Kifo ndiyo mapumziko

Kifo ndiyo mapumziko

Hujafikiria kwamba huwezi kuthibitisha uwepo wa hiyo mbingu kwa sababu haipo kiuhalisia, ni ya kwenye hadithi za kuungwaungwa na watu tu?
Misingi ya uhalisia wangu ni tofauti na misingi ya uhalisia wako.

Katika uhalisia wako ndio hakuna mbingu, kifo kinakuwa mwisho wa yote. Kifo. Baada ya hapa inakuwa ni kama vile hukuwahi tu hata kuwepo.

Katika uhalisia wangu mbingu ipo na kifo ni hatua. Hivyo kifo ni pumziko la muda. Baada ya hapo nitakuwa na kazi ya kufanya na changamoto mpya za kutatua.
 
Kupumzika kuna maana kwa yule atakayeamka tena na kutumia nguvu alizojichaji wakati wa mapumziko.

Kupumzika jumla hakupo. Hicho kinaitwa kifo.

Anayepumzika ni yule ambaye bado ataendelea kuwa na majukumu na wajibu wa kutimiza. Mifano ndo hayo mambo umeorodhesha.
Hapana, huhitaji kuamka tena ili uweze kupumzika.

Kwa sababu, hata mtu aliyelala usingizi masaa 10, akafariki katikati ya usingizi wake kabla hajaamka, yale masaa 10 aliyokuwa kalala alikuwa kapumzika pia.

Hatuhitaji aamke asubuhi ili tuseme kuwa alipumzika usingizini kwa masaa 10 kabla ya kufariki.
 
Naona kupumzika huku alikomaanisha mtoa mada ni kuondoka Kwa masaibu,changamoto za Dunia baada ya kufariki, kitakachotokea huko ulipokwenda baada ya kufa naona ni jambo la mtazamo...maana ukifa changamoto za uso wa Dunia nazo huondoka kama ni hivyo basi huko ni kupumzika pia.
Umeupiga mwingi
 
Hapana, huhitaji kuamka tena ili uweze kupumzika.

Kwa sababu, hata mtu aliyelala usingizi masaa 10, akafariki katikati ya usingizi wake kabla hajaamka, yale masaa 10 aliyokuwa kalala alikuwa kapumzika pia.

Hatuhitaji aamke asubuhi ili tuseme kuwa alipumzika usingizini kwa masaa 10 kabla ya kufariki.
Kupumzika kuna maana kwa atakayeamka.

Asipoamka kupumzika kwake hakuna maana hata.

Ndio maana nikasema hata kwenye kifo. Mtu akipumzika hiyo mazima asije kuamka abadani. Atarealize vipi hata kama amepumzika? Ila akiamka ndio atajua kuwa alipumzika.

Kwa hiyo baada ya maisha haya kuna mawili tu 1. Kupumzika mwanzo mwisho(Kifo) 2. Kupumzika kwa muda.

Matokeo baada ya kifo ni zzzz, nada, none, zero.
Matokeo baada ya kupumzika ni kuamka na kuanza kutekeleza majukumu mengine.
 
Mkuu,

Mbona unaacha kuongelea "kupumzika ni nini" unakwenda kwenye swali tofauti la "kupumzika kuna maana kwa nani"?

Mkuu,

Ikiwa katika maisha yako kila siku, kila saa, kila dakika unacharazwa mijeledi ile ya mkia wa taa, halafu kifo kinaenda kukufanya usisikie hayo maumivu wala usiwe na ufahamu, utasema hapo napo kupumzika hakuna maana kwa sababu ukifa hufahamu kitu? Huoni kwamba huko kutofahamu kitu ndiyo afadhali yenyewe inayoleta maana ya kupumzika, umepumzika kutoka maumivu ya maisha na kuepuka maisha ya maumivu makali kila siku?
 
Misingi ya uhalisia wangu ni tofauti na misingi ya uhalisia wako.

Katika uhalisia wako ndio hakuna mbingu, kifo kinakuwa mwisho wa yote. Kifo. Baada ya hapa inakuwa ni kama vile hukuwahi tu hata kuwepo.

Katika uhalisia wangu mbingu ipo na kifo ni hatua. Hivyo kifo ni pumziko la muda. Baada ya hapo nitakuwa na kazi ya kufanya na changamoto mpya za kutatua.
Sawa, lakini uhalisia wako hauna mantiki, umetokana na hadithi za kuungwaungwa na watu tu, na imani ya Mungu asiyekuwapo, ambaye tukimchambua kimantiki ataonekana kuwa na contradictions nyingi tu.

Uhalisia wangu hauna tatizo hilo la contradictions za kimantiki.
 
Mnajuaje mnaenda kupumzika wakuu! Mi sitaki kabisa hili jambo 😂
 
Mbona unaacha kuongelea "kupumzika ni nini" unakwenda kwenye swali tofauti la "kupumzika kuna maana kwa nani"?
Suala la kufafanua kupumzika ni nini tukilifafanua mwisho wa siku inabidi lilete maana kwa fulani mwenye uwezo wa kun'gamua maana yenyewe (some conscious being).

Mimi nimeenda mojakwa moja kwa subject mwenyewe maana mwisho wa siku yeye ndiye atakayeexperience maana hiyo. Na jambo jenyewe ni subjective ni personal. Huwezi ukapumzika kwa niaba ya fulani, huwezi kuelewa kwa niaba ya fulani na ikawa na maana kwake.

uhalisia wako hauna mantiki, umetokana na hadithi za kuungwaungwa na watu tu, na imani ya Mungu asiyekuwapo, ambaye tukimchambua kimantiki ataonekana kuwa na contradictions nyingi tu.

Uhalisia wangu hauna tatizo hilo la contradictions za kimantiki.
Chief, tungeweza kuendelea zaidi na majadiliano humu. Hatutamaliza. Lakini haitapendeza hii thread itrend sana. Wakati ingefaa kinyume chake; usiendelee kuwepo.

Sababu ni ulizotoa mwanzo kwamba inatrigger suicidal ideation kwa wanyonge walio-vulnarable. Nakubaliana nazo asilimia zote. Tafiti zinaonesha ikitokea mtu mmoja kajitoa uhai kuna mtindo wa kutrend 'fasheni' ya watu kujidedisha wanaiga.

Moderator Mhariri ingefaa huu uzi ufutwe ili kulinda afya za walaji.

Uhuru unadhibitiwa, na linapokuja suala la kuilinda jamii na vifo na majanga. Mna sababu zilizojitosheleza kuufunga huu uzi.
 
Suala la kufafanua kupumzika ni nini tukilifafanua mwisho wa siku inabidi lilete maana kwa fulani mwenye uwezo wa kun'gamua maana yenyewe (some conscious being).

Mimi nimeenda mojakwa moja kwa subject mwenyewe maana mwisho wa siku yeye ndiye atakayeexperience maana hiyo. Na jambo jenyewe ni subjective ni personal. Huwezi ukapumzika kwa niaba ya fulani, huwezi kuelewa kwa niaba ya fulani na ikawa na maana kwake.

Chief, tungeweza kuendelea zaidi na majadiliano humu. Hatutamaliza. Lakini haitapendeza hii thread itrend sana. Wakati ingefaa kinyume chake; usiendelee kuwepo.

Sababu ni ulizotoa mwanzo kwamba inatrigger suicidal ideation kwa wanyonge walio-vulnarable. Nakubaliana nazo asilimia zote. Tafiti zinaonesha ikitokea mtu mmoja kajitoa uhai kuna mtindo wa kutrend 'fasheni' ya watu kujidedisha wanaiga.

Moderator Mhariri ingefaa huu uzi ufutwe ili kulinda afya za walaji.

Uhuru unadhibitiwa, na linapokuja suala la kuilinda jamii na vifo na majanga. Mna sababu zilizojitosheleza kuufunga huu uzi.
Sababu hazitoshi kuufuta Uzi huu! Hizo unazoziona kama sababu za kuufuta Uzi huu zitahalalisha kuwa mafundisho mengi ya kidini ni batili kwa sababu yanaeleza uwepo wa maisha baada ya duniani.
 
Sababu hazitoshi kuufuta Uzi huu! Hizo unazoziona kama sababu za kuufuta Uzi huu zitahalalisha kuwa mafundisho mengi ya kidini ni batili kwa sababu yanaeleza uwepo wa maisha baada ya duniani.
Dah,

Yani nimejaribu kumuelewa mkuu, lakini umekaba mpaka penati ?

Kwa hivyo ndiyo kusema mkuu anatumia hoja yangu ya suicide ideation kama exit strategy tu au vipi?

Maana mimi nilishaona labda ana point nikae kimya tusipromote suicide triggering threads kama nilivyosema awali.
 
Anajificha kwenye shamba la karanga
 
Husomagi neno la Mungu?

"Yesu akamwambia, Amin nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi" LUKA 23:43.

huyu ni mtu mmoja mhalifu aliyekuwa ameuawa msalabani pamoja na Yesu akawa amemwomba Yesu amkumbuke katika Ufalme wake. Bwana Yesu hakumkatalia maombi yake. Huu ni uthibitisho kuwa kuna maisha baada ya haya ya duniani.

YESU NI MWOKOZI
Hiyo biblia katika muhubiri haisemi wafu hawajui neno lolote?
 
Hiyo biblia katika muhubiri haisemi wafu hawajui neno lolote?
WAFU, Hawajui neno lolote kwa kinachoendelea duniani. Yaani hawana tena connection na dunia. Wanayajua ya hukohuko waliko. Ndio maana ni upuzi kuwaomba ama kuwaombea wafu. Na ni machukizo mbele za Bwana.

YESU ANAOKOA
 
Kumbukumbu la Torati 18 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁰ Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
¹¹ wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
¹² Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
 
Kifo ndio uhuru wa kweli,utanishangaza kama utapinga kuwa duniani hakuna uhuru...uhuru wa kweli upo kaburini
Bro!upo sawa sawa?umekata tamaa kiasi hiki?hakuna anayejua "uhuru wa huko"kaburini.
Ni story za kusadikika TU,hakuna uthibitisho.
 
Kifo hajawahi kuwa adui wa mpenda aman ya ndani(Inner Peace)
 
Ondoeni hofu, ukifa hautahisi chochote wala kujua nini kinaendelea. Itakuwa kama zile siku ambazo bado hujazaliwa.

Baada ya miaka 100 utakuwa ushasahaulika kabisa katika uso wa dunia ukitoa 0.0001% ya watu maalumu watakao kuwa wanakumbukwa.
 
Hapo awali nilidhani ukiwa na hali fulani ya maisha unaweza kuwa na furaha muda mwingi wa maisha yako. Ukweli mchungu!

Ili binadamu apate pumziko halisi kimwili na kiakili basi aishi sehemu tofauti na hii Dunia.

Haijalishi ni mtu wa hali ipi kimaisha wote tunadondokea kwenye mtumbwi mmoja.

Njia pekee ya kuepuka ni kifo tu na hapo ndipo unaweza tengana na vurugu za duniani.
Mkuu usikate tamaa
 
Ungepewa nafasi ya kuamua uzaliwe au usizaliwe, yani unayaona maisha yako yote halafu unaulizwa, je, utakubali uzaliwe uishi maisha haya au unakataa, ungeamua vipi?

Hapo umepewa nafasi ya kuyakubali au kuyakataa maisha haya bila kifo kutokea, unaamua uzaliwe au usizaliwe.

Ungeamuaje?
 
Back
Top Bottom