- Thread starter
- #301
Hivi ninachoandika unasoma?
Ulifuatilia mjadala kuhusu "zama za giza" au unarukia tu kwa kuungaunga habari?
Unayekubali kuwepo kwa mungu kwa imani unaweza kuongelea "objectivity"?
Unaelewa kwamba imani na objectivity havichangamani?
Unajua kusoma na kuelewa kwa kituo?
Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?
Umeelewa nini nilipotoa mfano wa kusema polisi hawakuambii uthibitishe kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya, bali hutaka uthibitisho kwamba nyumba yako ina madawa ya kulevya?
Umeelewa nini nilipoandika kwamba mungu wenu hawezekaniki kuwepo, kama pembetatu duara isivyowezekanika kuwepo katika Euclidean geometry, kwa maana idea yake inajipinga yenyewe kabla mimi sijampinga kwa kukosa logical consistency?
Umeelewa nini?
Hata una uwezo wa kuelewa?
"Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?"
Fafanua Kwa nini kisichopo hakithibitishwi? na unauthibitisho gani kisichopo hakithibitishiki?