Kifuani nina mzigo wa hasira na kisasi, mgoni wangu kuwa makini

Kifuani nina mzigo wa hasira na kisasi, mgoni wangu kuwa makini

Kuna masela wanatoa hii huduma ni pesa yako tu, atatezeka hadi utamuonea huruma😁👇
images (100).jpeg
 
Sio uoga ndugu Ninatafuta unafuu moyoni mwangu kwakua Sasa Hivi nnagadhabu kubwa mnoo inaniumiza mwenyewe

Unaugua ugonjwa unaoitwa Oneitis, kwamba wewe ni boya na maisha yako yote unaona yapo kwa huyo mwanamke....na wameshajua wanakuumiza ndio maana!!...fanya hivi hasira zako kazimalizie gym tengeneza mwili, piga kazi sana tafuta pesa baada ya mwaka utaona matokeo lazima mwanamke ajirudisha mwenyewe na mwisho tafuta mtoto mzuri zaidi yake. Thats the best revenge
 
Binadamu tupo wa aina nyingi sana yaan kuna watu starehe yao kugonga wake za watu tu [emoji34][emoji34][emoji34]
Halafu wanawake nao inakuaje mke wa mtu unashoboka na wanaume nje ya mumeo

Washaachana hao
Sasa anataka akimuacha mwanamke asiwe na mahusiano mengine?
 
Nakosa maneno ya kukushauri. Nakuombea mungu akupe uwezo wa kumpuuza huyo mwanamke.
Hajaona thamani yako kwanini wewe unamuonesha kua anathamani kubwa kwako kiasi uko tayari kuyaharibu maisha yako na ya watoto wako kwa ajili yake? Ana thamani kiasi hicho?
Jiulize.
Then muone tu mtu kama watu wengine na wengi tu wamefanyiwa kama wewe au zaidi wakaumia baadae waka move on na wakapata furaha zaidi.Ni swala la muda tu uchungu huo utaisha.
 
Bora niteseke jela kuliko jinsi nnavyoumia moyoni
Ukateseke jela na wanao uwaache wenyewe.
Dunia ilivyojaa uzandiki hii?
Wafanywe mashoga na majambazi?
Wadhulumiwe Mali zako?
Wakose elimu?
Wanatizamwa na nani?
Ndoa ni nini kiasi isimamishe maisha yako kila leo unapost kuhusu same stuff?

Huyu mwanamke unayelia lia nae kila siku in the name ya kuwa una hasira sijui ntamkomesha mbona hana hata wazo na wewe?
Imeenda iache iende.
KUBALI KUSHINDWA.
Kwani kukubali defeat shilingi ngapi?
Kuna vita kupigana hata ukishinda ulishashindwa mwanzo.

Una mambo mengi ya msingi kutizama kuliko kulipa kisasi.
Watoto wako wanakuhitaji kuliko huyo unayejiapiza kummaliza.
Mwenzio anaendelea na maisha yake wee yako unaweka rehani!!
Mxxxxxxiiiew
Haitakusaidia.
Haitakurudishia mke.
Haitarejesha ndoa yako.
Some of us here we are best losers.
We Win while Defeated.
Think!
Think!
Think!
 
Achana na hizo mambo utajifia presha na magonjwa mengine bure .
Hizo nguvu Peleka kwenye kutafuta pesa acha kulia Lia eti umemlipia Mahari.
Hao watoto unaosema watateseka pengine sio wako vile vile.
 
Back
Top Bottom