Kifuatacho baada ya Job Ndugai kujiuzulu, tukae mkao wa kula

Hiki ndo nilichouliza kwenye uzi wangu fulani, ile dhana ya bunge kuwa muhimili huru wa kuishauri na kuisimamia serikali itabaki baada ya ndugai kuondoka, au bunge sasa litaenda kuufyata.........litabaki kupiga makofi tu wakati chifu na madelu wakiendelea kusaka mikopo popote ilipo......
 
Toka kwa hayati JPM ubovu wa katiba yetu ulijionyesha wazi kbsa na sasa ivi ndo kbsa inaonekana live bila chenga, siku jaji mkuu nea akizingua ataona cha moto, makamu wa raisi nae cku akiwa na mawazo tofauti kidogo na raisi kazi anayo, hivyo hivyo kwa waziri mkuu mpaka kwa watendaji wa huku chini kabisa. Katiba mpya ni suala la muda tuu ila lazima ije iwe leo, kesho ama kesho kutwa
 
Eti political trap [emoji23] [emoji1787]
Waswahili hatuna kumbukumbu katika bongo zetu huwa zinafuta haraka sana

Hata kama una PhD bado kukumbuka ni zero

Walipodukuliwa wale walikuwa wanasema jamaa ni Mshamba
Mlikejeli sana
Ila mkasahau kuwa hata nyie mnadukuliwa kila leo

Hujiulizi kwanini baada ya kuomba msamaha akajiuzuru baada ya hapo?
 
Bado sijakupata vizuri ndugu....hoja yako hapa ni ipi ukiachana na mambo za kidukulilo na kudukuliwa.

Naomba ufafanuzi wako,unajaribu kumaanisha nini yaani.
 
Mjadala ufungwe hapa.
 
Duu wewe somo la presidential Government vs parliamentary government ulielewa vizuri sana.
 
GT wameelewa hii kitu..moto wa Katiba unakuja kwa mbaali TL na Glema
 
Kuondoka kwa ndugai kumenifanya nione mapungufu mengi sana kimfumo

1 . Hii nchi ina mhimili moja tu hizi zingine geresha
2. Hoja za mashiko hazipewi nafasi
3. Tunako elekea wimbo wa katiba mpya tutaimba wote ...muda ni mwalimu mzuri
Mkuu nchi Hii ina Mihimili mitatu, lakini Hii miwili iliyobaki yote wasimamizi wa Hii Mihimili wako under roof ya Huyo mwenzao.
1. Rais ambae ni m/kiti wa chama anapendekeza yy Jina la mtu Kuwa spika

2. Rais ambae ni mkuu wa muhimili wa Regime yy ndio anaemteua Mtu Kuwa CJ

So wote hawa wanadepend kwa hyo anaewateua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hapa ndo ule ule ukweli kuwa tuna mhimili mmoja wenye nguvu kuliko mingine unadhihirika.

Tukubali tu kuwa hatuna mihimili mitatu iliyo huru na yenye usawa.
 
Bado sijakupata vizuri ndugu....hoja yako hapa ni ipi ukiachana na mambo za kidukulilo na kudukuliwa.

Naomba ufafanuzi wako,unajaribu kumaanisha nini yaani.

Ni hapo unaposema “mtego” ninavyoona hatakuwa na nguvu tena ya kufanya kitu ni kama wamevunja miguu
Siasa za Africa tunazijua wote na nchi nyingi Rais ana nguvu sana na kuweza kufanya chochote

Katiba inahitajika sawa lakini Job alikuwa na nguvu akiwa kwenye kile kiti ila sasa atabaki kipiga meza tu kama na Ubunge hataachia ni hayo tu
 
Mnacheza ngoma wanayopiga wao mtaangaika sana na mtawaza na kutafakari sana ila jua CCm ni chama kinachotumia akili sana kuliko maneno na mihemko ya kisiasa

**** uliwai kufuatilia issue ya Rowasa kipindi kile anataka uraisi bas utaelewa kwa nn CCm ni chama kinachotumia akili kuliko chama chochote kile Africa

Wengi walitegemea lowasa ataiua au kuivunja ata kuizoofisha Ccm ila kilicho mkuta ata yy hakuamin alitoka akajikuta katoka pekeake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…