Kigamboni: Watuhumiwa kutandaza mabomba na kuiba mafuta yanayoenda bandarini

Kigamboni: Watuhumiwa kutandaza mabomba na kuiba mafuta yanayoenda bandarini

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama wamebaini nyumba iliyopo mtaa wa Ugindoni iliyotandazwa mashine zinazotumika kuchimba visima vya maji lakini badala ya kuchimba chini kuelekea maji yalipo, wanachimba kuelekea usawa yalipo mabomba ya mafuta yanayotoka baharini kuelekea bandarini.

Mafuta hayo yanachukuliwa baada ya 'flow meter' kusoma na kutambulika yamepokelewa nchini lakini kabla ya kufika kituo cha mwisho ndipo mabomba hayo yanapoelekea.

Ndani ya nyumba hiyo kuna mashine na mipira ambayo inavuta mafuta na kujazwa. Nyumba hiyo ina ulinzi mkubwa na taarifa za awali zinasema muhusika amepangisha eneo hilo lenye kodi ya milioni 60 kwa mwaka huku akiwa amelipa miaka miwili na hakuna shughuli inayoendelea zaidi ya kisima ambacho mabomba yake yanaelekea baharini.

=========




Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana

Sawa DC kazi nzuri, ila kajifunze namna ya kujieleza vizuri na kuwa na mpangilio mzuri wa maneno
 
Nadhani serikali inatakiwa kufunga mita mwanzoni na mwisho mwa mabomba yake, hiyo itasaidia kujua kama kiasi cha mafuta kinachoingizwa toka kwenye meli ni kilekile kinachotoka kwenda kwenye matank
 
huu wizi ni hatari tupu. yaani hao ni mafia.
unapaswa uchunguzwe na wataalamu walio bobea na waadilifu.

lkn jambo lililo nishangaza iweje yadi kubwa kama ile polisi wafanye ambushi bila kukamata mtu hata mmoja, hata mlinzi hakuwepo!!! kuna watu miongoni mwa si waadilifu, kuna njama za hali ya juu, IGP ingilia kati na utoe maelekezo ya namna ya ku deal na uhalifu wa namna hiii.
 
Kwahio kwenye hio destination walikuwa hawashituki kuona loss ya ujazo wa lita za kutosha kutoka mzigo unaoingia na kupimwa na unaofika kwenye matenki ?
 
Kweli bado tuko nyuma sana au ndio njia za kupumbaza watu

Hapo kabla ya kuingia hapo ilikuwa waweke makachero na kupiga picha za kurekodi mienendo yote na ni nani anaingia na kutoka
Wangefanikisha kumdaka Boss mwenyewe kiulaini ila sasa kufanya hivyo maana yake ni kumwambia Boss kimbia kimeumana

Nionavyo hapa hakuna kitu watakamatwa walinzi na mwenye nyumba tu
Labda wawe na njia zingine za kumuwinda huyo Don
 
Sasa Magufuli anahusikaje hapo. Hao si wezi Kama wezi wengine au kosa lake ni kule kupiga vita wizi kwa maslahi ya taifa. Lazima tukubali alijitahidi kwa uwezo wake ila haizuii ukweli kwamba kuna wachache walikuwepo bado ambao mmoja wapo ni hawa
Hili limefanyika chini ya utawala wake
 
Wewe ni mpumbavu.

Kwani nani alikwambia nami ni fisadi/mhujumu/msaliti wa nchi yake?
Wewe sio fasadi/mhujumu/msaliti wa nchi yako, basi kaa kwa kutulia na utulivu wenzako wakipiga madili mazito kama hayo
 
Punguzeni chuki kwa marehemu.. Mumejazwa chuki dhidi yake kias cha kumchukia kwa kila kosa na makosa ambayo hausiki nayo..

Hapo mwendazake anahusika vipi? Mbona hata kipindi chake alishawahi kukamata watu kama hao na ndio hao mlikuwa mnalaumu kuwa anawabambikia kesi? Ndio haohao leo hii wanafunguliwa A/C zao na mnashangilia??

Lakn naamini Jpm sio bure, iko siku midomo na vidole hivi vinamuandika vibaya siku itafika vitakuja kuandika kulilia uwepo wake na midomo itakuja kutamka umuhimu wa uwepo wake.
Vitakua vidole vya chato labda
 
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama wamebaini nyumba iliyopo mtaa wa Ugindoni iliyotandazwa mashine zinazotumika kuchimba visima vya maji lakini badala ya kuchimba chini kuelekea maji yalipo, wanachimba kuelekea usawa yalipo mabomba ya mafuta yanayotoka baharini kuelekea bandarini.

Mafuta hayo yanachukuliwa baada ya 'flow meter' kusoma na kutambulika yamepokelewa nchini lakini kabla ya kufika kituo cha mwisho ndipo mabomba hayo yanapoelekea.

Ndani ya nyumba hiyo kuna mashine na mipira ambayo inavuta mafuta na kujazwa. Nyumba hiyo ina ulinzi mkubwa na taarifa za awali zinasema muhusika amepangisha eneo hilo lenye kodi ya milioni 60 kwa mwaka huku akiwa amelipa miaka miwili na hakuna shughuli inayoendelea zaidi ya kisima ambacho mabomba yake yanaelekea baharini.

=========




Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana

Hawa wezi ,Basi wakamatwe kwanza mali zao zote zitaifishwe, pili walipe pesa ya lita 60 kila siku KWA miaka miwili na nusu the wapewe cheti Cha wezi bora Tz ,wasifungwe
 
Watu wataacha vipi hiyo michezo wakati wakishikwa adhabu yake ni ndogo tu, halafu tatizo ni kubwa lakini tunalipa attention ndogo sana.

Ulaya nishati ni agenda number moja ya national security; heh yaani we ukiivamia nchi yeyote ya ulaya mahala ambapo utakutana midege imejipanga inakusubiri na kila ya aina ya kombora linakusubiri ni kwenye storage zao za mafuta, vituo vya kuzalisha umeme, pipeline za mafuta na gas. Ukipiga ivyo vitu jeshi aliendi popote, nchi aizalishi chochote, chakula na bidhaa zingine aziendi popote ni umeshinda vita.

Yaani mtu kabisa anaweza fikia pipeline za mafuta Tanzania dah, tena mtu tu wakawaida aisee; nyie watu huo mchezo wa national security narudia tena ni wa vipanga you are not serious.

Mtu tu wa kawaida anawezaje fikia kitu sensitive kama icho kwenye maswala ya national security na ku tamper na miundombinu yake na wala umuoni waziri wa mambo ya ndani hapo au jeshi kuogopa tukio hilo.

Mjomba hilo swala nchi za wenzetu utafanywa mfano mtu mwingine asifikirie tena kujaribu.

Yaani we jua siku Tanzania ikiingia vitani sehemu ya kwanza adui anayoanza nayo ni hayo mafuta ya bandarini na bomba ya Kinyerezi sasa zalisha umeme wako wote sehemu moja uone shughuli yake ya kukutangwa itakavyokuwa rahisi. Utabaki na migari ya jeshi na ndege zisizoweza kwenda popote, narudia tena yaani mtu anachezea bomba la mafuta yanayoingia nchini aisee.
Mimi nimeshangaa pia ili swala limeongozwa na DC bila shaka huu mchezo uko Known, Bongo tuancheza sana aisee juzi kuna pipeline fulani zilikuwa hacked kule US kwenye states fulani, na hio state ika declare state of Emergency, Sisi hatuna attention na nishati soma hata National policy ya nishati utajiona, tunasahau bila nishati hata ulinzi hauwezekaniki
 
Mtandao mkubwa sana, lazima kuna watu walikuwa wanafaudu, kuanzia polisi mpaka TRA, documents za kutembeza lori la mafuta na manunuzi na mapato, utafoji mara 1,1, huwezi kufoji kila siku.

Duuh hii nchi tajiri. Kwerrriiii kweeerrii
Sasa tutakodisha maeneo yetu kweli??

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Mkuu kwa kigambon Kuna mengi sana yanaendelea huko hili mbona ndogo Sana tukisema tumwage mboga hapa wengne kesho tu tutaitwa marehemu kutokana na mfumo wa nchi yetu kutokulinda watoa Siri
Mkuu, tafuta anonymous method ureport izo taarifa huo ndio ulinzi wa taifa letu, trust me wapo waliopewa dhamana na ni watiifu sana
 
Wewe ni mmoja wapo.
Mtakomeshwa, hatuwezi kuendelea kuiona nchi yetu ikichezewa na vilaza kama nyinyi.
Hahaha sawa mkuu kalamu1 baki na akili zako tuache sisi vilaza tuangalie jinsi ya kuishi hapa mjini
 
Aisee

Sasa hii inahusiana vipi na Magufuli?

Hivi ukiwa chadema unakua taahira? Mbona watu wengi wanaomuamini Mbowe ni kama haziwatoshi?

By the way, huwezi kua na akili timamu ukawa mfuasi wa Mbowe na cham chake alichopewa kama zawadi ya birthday na baba mkwe wake.
Magu mwizi yeye ndio kajaza vibaka ndani ya system,dada punguza genye
 
Back
Top Bottom