Kifo hakipangwi na Mungu

Kifo hakipangwi na Mungu

Hivi ninachoandika unasoma?

Ulifuatilia mjadala kuhusu "zama za giza" au unarukia tu kwa kuungaunga habari?

Unayekubali kuwepo kwa mungu kwa imani unaweza kuongelea "objectivity"?

Unaelewa kwamba imani na objectivity havichangamani?

Unajua kusoma na kuelewa kwa kituo?

Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?

Umeelewa nini nilipotoa mfano wa kusema polisi hawakuambii uthibitishe kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya, bali hutaka uthibitisho kwamba nyumba yako ina madawa ya kulevya?

Umeelewa nini nilipoandika kwamba mungu wenu hawezekaniki kuwepo, kama pembetatu duara isivyowezekanika kuwepo katika Euclidean geometry, kwa maana idea yake inajipinga yenyewe kabla mimi sijampinga kwa kukosa logical consistency?

Umeelewa nini?

Hata una uwezo wa kuelewa?

"Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?"

Fafanua Kwa nini kisichopo hakithibitishwi? na unauthibitisho gani kisichopo hakithibitishiki?
 
Nyani Ngabu said:
Hayo chini ndo maswali niliyokuuliza.

Hujajibu hata moja!
Mkuu,naomba nijibu kwa niaba yake kama hutojali

1]Kama huyo mungu tayari una tajiriba/ uzoefu naye, iweje tena uamini kwamba yupo?
Labda niiweke hivi,unaweza kuwa na Direct au indirect experience

Hajawahi kumuona Mungu,yeye ana indirect experience

Ili ujue kama kitu kipo
lazima uki-experience directly,otherwise bado utaendelea kuamini

2]Sasa kama yupo kweli [kwa mujibu wa hiyo tajiriba/ uzoefu wako kwake na kwa maisha ya wengine], kwa nini unaamini, na si kujua, kwamba yupo?
Nafikiri nimekujibu vema hapo juu

3]Vilivyopo huwa vinaaminika au huwa vinajulikana kuwa vipo?

Vinaweza kuaminika au kujulikana pia
Theoretically,tunaamini kuwa ulimwengu unatii cosmological principles
Yaani sheria za asili ni sawa ulimwengu mzima

Lakini hakuna anayejua
Je ulimwengu huo haupo,kwasababu ni wa kuaminika tu?

4.Mwisho,kujua na kuamini ni vitu viwili tofauti
 
Hujaelewa swali.

Swali ulilojibu si nililouliza.

Kabla watu kuwapo, alikuwapo mungu. Kwa mujibu wenu.

Swali langu linahusika na misimgi ya ulimwengu ilivyowekwa kabla ya watu kuwapo, huwezi kuwalaumu watu kwa matendo yao wakati mungu ndiye katia mipaka ya kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.

Pia, mnayemsema mungu anayeacha mabaya yatokee kwa watoto kwa sababu ya makosa ya wazazi, wakati ana uwezo wa kuzuia hayo, ni mungu kweli huyu? Ana upendo kweli huyu?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hakuumba ulimwengu ambao watoto wasio na hatia hawawezi kufa kwa ulevi wa mama zao?

Better yet, kwa nini hakuumba ulimwengu ambao ulevi hauwezekani?

Hakuweza kuumba ulimwengu huo?

Au aliweza hakutaka tu?

Kama hakuweza, ni kweli ana uwezo wote?

Kama aliweza, ila hakutaka tu, ni kweli ana upendo wote?
Bila shaka kama kuna mungu kama huyo, basi atakuwa mpumbavu sana
 
Nimesikiliza watu wengi mtu akifa wanasema "Mungu amepanga". Uongo huu umepita kizazi hata kizazi ili tufarijike katiba misiba.

Ukweli ni huu, Mungu hapangi kifo cha mtu chini ya miaka 70. Mtu anayekufa akiwa na miaka zaidi ya 70 ni mapenzi ya Mungu.

Mungu hana kitabu ameandika aina ya kifo cha mtu chini ya miaka 70. Watu wanakufa kutokana na aina ya maisha wanayo ishi, mazingira wanayoishi na imani za kishetani.
Haisaidii
 
Nimekuuliza habari ya mungu alivyopanga, kabla watu hawajaumbwa.

Kwa nini mungu alipanga hivi na si vingine.

Utasemaje it is not up to god?

Una maana mungu hakuumba ulimwengu?

Kama aliumba, utasemaje kanuni alizotumia kuumba ulimwengu hatuwezi kuuliza kwa nini kaumba hivi na si vile?
Sasa wewe hapa sijui unataka nini. Mungu lazima angepanga tu. Na huo ndio mpango aliochagua.
Amepanga hivi unasema kwa nini hakupanga vile. Na angepanga vile ungesema kwa nini hakupanga hivi.

Kusema it's not all up to God namaanisha kwamba Mungu na mwanadamu wote wana role ya kuplay ktk kuhakikisha kuwa mwanadamu anakuwa ktk ukamilifu wake.

Unaposema kwa nini Mungu aliumba dunia ambayo kifo kinawezekana, u are being illogical and unfair.
Kwanza kifo ni kizuri....kifo ni kitu cha asili. Bila kifo hata wewe pengine usingekuwepo...

Pili, huwezi kuishi irresponsibly ili mwisho wa siku umtupie Mungu lawama zote.
 
Hayo chini ndo maswali niliyokuuliza.

Hujajibu hata moja!

Ngoja nijaribu tena:

1]Kama huyo mungu tayari una tajiriba/ uzoefu naye, iweje tena uamini kwamba yupo?

2]Sasa kama yupo kweli [kwa mujibu wa hiyo tajiriba/ uzoefu wako kwake na kwa maisha ya wengine], kwa nini unaamini, na si kujua, kwamba yupo?

3]Vilivyopo huwa vinaaminika au huwa vinajulikana kuwa vipo?

4]Au hayo maneno 'kuamini na kujua' huwa yanatumika interchangeably?
Katika kukujibu naomba nikuulize tena....

Wewe unaamini au unajua kuwa kuna sayari inayoitwa jupiter?
 
"Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?"

Fafanua Kwa nini kisichopo hakithibitishwi? na unauthibitisho gani kisichopo hakithibitishiki?
Kisichopo hakithibitishiki kwa sababu hakipo ili kuthibitishwa.

Uthibitisho ni kwamba, hakuna kisichopo kinachothibitishika, kama kipo kitaje.
 
Sasa wewe hapa sijui unataka nini. Mungu lazima angepanga tu. Na huo ndio mpango aliochagua.
Amepanga hivi unasema kwa nini hakupanga vile. Na angepanga vile ungesema kwa nini hakupanga hivi.

Kusema it's not all up to God namaanisha kwamba Mungu na mwanadamu wote wana role ya kuplay ktk kuhakikisha kuwa mwanadamu anakuwa ktk ukamilifu wake.

Unaposema kwa nini Mungu aliumba dunia ambayo kifo kinawezekana, u are being illogical and unfair.
Kwanza kifo ni kizuri....kifo ni kitu cha asili. Bila kifo hata wewe pengine usingekuwepo...

Pili, huwezi kuishi irresponsibly ili mwisho wa siku umtupie Mungu lawama zote.
Hujajibu swali. Umeliepuka tu.

Kwa nini mungu kaumba dunia yenye mabaya, mateso, magonjwa, uonevu, ukatili etc wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wa kuumba dunia ambayo yote hayo hayawezekani bila kujipunguzia chochote?

Unaongeaje habari za "huwezi kuishi irresponsibly" kwa mtoto anayekufa wakati wa kuzaliwa?

Huyo mtoto kaishi vipi irresponsibly?
 
Umejuaje kwamba Mungu kaumba dunia yenye mabaya yote hayo? Nini kinakufanya usione kwamba Mungu kaumba dunia ambayo ni pure na hayo mabaya yametokana na complexity ya hii dunia?

Kwa mfano vita vinasababishwa na ubinafsi na uchu wa madaraka wa binadamu. Sasa unataka kuniambia Mungu aliumba vita?

Mtoto wa mtu akiwa changudoa utasema mzazi wake alizaa changudoa?

Ukihitimisha hivyo utakuwa hutendi haki na utakuwa kinyume na falsafa yako ya kutumia logical reasoning.
 
Mkuu,naomba nijibu kwa niaba yake kama hutojali

Wewe msaidie tu kama unaona kalemewa.

Labda niiweke hivi,unaweza kuwa na Direct au indirect experience

Sawa. Hivi hujui Kiswahili cha 'experience'?

Hajawahi kumuona Mungu,yeye ana indirect experience

Okay....hiyo unayoiita indirect experience ndo nini? Waweza kunipa mifano?

Ili ujue kama kitu kipo
lazima uki-experience directly,otherwise bado utaendelea kuamini

Anhaa....kwa hiyo hajui basi kwamba mungu yupo bali anaamini kwamba mungu yupo, siyo?

Nafikiri nimekujibu vema hapo juu

Sidhani kama umenijibu vema. Umejitahidi kwa kiasi chako.

Vinaweza kuaminika au kujulikana pia

Okay....

Theoretically,tunaamini kuwa ulimwengu unatii cosmological principles
Yaani sheria za asili ni sawa ulimwengu mzima

Wewe kidogo naona unajua unachokisema.

Lakini hakuna anayejua
Je ulimwengu huo haupo,kwasababu ni wa kuaminika tu?

Kama upo basi si wa kuaminika tena. Utakuwa ni wa kujulikana.

4.Mwisho,kujua na kuamini ni vitu viwili tofauti

Kidogo naanza kupata imani na wewe kwamba walau unajua unachokisema.

Sasa unaweza kunipa tofauti ya kujua na kuamini, kwa maneno yako mwenyewe?
 
Hujajibu swali. Umeliepuka tu.

Kwa nini mungu kaumba dunia yenye mabaya, mateso, magonjwa, uonevu, ukatili etc wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wa kuumba dunia ambayo yote hayo hayawezekani bila kujipunguzia chochote?

Unaongeaje habari za "huwezi kuishi irresponsibly" kwa mtoto anayekufa wakati wa kuzaliwa?

Huyo mtoto kaishi vipi irresponsibly?

Mungu hajaumba mabaya wala uovu
Bali uovu kauleta mwanadam baada ya kumuasi Mungu

Binadam kapewe fursa ya kuchagu[Free will]
Hivyo Mungu hawezi kuingilia uamuzi wake
 
Umejuaje kwamba Mungu kaumba dunia yenye mabaya yote hayo? Nini kinakufanya usione kwamba Mungu kaumba dunia ambayo ni pure na hayo mabaya yametokana na complexity ya hii dunia?.

Bado hujaelewa swali. Hiyo complexity imekuja bila mungu kuipanga? Au alipanga iwepo na baadaye ikaleta mabaya?

Kama imekuja bila mungu kuipanga, je ni kweli mungu anajua na kuweza yote? Mbona complexity imekuja bila kupangwa?

Kama aliipanga complexity iwepo na baadaye ikaleta mabaya, utasemaje kwamba hakuumba ulimwengu unaowezekana kuwa na mabaya?

In any case, ultimately your god is responsible for the world.Ukisema watu wamefanya dhambi ndiyo maana ulimwengu ukawa na mabaya, nitakuuliza, mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu hawawezi kufanya dhambi?

Kwa mfano vita vinasababishwa na ubinafsi na uchu wa madaraka wa binadamu. Sasa unataka kuniambia Mungu aliumba vita?.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao uchu wa madaraka hauwezekani?

Mtoto wa mtu akiwa changudoa utasema mzazi wake alizaa changudoa?.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao uchangudoa hauwezekani?

Kama alishindwa, ni kweli ana uwezo wote?

Kama hakushindwa ila aliamua tu kutouumba, je, ni kweli ana upendo wote?

Mfano wako wa mzazi na mtoto ni mfano fyongo. Mzazi hana control juu ya maisha ya mtoto kama mnavyosema mungu ana control juu ya ulimwengu. Unapotoa mfano, toa mfano wa vitu vinavyofanana ama kulingana kwa namna Fulani.

Ukihitimisha hivyo utakuwa hutendi haki na utakuwa kinyume na falsafa yako ya kutumia logical reasoning.

Mfano wako una mawaa na mtu anayetumia mantiki hawezi hata kuutumia.

Zaidi ya hapo, kama unajua kwamba huwezi kumlaumu mzazi kwa makosa ya mtoto, wala mtoto kwa makosa ya mzazi, ungejua kwamba habari ya mungu kumhukumu mtoto kuzaliwa mfu kwa sababu mama yake alikuwa mlevi ni habari isiyoyumkinika kwa mtu yeyote anayetumia ubongo wake kufikiri.
 
Katika kukujibu naomba nikuulize tena....

Wewe unaamini au unajua kuwa kuna sayari inayoitwa jupiter?

You are employing sidetracking tactics.

Hapa tupo tunaongelea uwepo na uwezo wa mungu halafu wewe unaleta habari za Jupita.

Maswali umeulizwa toka jana. Ukaahidi utarudi kuyajibu ukishakunywa chai.

Nasadiki chai ushakunywa na pengine hata chakula cha mchana ushakula. Sitashangaa kama hadi supu ushakunywa.

Maswali yangu bado hujajibu lakini unaniuliza swali lako.

Nikikujibu hilo swali lako tutatoka kwenye maswali niliyokuuliza na kuanza kuhojiana kuhusu Jupita.

Hapana. Jibu kwanza maswali yangu. Tukimalizana na hayo ndo tutaenda huko kwenye Jupita na hata Mushtara kama utapenda.

Sawa?
 
Mungu hajaumba mabaya wala uovu
Bali uovu kauleta mwanadam baada ya kumuasi Mungu

Binadam kapewe fursa ya kuchagu[Free will]
Hivyo Mungu hawezi kuingilia uamuzi wake
Hujaelewa swali.

Naongelea pale mungu alipokuwa anapanga kuumba dunia.

Alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao uovu hauwezekaniki kabisa, hata mwanadamu ajitahidi vipi hawezi kufanya uovu.

Kama vile ambavyo mwanadamu hawezi kurudi nyuma katika muda kwa sasa, muda unaenda mbele tu.

Sasa kwa nini mungu hakuumba ulimwengu huo ambao uovu, mabaya, mateso, majanga etc haviwezekaniki kabisa?

Naongelea kabla mwanadamu hajatokea, mungu anaumba ulimwengu.Kwa hiyo usiniambie habari za uovu umeletwa na matendo ya binadamu.
 
Wewe msaidie tu kama unaona kalemewa.

Sawa. Hivi hujui Kiswahili cha 'experience'?

Okay....hiyo unayoiita indirect experience ndo nini? Waweza kunipa mifano?

Anhaa....kwa hiyo hajui basi kwamba mungu yupo bali anaamini kwamba mungu yupo, siyo?

Sidhani kama umenijibu vema. Umejitahidi kwa kiasi chako.

Okay....

Wewe kidogo naona unajua unachokisema.

Kama upo basi si wa kuaminika tena. Utakuwa ni wa kujulikana.

Kidogo naanza kupata imani na wewe kwamba walau unajua unachokisema.

Sasa unaweza kunipa tofauti ya kujua na kuamini, kwa maneno yako mwenyewe?

Ahsante kwa kuniami

Kwa uelewa wangu,kuamini hakuhitaji factual knowledge

Mtu anaweza kuamini chochote anachotaka,lakini ili ujue lazima uwe na direct perception pamoja na uelewa wa hicho kitu

Labda nikuulize wewe,
Unaamini kuwa Mungu hayupo au unajua kuwa Mungu hayupo?[utanisamehe kama wewe ni theist]
 
Back
Top Bottom