Ad majorem
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 939
- 1,460
Kwani Magufuli aliwahi kusema wizi serikalini umeisha?Vita dhidi ya ufisadi ni endelevu. JPM alipambana kwa nafasi yake na alifanikiwa pakubwa. Sote tunakumbuka sakata la Flowmeter ya mafuta na yule mwarabu wa Kigamboni aliyekua katoboa Bomba la Mafuta na kuyachanel kwake. Ni mjinga tuu atakayemlaum Magu katika hili.Usingeambiwa sasa kama kuna wizi, ungeendelea kufichwa tu
Sio rahisi upigaji kama huo kusiwe na mkono wa vigogo serikalini.
Halafu wale teeth wa kipindi Cha mwenda zake walikuwa wapi? Maana tunaambiwa walikuwa hatari balsa
Hivi kwa mfano wangekuwa ni magaidi na kuamua kulipua hayo mapipa ya mafuta si walikuwa washafanikiwa.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama wamebaini nyumba iliyopo mtaa wa Ugindoni iliyotandazwa mashine zinazotumika kuchimba visima vya maji lakini badala ya kuchimba chini kuelekea maji yalipo, wanachimba kuelekea usawa yalipo mabomba ya mafuta yanayotoka baharini kuelekea bandarini.
Mafuta hayo yanachukuliwa baada ya 'flow meter' kusoma na kutambulika yamepokelewa nchini lakini kabla ya kufika kituo cha mwisho ndipo mabomba hayo yanapoelekea.
Ndani ya nyumba hiyo kuna mashine na mipira ambayo inavuta mafuta na kujazwa. Nyumba hiyo ina ulinzi mkubwa na taarifa za awali zinasema muhusika amepangisha eneo hilo lenye kodi ya milioni 60 kwa mwaka huku akiwa amelipa miaka miwili na hakuna shughuli inayoendelea zaidi ya kisima ambacho mabomba yake yanaelekea baharini.
=========
Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana
Tukumbushane LIKE OIL ni ya nani???Wahusika wote wakamatwe, akiwemo mmiliki wa hiyo nyumba na wenye hayo malori kama yanavyoonekana hapo kampuni ya LAKE OIL.
Aliyemteua ni nani huyo IGP? Ukiteua watu wabovu lawama lazima zirudi kwakoKwani Magu ndiyo alikua IGP au DCI!? Lawama zote alaumiwe IGP!!
Usishangae kamanda wa kanda maalum ndiye alikuwa anatoa lindo kwa nyumba ile.nimeona hiyo taarifa Jana kupitia kituo cha Chanel ten kwakweli inatisha!!!
kweli Jeshi letu la polisi wilaya zote za DSM tunawaomba wafanye kazi zao kwa uadilifu ili kubaini aina zote za uhalifu zinazo endelea ktk jiji hili la dsm.
Operesheni tokomeza uhalifu iendelee
Mpaka akamate yeye hiyo bandari haina ulinzihata ungeambiwa ungesema ni kiki wametengeneza wenyewe. kwani wakat JPM anavamia bandarini anakamata ma container ya makinikia mlisema ni kiki
Kuna kitu chini ya kapeti hii si bureLakiiini, mkuu 'mrangi' kuna kitu bado sikielewi jinsi hili jambo lilivyojitokeza.
Hii ni 'scandal' kubwa saaana, tena inayopiga panapouma kabisa. Wizi mkubwa kabisa.
Sasa fikiria mtu anayesimama na kulizungumzia swala hili ni huyo Binti, Mkuu wa Wilaya, sijui na timu yake ya nini? Ulinzi!
Hivi kuna polisi walijihusisha, au ndio hao wenye bunduki?
Something does not add up!
Siyo kwamba wapo nyuma ni rushwa tu.Hii hamishahamisha ya mapolisi leo huyu ni Rpc Mara kesho kapandishwa mwingine akaletwa tuombe iwe ya kutokomeza huu uhuni na siyo kuuficha.
Angalia video kwanza uone,huyu mwizi wa sasa ana miaka miwili nani alikuwa anatawala? Ungesikia wap habari zake kama vyombo vya habari havipo huru?Kwani Magufuli aliwahi kusema wizi serikalini umeisha?Vita dhidi ya ufisadi ni endelevu. JPM alipambana kwa nafasi yake na alifanikiwa pakubwa. Sote tunakumbuka sakata la Flowmeter ya mafuta na yule mwarabu wa Kigamboni aliyekua katoboa Bomba la Mafuta na kuyachanel kwake. Ni mjinga tuu atakayemlaum Magu katika hili.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama wamebaini nyumba iliyopo mtaa wa Ugindoni iliyotandazwa mashine zinazotumika kuchimba visima vya maji lakini badala ya kuchimba chini kuelekea maji yalipo, wanachimba kuelekea usawa yalipo mabomba ya mafuta yanayotoka baharini kuelekea bandarini.
Mafuta hayo yanachukuliwa baada ya 'flow meter' kusoma na kutambulika yamepokelewa nchini lakini kabla ya kufika kituo cha mwisho ndipo mabomba hayo yanapoelekea.
Ndani ya nyumba hiyo kuna mashine na mipira ambayo inavuta mafuta na kujazwa. Nyumba hiyo ina ulinzi mkubwa na taarifa za awali zinasema muhusika amepangisha eneo hilo lenye kodi ya milioni 60 kwa mwaka huku akiwa amelipa miaka miwili na hakuna shughuli inayoendelea zaidi ya kisima ambacho mabomba yake yanaelekea baharini.
=========
Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana
Sasa kuna wengine mpaka wafike huko “ ungindoni “,itabidi wapimwe COVID-19,wapande ndege Waite UBER ndio wafike huko watafute hao vijana waanze kuwabembeleza wawape mkanda mzima!!.Kama huo mkanda wewe unao huoni ukiutoa hapa utaokoa mambo mengi kwa waja wake muumba nawe ukapata kiji baraka kidogo?.Asante mkuu hyo ishu ya hapo ungindoni ilikuwa inajulikana mda sna mkuu sema nadhan wameharibiana wenyewe wakubwa
DAB anajua mchongo mzma na ndio waliokuwa wakimweka mjin na alilifumbia macho
Ukienda pale ungindon uliza vijana watakupa mkanda mzma
Kwahiyo irudiwe?.Hii scandal ilitakiwa aivumbue PM au mama mwenyewe ... kama vipi PM atembelee eneo
Mara ngapi nilisema humu kuhusu ujambazi wa Kakoko through Jiwe ktk mafuta bandarini ?Kosa lake ni kutuficha kila kitu. Ww ndani ya miaka mi5 uliwahi kusikia wizi? Unafikiri wiz haukuepo?
Flow meter zikifanya kazi vizuri wizi wa jinsi hii hauwezi kutokujulikana. Hivyo kama hizo mita zilikuwa nzuri vigogo wanaoshughulikia mafuta ni sehemu ya tatizo.
Iwapo flow meter ni mbovu - ni kwa nini? Bado vigogo wa mafuta wanahusika tu. Hazitengenezwi au kubadilishwa kwa sababu wanazojua.
Pengine ni bora biashara ya kuingiza na kusambaza mafuta ingekuwa mikononi mwa watu/kampuni binafsi - serikali ichuke kodi.