaa kama hadi supu ushakunywa.

Maswali yangu bado hujajibu lakini unaniuliza swali lako.

Nikikujibu hilo swali lako tutatoka kwenye maswali niliyokuuliza na kuanza kuhojiana kuhusu Jupita.

Hapana. Jibu kwanza maswali yangu. Tukimalizana na hayo ndo tutaenda huko kwenye Jupita na hata Mushtara kama utapenda.

Sawa?
 
Mungu hajaumba mabaya wala uovu
Bali uovu kauleta mwanadam baada ya kumuasi Mungu

Binadam kapewe fursa ya kuchagu[Free will]
Hivyo Mungu hawezi kuingilia uamuzi wake
Hujaelewa swali.

Naongelea pale mungu alipokuwa anapanga kuumba dunia.

Alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao uovu hauwezekaniki kabisa, hata mwanadamu ajitahidi vipi hawezi kufanya uovu.

Kama vile ambavyo mwanadamu hawezi kurudi nyuma katika muda kwa sasa, muda unaenda mbele tu.

Sasa kwa nini mungu hakuumba ulimwengu huo ambao uovu, mabaya, mateso, majanga etc haviwezekaniki kabisa?

Naongelea kabla mwanadamu hajatokea, mungu anaumba ulimwengu.Kwa hiyo usiniambie habari za uovu umeletwa na matendo ya binadamu.
 

Ahsante kwa kuniami

Kwa uelewa wangu,kuamini hakuhitaji factual knowledge

Mtu anaweza kuamini chochote anachotaka,lakini ili ujue lazima uwe na direct perception pamoja na uelewa wa hicho kitu

Labda nikuulize wewe,
Unaamini kuwa Mungu hayupo au unajua kuwa Mungu hayupo?[utanisamehe kama wewe ni theist]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…