Kifo ndiyo mapumziko

Ingekuwapo option ya kubaki duniani wengi tungeifuata
TAFUTA PESA kijannah huko hakuna mapumziko tena kama kwa wale wanaodai kuna kuchomwa moto hayo mapumziko yako wapi...??


Bora tu nibaki zangu duniani na pesa zangu.
 
Na kanisa ni moja
KATORIKI, TAKATIFU LA MITUME
 
Nyakati zinapokuwa ngumu maishani basi binadamu hutafuta suluhisho la kudumu
 
Una experience na huko? Unaandika kwa kujiamini kana kwamba ulishawahi kwenda ukaona na kurudi, dini zisiwapumbaze hakuna anayejua uhalisia nini kinaendelea baada ya kufa.
Husomagi neno la Mungu?

"Yesu akamwambia, Amin nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi" LUKA 23:43.

huyu ni mtu mmoja mhalifu aliyekuwa ameuawa msalabani pamoja na Yesu akawa amemwomba Yesu amkumbuke katika Ufalme wake. Bwana Yesu hakumkatalia maombi yake. Huu ni uthibitisho kuwa kuna maisha baada ya haya ya duniani.


YESU NI MWOKOZI
 
Luka 16 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
²⁰ Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
²¹ naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
²² Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
²³ Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
²⁴ Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
²⁵ Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
²⁶ Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
²⁷ Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
²⁸ kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
²⁹ Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
³⁰ Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
³¹ Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.



Huu ni ushahidi mkubwa kuwa kuna maisha baada ya kifo. Aidha raha pamoja na Yesu au tabu na mateso pamoja na mashetani. Muda wa kuchagua ni sasa.
 
Ayubu 14 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
² Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.


Maisha ya duniani ni mafupi sana, hata ungekaa miaka 90 au mia. Ni mafupi sana ukilinganisha na yale ya milele pamoja na Mungu. Amua kumkabidhi Bwana Yesu maisha yako leo.
 
Yah ni kweli kifo ni mapumziko lakini ni kama utayaandaa hayo mapumziko ukiwa hai. Vinginevyo ni kibano mfululizo milele.
Tuombe sana Allah atujaalie tuwe miongoni mwa watakaopumzika. Aamin.
 
Amina Baba Mtumishi
 
Kifo ni Ibadan,kwetu huku kila wiki tunazika,ibilisi mtoa roho kaweka kiti kabisa Kanda yetu
Kifo kipo Kila sehemu mkuu,Ndio Maana hakuna kijiji kisicho na Shamba la kuzikia wafu,labda kule kwa Wahindi ambako maiti huchomwa moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…