Kifo ndiyo mapumziko

Kifo ndiyo mapumziko

Ingekuwapo option ya kubaki duniani wengi tungeifuata
TAFUTA PESA kijannah huko hakuna mapumziko tena kama kwa wale wanaodai kuna kuchomwa moto hayo mapumziko yako wapi...??


Bora tu nibaki zangu duniani na pesa zangu.
 
Ni sahihi, duniani hakuna raha kamilifu. Furaha na raha kamilifu iko peponi (paradiso). Hii hupatika kwa kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi.

Kwa upande wa pili (kuzimu) kuna mateso na shida zaidi ya hapa duniani. Hivyo kila mmoja aitafute pepo kwa kuitumia neema iliyopo sasa (APOKEE WOKOVU), ili apate maisha ya raha atokapo kwenye hii dunia.


YESU NI BWANA NA MWOKOZI
Na kanisa ni moja
KATORIKI, TAKATIFU LA MITUME
 
Kuna siku nilikuwa nakwenda kazini, nikawa napita kwa rafiki yangu mmoja kumjulia hali.

Nikamkuta amelala kitandani amenyong'onyea.

Nikamuuliza vipi hali, mbona hivyo?

Akasema hajisikii vizuri.

Tukaongea mambo gani sijui, topic ikaenda kwenye kifo.

Nikawa nasema maneno kama haya ya kifo ni mapumziko, kidhahania sana.

Kesho yake nikapata habari yule kijana alijipiga risasi kwao.

Iliniuma sana, nikajiuliza sana kama yale mazungumzo yangu yalichangia maamuzi yake yale.

Toka siku hiyo, nakuwa muangalifu sana kufanya maongezi haya ambayo yanaweza kuwa na suicide ideation triggers yakawafanya watu wengine waone kujiua ni poa tu.
Nyakati zinapokuwa ngumu maishani basi binadamu hutafuta suluhisho la kudumu
 
Una experience na huko? Unaandika kwa kujiamini kana kwamba ulishawahi kwenda ukaona na kurudi, dini zisiwapumbaze hakuna anayejua uhalisia nini kinaendelea baada ya kufa.
Husomagi neno la Mungu?

"Yesu akamwambia, Amin nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi" LUKA 23:43.

huyu ni mtu mmoja mhalifu aliyekuwa ameuawa msalabani pamoja na Yesu akawa amemwomba Yesu amkumbuke katika Ufalme wake. Bwana Yesu hakumkatalia maombi yake. Huu ni uthibitisho kuwa kuna maisha baada ya haya ya duniani.


YESU NI MWOKOZI
 
Luka 16 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
²⁰ Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
²¹ naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
²² Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
²³ Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
²⁴ Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
²⁵ Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
²⁶ Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
²⁷ Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
²⁸ kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
²⁹ Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
³⁰ Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
³¹ Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.



Huu ni ushahidi mkubwa kuwa kuna maisha baada ya kifo. Aidha raha pamoja na Yesu au tabu na mateso pamoja na mashetani. Muda wa kuchagua ni sasa.
 
Ayubu 14 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
² Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.


Maisha ya duniani ni mafupi sana, hata ungekaa miaka 90 au mia. Ni mafupi sana ukilinganisha na yale ya milele pamoja na Mungu. Amua kumkabidhi Bwana Yesu maisha yako leo.
 
Yah ni kweli kifo ni mapumziko lakini ni kama utayaandaa hayo mapumziko ukiwa hai. Vinginevyo ni kibano mfululizo milele.
Tuombe sana Allah atujaalie tuwe miongoni mwa watakaopumzika. Aamin.
 
Ni sahihi, duniani hakuna raha kamilifu. Furaha na raha kamilifu iko peponi (paradiso). Hii hupatika kwa kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi.

Kwa upande wa pili (kuzimu) kuna mateso na shida zaidi ya hapa duniani. Hivyo kila mmoja aitafute pepo kwa kuitumia neema iliyopo sasa (APOKEE WOKOVU), ili apate maisha ya raha atokapo kwenye hii dunia.


YESU NI BWANA NA MWOKOZI
Amina Baba Mtumishi
 
Back
Top Bottom