Kifo hakipangwi na Mungu

Kifo hakipangwi na Mungu

Nimeandika zaidi ya miaka 70 so it can be 90 au 100. Jaribu kuwa na open minded utajifunza vingi mkuu!

Hujanielewa???

Why not 50 or 60 and above?

Swali la msingi ni kwamba hiyo 70 umeitoa wapi? Kwa nini 70 ndo minimum na siyo namba nyinginre yoyote?

Kwa nini usisema from 80 and above or 100 and above?
 
Mungu kwenye vitabu vyenu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Utamfananishaje na mtu ambaye hana uwezo wote, ujuzi wote wala upendo wote?
Umejibu swali moja tu,rudi na majibu ya mawili yaliyobakia.
 
Kweli kabisa
Ukiwa mvutaji wa sigara utakufa kwa cancer
Mpenda pombe sana utapata figo problem
 
Mimi sikubali kuwepo kwa mungu.

Unaweza kuthibitisha mungu wako yupo?
Mimi sijakuuliza kama unakataa au unakubali.
Endelea na biashara yako ndugu, pumzi zinakusumbua tu. Siku utaanza kukwea pipa na kukufikisha kilele cha Mlima Kilimanjaro au anga za mbali utaomba oxygen mask kwa asiyekuwepo.

Utathibitisha mwenyewe uwepo wa mungu wako, utakapokuwa kiakili na maarifa.

Kwa nini unataka uthibitishiwe uwepo wa mungu?
Itakusaidia nini?


 
Kuwepo kwa mungu hakujaweza kupita mtihani wa logical consistency.

Ukiwa mtoto, ni rahisi kuamini mungu, father Christmas, Santa Claus na vinyamkera vingine vingi. Kwa sababu akili inakuwa bado haijakua.

Ukikua, unatakiwa kuanza kuhoji habari za uwepo wa mungu kwa kuziweka katika mitihani ya logical consiatency.

Na mungu wenu anashindwa logical consistency.

Hayupo consistent. Anajipinga mwenyewe, kwa namna ambayo inaonyesha ni hadithi tu, hayupo kiukweli.
Nilicho kushauri ufanye hapa ni kueleza yale ambayo yalikuwa yanakufanya uamini uwepo wa mungu,kisha uanze kuchambua hapa ni vp hayo mambo hayana uhusiano na kuwepo kwa mungu.
Kama ulianza kuhoji na ukahitimisha kuwa hakuna mungu basi sie tunachotaka ni vp kuhusu yale yafanyayo watu waamini kuna mungu ueleze kutokuwa na uhusiano na uwepo wa mungu.
 
Hujanielewa???

Why not 50 or 60 and above?

Swali la msingi ni kwamba hiyo 70 umeitoa wapi? Kwa nini 70 ndo minimum na siyo namba nyinginre yoyote?

Kwa nini usisema from 80 and above or 100 and above?
Kasoma Zaburi 90: 10....lakini zaburi hii ilikua nI maneno ya Daudi....sidhani uchukulie maneno yake kuwa ndio sheria mtu afike umri huo afe!!! Hebu nieleweshe vizuri maana naona wengine wanaenda hadi miaka 130.
 
TOFAUTI KATI YA KIFO NA MAUTI
Pastor/Mwlm:Emmanuel

Shalom baada yakuzungu mzia dalili za mtu mwenye roho ya ( Jini mahaba Jana nilikuahidi kuwa nitaruditena kwa dalili za mtu mwenye roho ya mauti na dalili za mtu ambae nyota yake inashida

Leo ngoja nianze na "mauti"
Tujue kwanza nini maana ya mauti na kifo

1. MAANA YA KIFO NI NINI?
• Ni mwisho wa maisha ya kimwili au kiroho?
• Kukosa au kutokuwa na uhai.?
• Kutokwa na Roho / Pumzi?
• Ni hali ya kufarakana au kutengana kwa vitu au hali zinazofanya uhai kuwepo.
• Upo uhai wa aina tatu wa mwilini, nafsini na rohoni; vivyo hivyo na aina za kifo.

• KIFO NI HALI bali MAUTI ni Roho

2. MAANA YA MAUTI NI NINI?
• Ni roho inayoleta kifo au kukosekana kwa uzima ambao mtu amejaliwa na Mungu awe nao.
• Ni usingizi wa wa nafsi za mtu(yaani, mtu-roho,mtu-uhai, na mtu-mwili).
• Ni roho inayoifanya nafsi kutokuwa na uwezo wa kufanya chochote(inactive), akiwa hana ufahamu wowote au ana ufahamu lakini wa kukosa utashi, yaani kufanya maamuzi katika akili na kufanya chochote kile(akili kutiwa giza)!

Kumbuka kila kitu kabla hakijajidhihirisha kwenye mwili wa dam na nyama nilazima kianzie ndani kwanza hivyo ndani kuna mamlaka ( roho , nguvu) zinazosababisha mambo ya tokee kwa nje

3. SABABU YA MAUTI NI NINI?

• KUPINGANA NA MUNGU ALIYE UZIMA WA MILELE(kuwa adui wa Mungu) – husababisha Mauti/kifo!
• Dhambi na uasi dhidi ya Mungu
• Huzuni ya kidunia-kupoteza matumaini.
• Kuifuata nia ya Mwili badala ya nia ya Roho Mtakatifu.

Tunaona katika
Warumi 8:5
"Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. "


• Kutokuwa na Roho Mtakatifu wa Mungu.
• Kuingiliwa na / au Roho ya Mauti kumfunga mtu.
• Kukosa chakula na kinywaji cha kiroho.
• KUTOKUMUAMINI MUNGU KUPITIA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI!

• Kuingiliwa, kupagawa, kufungwa na kuwa chini ya shetani au mali ya shetani.
• Kupungukiwa na utukufu wa Mungu.

4. AINA ZA MAUTI:
zipo aina kuu mbili:
(1.)Kulala Usingizi wa Mauti
(1b)Kufa Mauti)
(2) MAUTI YA PILI.

I. MAUTI YA KWANZA Ipo Katika Namna /Aina Mbili:
i. AINA YA KWANZA YA MAUTI YA KWANZA NI (1)KULALA USINGIZI WA MAUTI
(2)Ni usingizi wa mauti – yaani kulala mauti.
• Roho ya Mauti – humwingilia na kumfunga mtu;

(Mfano wa kupata picha ya Mauti hii: wapo wanyama ambao kipindi cha uhaba wa chakula au baridi kali sana hulala usingizi wa mauti(hibernation) hadi kipindi kizuri; na tena wapo wadudu waitwao mavu au kuna aina ya manyigu yenye miguu ya rangi nyeusi na njano, ambao huandaa kiota cha udongo au shimo katika mti, na boriti za kenchi ya nyumba; na kisha huwakamata wadudu, na hasa hupendelea kuwamata buibui – kisha huwadunga mwiba wake(sting) wenye sumu inayomtia buibui huyo ganzi asiweze kuoza wala kufanya chochote, bali kulala kama maiti kwa siku nyingi, kiasi kwamba mayai ya mavu au nyigu huyo yaliyotagwa na kuwekwa pamoja na buibui huyo huanguliwa na kisha buibui hao huwa chakula na lishe kwa watoto wa nyigu au mavu huyo.) Ndivyo hata roho ya mauti humwingilia na kumfunga mtu(kumpagaa) kama yafanyavyo mapepo; na kumtia mtu GANZI KATIKA NAFSI YAKE inayomfanya mtu-uhai, mtu-mwili, au mtu-roho; kuwa katika USINGIZI WA MAUTI, na nafsi ya mtu huyo huwa katika hali ya kutoweza kufanya chochote au usingizi wa(milele)wa kutoweza kuamka tena(huwa maiti).

KATIKA HALI HII MTU HUZIKWA AKIWA AMELALA TU, KWAMBA HAJAFIKIA MWISHO WA MAISHA YAKE HAPA DUNIANI! KWA MAANA NYINGINE, KWA KUTOWEZA KUPAMBANUA KWETU ROHO YA MAUTI, TUMEWAZIKA WATU WENGI WAKIWA HAI NDANI YA MAJENEZA WASIOSTAHILI KUZIKWA! NA HIVYO HUPELEKEA WAO KUFIA WAKIWA WAMEFUKIWA MAKABURINI, AMBAO HAWAKUFA TOKEA HOSPITALINI AU NYUMBANI TULIKOWAONA KAMA WAMEKUFA!
Roho hii ni mbaya sana kwani ni ni roho wanayoitumia wachawi au waganga kuuwa watu kuwafanya misukule na ni roho ambayo huitumia pia kuuwa biashara kazi nyota mafanikio ya mtu elimu uchumi nk...

Roho hii hufanya vitu hivyo kuonekana kanakwamba vimekufa lakini viko hai unaweza kukuta mtu anakuambia mimi nilikuwa napata pesa sana hapo nyuma au nilikuwa napendwa sana na watu au nilikuwa nafanya biashara sana lakini sasa sijui kilichotokea,
Ukiona hivyo ujue kwenye ulimwengu wa Roho ni mamlaka hii ilitumika kuuwa hivyo vitu huwa vinakufa taratibu sana na kwenye ulimwengu wa roho huwa wachawi wana tumia sindano inayotitwa (syribock) hii ni sindano inayotengenezwa kwa njia za kipepo na hutumika kudunga watu biashara kazi hata chochote kile ili kife


Usishangae nimesema kazi biashara au ndoa hata pesa zinaweza kudungwa sindano hii kwenye ulimwengu wa roho kila kitu kina uhai hivyo ukiweza kuingia ( kuutumia ) ulimwengu wa roho unaweza kufanya chochote

[Waefeso 4:19; 17
Tunaweza tukaiona namna hii roho itendavyo kazi

"Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao; 18 ambao; AKILI ZAO ZIMETIWA GIZA, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao; 19 AMBAO WAKIISHA KUFA GANZI wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani. PILI:

Katika Injili ya Yohana 11: 9
Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. 10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. 11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, AKAWAAMBIA, RAFIKI YETU, LAZARO, AMELALA; LAKINI NINAKWENDA NIPATE KUMWAMSHA. 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini YESU ALIKUWA AMENENA HABARI YA MAUTI YAKE; NAO WALIDHANIA YA KUWA ANANENA HABARI YA KULALA USINGIZI. 14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. 15 Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake.]


• Katika aina hii ya mauti iliyokuwa imempata ndugu yetu Lazaro inategemea ni kwa kiwango gani mauti imemfunga au imemshika mtu; hivyo mtu huweza kuona anavyopelekwa kuwekwa kwenye jeneza hadi kuzikwa, lakini hawezi kufanya chchote ili kujitetea na kusema-sijafa! Biblia ina iita mauti ya namna hii ni mauti ya uchungu
"Na hapo ndipo ulipo uchungu wa mauti"

Na tena katika hali hii mtu anaweza asitambue chochote!
• AINA HII YA MAUTI ilishindwa kumshika BWANA YESU, hata akafufuka, akatoka kaburini yu hai milele!
• Kwa hiyo mtu akipona na mauti hii, hatapatikana tena na MAUTI ILE YA PILI!

• Wachawi na mapepo huitumia aina ya roho hii ya mauti katika kumfanya mtu kuwa msukule(ndondocha au zombie-mzuka), ili kuilaza nafsi ya mtu (mtu-mwili, mtu-uhai, au mtu-roho) katika USINGIZI WA MAUTI, kwa kuitwaa nafsi (wenyewe wanaita nyota, kingereza ni astral bodies) na kwenda kumtumikisha mtu huyo.
• Humfanya mtu-uhai kuwa inactive/hibernate, hivyo hapumui mwilini kama buibui aliyetiwa ganzi na nyigu au mnyama alalaye usingizi wa mauti kipindi cha baridi kali alalavyo!
• Humfanya mwanadamu afe kabla ya wakati ule uliokusudiwa au uliopangwa na Mungu kwa mtu huyo kuondoka duniani, na kumuingiza katika ulimwengo wa kiroho!

Isaya 57:3
" Lakini ninyi karibuni hapa, enyi wana wa mwanamke mchawi, uzao wa mzinzi na kahaba. 4 Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani? Mmepanua vinywa vyenu, na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo; 5 ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi; ninyi mnaoua watoto mabondeni, chini ya mianya ya majabali? 6 Sehemu yako i katika makokoto ya bonde; hayo ndiyo kura yako; umeyamwagia hayo sadaka ya kinywaji, umeyatolea sadaka ya unga; je! Niwe radhi na mambo hayo? 7 Umeweka kitanda chako juu ya mlima mrefu ulioinuka sana; ukaenda huko ili kutoa dhabihu. 8 Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona. 9 Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata kuzimu.

Hapa ni aina hii ya roho ndiyo iliyo kuwa inazungumziwa


Isaya 28:15
15 Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;
Hii ni roho mbaya sana huwa ni roho ya maagano ikimwingia mtu au biashara au ndoa au kazi ya mtu ni lazima ujue ni agano gani lililofanyika ndipo uweze kuitoa

Agano maanake ni mapatano mkataba uliofanywa na pande mbili na kutokana mahali penye agano la roho hii ya mauti ni agano linalofanywa kati ya mhusika mauti na mizimu agano hili huwa na nguvu sana, ndio maana kama wachawi wakifanya agano hili kwenye kazi ndoa au chochote kile kwenye maisha yako kulivunja ni ngumu sana tuna watu wengi wana shida matatizo ya kiuchumi na wengi roho hii ya mauti ndio iliyotumwa kwao sasa ukiwambia MTU atulie utatuzi uendelee kutafuta taratibu anataka muujiza ya hapo hapo acha ni kuhakikishie kama roho hii IPO itabidi uzame sana kwenye maombi

• Katika kifo hiki, roho inakuwa bado haijaingia paradiso wala kuzimu; HAPA NDIPO INATAKIWA KUIKEMEAA ROHO YA MAUTI IMWACHIE MTU, kwani hajafikia mwisho wa safari yake hapa duniani, NAYE ATARUDI KUWA HAI TENA! kwani roho ikishingia paradiso au kuzimu, huo ndio mwisho wa mtu huyo kuishi hapa duniani! Na ni kwamba anasubiri tu kwenda mbinguni au jehanamu!

Ikumbukwe biblia inasema " msiwaogope wauuao mwili wasiweze kuua roho" hivyo MTU aliye uawa kwa roho hii roho yake nitaendelea kubaki mpaka wakati wa Mungu kuiondoa hiyo roho kufika

• Mfalme Daudi katik Zaburi 23: anautaja usingizi wa mauti kama bonde la uvuli wa mauti.

II. AINA YA PILI YA MAUTI YA KWANZA NI - KUFA MAUTI ( 1.Kwa Baraka 2. Kwa Laana)
• Ni kuondoka hapa duniani baada ya kutimiza kusudi la Mungu.
• Ni roho au nafsi ya mtu kufikia mwisho wa maisha yake hapa duniani kwa namna mbili zifuatazo:
• Ni kuufikia siku ile ya kuuvua mwili wa nyama ili kuuvaa mwili ule wa roho.

Nitaendelea zaidi kwa somo hili
Asomae na afaham inawezekana mambo haya yakawa magumu sana kwako najaribu kumsihi Mungu anipe lugha rahisi zaidi ya kukufikishia jumbe hizi iliuelewe endelea kusoma na kusoma itakusaidia

Mungu akubariki
Pastor/Mwlm :Emmanuel
 
Kasoma Zaburi 90: 10....lakini zaburi hii ilikua nI maneno ya Daudi....sidhani uchukulie maneno yake kuwa ndio sheria mtu afike umri huo afe!!! Hebu nieleweshe vizuri maana naona wengine wanaenda hadi miaka 130.

Kumbe imeandikwa kwenye bible!! Fine.

NB:Mimi siyo mchungaji.

Zaburi 90:10.

Siku za miaka yetu ni miaka sabini,Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini.Kiburi chake ni taabu na ubatili.Maana chapita upesi tukatokomea mara.


Je hilo andiko ndilo limemfanya mtoa mada kufanya hitimisho lake?Yuko sahihi?

Kwa mujibu wa andiko hilo miaka 70 ni umri elekezi wa sehemu aliyokuwa akiishi mwandishi na nyakati hizo.

Swali:Huyo mwadishi aliishi wapi na lini? Je alifanya utafiti wa hiyo life expectancy mpaka tuliko sisi?lini?

Hiyo life expectancy ni fixed kwa miaka yote na sehemu zote? Why and how?
 
Mimi sijakuuliza kama unakataa au unakubali.
Endelea na biashara yako ndugu, pumzi zinakusumbua tu. Siku utaanza kukwea pipa na kukufikisha kilele cha Mlima Kilimanjaro au anga za mbali utaomba oxygen mask kwa asiyekuwepo.

Utathibitisha mwenyewe uwepo wa mungu wako, utakapokuwa kiakili na maarifa.

Kwa nini unataka uthibitishiwe uwepo wa mungu?
Itakusaidia nini?



Hujajibu swali nililokuuliza.

Hujathibitisha kuwapo kwa mungu.

Huwezi kuthibitisha kuwepo kwa mungu huyu.

Kwa sababu hayupo.
 
Nilicho kushauri ufanye hapa ni kueleza yale ambayo yalikuwa yanakufanya uamini uwepo wa mungu,kisha uanze kuchambua hapa ni vp hayo mambo hayana uhusiano na kuwepo kwa mungu.
Kama ulianza kuhoji na ukahitimisha kuwa hakuna mungu basi sie tunachotaka ni vp kuhusu yale yafanyayo watu waamini kuna mungu ueleze kutokuwa na uhusiano na uwepo wa mungu.
Yafanyayo watu kuamini uwepo wa mungu kama yapi?
 
Hujanielewa???

Why not 50 or 60 and above?

Swali la msingi ni kwamba hiyo 70 umeitoa wapi? Kwa nini 70 ndo minimum na siyo namba nyinginre yoyote?

Kwa nini usisema from 80 and above or 100 and above?

Mkuu number ya miaka isikusumbue, ni hivi kifo cha uzeeni ni mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo miaka ya uzeeni yeyote ndio maana yangu.
 
Hujajibu swali nililokuuliza.

Hujathibitisha kuwapo kwa mungu.

Huwezi kuthibitisha kuwepo kwa mungu huyu.

Kwa sababu hayupo.
Wacha janja yako: Anza wewe na post #69 na #79
 
Kwako wewe mungu ni nini?
Kwa nini huwezi kufananisha binadamu na mungu?
mungu yupi asiyekuwepo?
Hii post nishakujibu maswali yote, lakini umeitaja nikujibu, nakujibu tena.

Kwangu mimi mungu ni hadithi ya kufikirika ya kitu kisichopo na kisichoweza kuwapo kama "pembetatu duara" katika Euclidean Geometry.

Pembetatu duara haiwezi kuwepo kwa sababu ina "inherrent contradiction", mungu wenu mnayemsema hawezi kuwepo kwani naye ana inherrent contradiction. Upande mmoja tunaambiwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, upande mwingine tunaona kaumba ulimwengu ambao umewezekana kuwa na mabaya mengi na mateso mengi. This is an inherrent contradiction on a par with "pembetatu duara".

Ukiamini mungu huyu yupo ni sawa sawa na mtu anayeamini "pembetatu duara" ipo.

Both are inherrent contradictions.

Kwa nini huwezi kufananisha mungu na binadamu?

Kufananisha vitu ni lazima ufananishe vinavyofanana.

Huwezi kulinganisha barabara na wimbo wa taifa. Unalinganisha barabara na barabara na wimbo kwa wimbo.

Sasa utalinganishaje mungu, ambaye unasema ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote uende kumlinganisha na binadamu ambaye hana ujuzi wote, upendo wote wala uwezo wote?

Mungu yupi asiyekuwepo?

Huyo unayesema yupo na kuweka mipost kibao hapa kumtetea.

Thibitisha kwamba yupo kama unasema yupo bado.
 
Mimi sikubali kuwepo kwa mungu.

Unaweza kuthibitisha mungu wako yupo?

kiranga! sasa tufanye hivi niruhusu nikuombee upate matatizo makubwa wewe na familia yako, Hapo utathibitisha mwenyewe kuwa Mungu yupo au hayupo. Je unaniruhusu?
 
Back
Top Bottom