Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Misingi ya uhalisia wangu ni tofauti na misingi ya uhalisia wako.Hujafikiria kwamba huwezi kuthibitisha uwepo wa hiyo mbingu kwa sababu haipo kiuhalisia, ni ya kwenye hadithi za kuungwaungwa na watu tu?
Katika uhalisia wako ndio hakuna mbingu, kifo kinakuwa mwisho wa yote. Kifo. Baada ya hapa inakuwa ni kama vile hukuwahi tu hata kuwepo.
Katika uhalisia wangu mbingu ipo na kifo ni hatua. Hivyo kifo ni pumziko la muda. Baada ya hapo nitakuwa na kazi ya kufanya na changamoto mpya za kutatua.