Kifo hakipangwi na Mungu

Napopata wakati mgumu ni pale mtu anapokufa watumishi wa MUNGU na ndugu kumuombea mtu mfu alale mahali pema peponi,hua sielewi,mtu alikua mwizi,mchawi wa kudhuru manadamu wengine,jambazi muuaji,mtembea na wake/ waume za watu,muongo wa kupindukia,eti akilala mauti ghafla inaandaliwa misa na maombi yanasemwa alale mahala pema peponi,kulala mahala pema peponi ni kazi ya MUNGU mwenyewe anapompima mtu na matendo yake alokua akifanya hapa duniani,hua napata shida nilipokua nikijua tabia za marehemu tena amekata ghafla bila kufanya toba,lakini tunasema alale mahala pema peponi...dah!
 

Mkuu huo ndio unaitwa udini tu, utaratibu tu wa ibada. Sala zote kwa ajili ya marehemu hazina maana yeyote kwake yeye. Ndio maana ni muhimu kuishi maisha ya kumpendeza Mungu wakati uko hai. Ufifa tu game is over.
 
Mungu hapangi kifo kwa sababu hayupo.

Kama yupo naomba kuthibitishiwa.

Uthibitisho ni huu- hakuna anayekuamsha asubuhi unajikua umeamka, hukufanya kitu cha ziada unafanya uamke na unavuta oxygen yake ya bure. Akizuia hiyo hewa kwa takika tano huna uhai. Kwa kifupi huu ni uthibitisho tosha ya kuwa Mungu yupo.
 
Uthibitisho ni huu- hakuna anayekuamsha asubuhi unajikua umeamka, hukufanya kitu cha ziada unafanya uamke na unavuta oxygen yake ya bure. Akizuia hiyo hewa kwa takika tano huna uhai. Kwa kifupi huu ni uthibitisho tosha ya kuwa Mungu yupo.
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Umeaema hakuna anayeniamsha.

Nakwambia nithibitishie kwamba mungu yupo, unaniambia mungu ananipa oxygen.

Unajuaje kama ni mungu na si kitu kingine chochote tofauti?
 

Kwa hyo na Mugabe anakula bonasi yake
 
Hiyo miaka 70 wewe umeitoa wapi? Kwa nini siyo 90 au 100?

Au na wewe umekuja na TIMELY MESSAGE FROM HEAVEN kama Kibwetele?

Kama na wewe huna ushahidi basi unapaswa upuuzwe tu maana huna tofauti na hao unaowakosoa.

Hizi siyo zama za kuaminishana.

Nimeandika zaidi ya miaka 70 so it can be 90 au 100. Jaribu kuwa na open minded utajifunza vingi mkuu!
 
Uthibitisho ni huu- hakuna anayekuamsha asubuhi unajikua umeamka, hukufanya kitu cha ziada unafanya uamke na unavuta oxygen yake ya bure. Akizuia hiyo hewa kwa takika tano huna uhai. Kwa kifupi huu ni uthibitisho tosha ya kuwa Mungu yupo.

Kwahyo zile oxygen pump mahospitalin zinaendeshwa na mungu ndani yake
 
Umri wa mwanadamu ni miaka sabini akiwa na nguvu ni miaka 80 baada ya hapo unaishi miaka ya ubatili
Mkanganyiko:
Siku moja kwa Mungu ni kama siku elfu kwa mwanadamu
Yote ni maandiko matakatifu yahitaji hekima ya kimungu kuweza kufunuliwa
Nb: sijakupinga nimeongezea
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Umeaema hakuna anayeniamsha.

Nakwambia nithibitishie kwamba mungu yupo, unaniambia mungu ananipa oxygen.

Unajuaje kama ni mungu na si kitu kingine chochote tofauti?

Kiranga mbona hii iko wazi kabisa, unataka uthibitisho gani wakati nimesha kupa hapo juu.
Mungu yupo = unaamka kila asubuhi ni yeye anafanya hayo
Oxygen = ni uumbaji wake tunavuta wote bure
Ninajuaje = Ni Mungu tu mwenye uwezo huo na sio kitu kingine chochote.
 
Hakuna hata kimoja hapo kinachothibitisha uwepo wa mungu.

Nakuuliza unajuaje kwamba mungu yupo? Unajibu ni mungu tu mwenye uwezo huo.

That is a cyclical argument.

Nakuuliza unaweza kuthibitisha mungu yupo? Kabla ya kuthibitisha kwamba mungu yupo, inakuja na conclusion kwamba ni mungu tu ndiye anayeweza kumpa binadamu oxygen.

Unajuaje kwamba ni mungu tu?
 

Swali hilo limeulizwa na watu wengi ulimwenguni kote, na jibu bado ni gumu sana kueleweka kwa watu wengi kirahisi ulimwenguni kote. Hivyo kuna vithibitisho vingi vinavyo tuonyesha kuwa Mungu yupo. Kwa mfano umbaji wa binadamu, dunia na elements zake. Mimi nafikili tukubaliane kutokukubaliana kwamba Mungu Yupo. Kama wewe unalojibu la unajuaje tujuze.
 
Uumbaji wa binadamu ukoje?

Mbona unasema mambo jumlajumla tu bila details?

Unaweza kuonyesha kwamba binadamu kaumbwa na mungu tu na hawezi kuwa ametokea vibgine vyovyote?

"Dunia na elements zake" inathibitishaje kuwapo kwa mungu?

"Kukubaliana kutokubaliana" ni kitu gani?

Ni kukubaliana au kutokubaliana?
 
Kiranga unapenda sana ligi na believers kwanza mnamtafisiri Mungu yupi apa? Au tuelezane kwanza nini maana ya Mungu yani God
 


Mkuu kiranga naamini hata nikijibu maswali yako in details bado swali lako litabaki kuwa pale pale unajuaje! na haitaishia hapo. kila jibu litakuwa na swali hivyo tunaweza tusimalize leo. Mimi naona tukubaliane au kutokubaliana kuwa Mungu yupo. Kama wewe unalojibu la unajuaje nijuze ningependa kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…