Kigezo cha Rais bora hakipimwi na wanyonge, Wanyonge hawaelewi chochote kuhusu siasa wala uchumi

Nashukuru kwa kuleta hii mada hapa. Muda mrefu nimekuwa nikiwaza hivyo pia. Kupendwa na wanyonge ni dalili ya kuwa haufai, mbele ya werevu.

Infact hii demokrasia ya kila mtu kupiga kura ndo imetufikisha hapa. "Wanyonge" hawapaswi kupiga kura. Uelewa wao wa mambo ni mdogo mno...wanadanganyika kwa propaganda.
 
Hamueleweki.....

Mliibiwa kura? Ndiyo

Watawala wanapendwa na wanyonge
( mnawaita wajinga wasio na uelewa) ? Ndio

Wanyonge ni wengi kwenye Taifa? Ndio

Asa kura zipi mliibiwa? Kama mnaowaita wajinga ni wengi na ndio ambao huchagua utawala
 
Danganyanane huko mitandaoni lakini tulioko vijijini tunajua jinsi CCM inakubalika. Huku hakuna upinzani. Ni chini ya 30% na kumbuka 70% ya population wako vijijini.
Uje uchaguzi wa kusimamiwa na malaika bado itaongoza vijijini
Kama mnakubalika hivyo wizi ww kura huwa mnafanya wa nini? Ni vijiji gani unaongelea boss, labda vya huko Ukraine sio hivi hivi tunavyotembelea sisi. Kijiji kikishaingia smartphone hakuna uwezekano wa ccm kuendelea kutamba.

Nimekuambia chaguzi 2 tu zinatosha kuiondoa ccm madarakani kwa box la kura, ama kuinyima nguvu ya maamuzi bungeni ambako hupitisha sheria za kuibeba ccm.

Hao unaosema wanaikubali ccm huko vijijini sio kwa ajili ya ushawishi, bali ni kutokana na sababu za kihistoria na hofu wanayojengewa watu wa vijijini.

Huko vijijini tunakoenda tunakuta vijana wamevaa suruali za chini ya makalio na kunyoa viduku, mabinti sket fupi ndio ccm itakubalika? Wadanganye ccm waheshimu box la kura ndio utajua hicho chama zama damu muda wake umeisha.
 
Na bado unaiita ni Demokrasia?
Ambayo itakuruhusu wewe na kikundi chako cha watu wachache kufanya maamuzi kwa ajili ya hao wengi unaowaita wajinga?

mmeshindwa kuwabadilisha watu wafikiri kama nyinyi sasa mnataka kuwaondoa kabisa,
 
So imehalalasha wizi wenu wa kutisha wa awamu yenu pendwa ya kinyonge? Wapuuzi sana walituita wanyonge ili watuibie. Nashukuru Mungu nilipinga kuitwa mnyonge mpaka siku alipotwaliwa aliyekuwa anatuita wanyonge.

Bado ww ni mnyonge Tu, na juzi hapa umepigwa Bilion 7 Kwa ajili ya movie, so Kula Kwa urefu wa kamba yako
 
Kura ziwe na weighting. Uelewa mdogo iwe moja,uelewa mkubwa iwe hata 1000 kwa mtu mmoja
Kwa hiyo Dr. Musukuma (PhD) kura yake haitakiwi kuwa na uzito sawa na ya kibajaji.....
 
Huna akili timamu.

KANU ni jina tu kama ilivyo JUBILEE na ODM, Leo Kuna Azimio na UDA lakini watu Ni WALE WALE

Hata ccm ikitoka madarakani unadhani watakuja wachina kukaa madarakani, watakaa hawahawa watanzania, lakini hii laana iitwayo ccm itaondoka na mambo mengi yatabadilika.
 
Bado ww ni mnyonge Tu, na juzi hapa umepigwa Bilion 7 Kwa ajili ya movie, so Kula Kwa urefu wa kamba yako
Bora tumepigwa na tumeambiwa. Kuna huyo mwendazake alikuwa mstari wa mbele kwenye madhabahu nakusema hakuna wizi ila aliiba mpaka hela ya chumvi ya mboga. Unatuita wanyonge halafu unatuibia? Bora utuite matajiri halafu utupore tutafarijika matajiri tumeporwa.
 
Nchi hii kura haziamui nani awe Rais, kamuulize Lowassa

Hata huyo mkombozi wenu mnaemsifia sana hakuamini kwenye kura ndio maana alifanya uhuni zaidi kwenye uchaguzi kuliko rais yoyote
 
Kwahiyo kitu pekee kizuri kutoka kwa Hao watu wa daraja la chini ni kura zao tu ?! Au !! Maana umesema hawajui chochote kuhusu masuala ya uchumi etcetera , of course hata huko wanapojinasibu nchi zimeendelea watu wengi huwa wanaangalia zile basic needs za kila siku wanamudu kuzipata ?? Kulingana na kipato chao ?? Kama wanashindwa kumudu lazima utasikia kelele nyingi !!
 
Ogopa sana hilo tabaka.

Siku wakichoka hapatakalika na utatamani uombe nafasi ya kutubu lakini haitakuwepo.

Ni hatari sana kuendelea kumkandamiza maskini kwa muda mrefu bila kumpa pumzi.
Hamna anaye justify wanyonge kukandamizwa, ila kutumia wanyonge kama kipimo cha rais bora ni yupi ni misleading
 
Tanzania kila mtu Ni MWIZI.

Hata ukimpa fundi kazi ya UJENZI wewe tegemea kuibiwa SIMENTI, MBAO na MABATI
Wamezaliwa ni wezi kama ukoo wa panya ? Au wamefundishwa kuwa wezi ?? Na je kama hali ndio imekuwa hivyo tuendelee kuwa hivyo hivyo ??!
 
Hata ccm ikitoka madarakani unadhani watakuja wachina kukaa madarakani, watakaa hawahawa watanzania, lakini hii laana iitwayo ccm itaondoka na mambo mengi yatabadilika.
Litaondoka jina tu CCM.

Watu watakuwa wale wale.

Lowassa wa CCM ndiyo yule yule wa CHADEMA.

Wewe ni MFUASI UPEPO.

Bible inasema inasema palipo na mzoga ndipo watakapo kusanyikia TAI.

Hata Leo ikiingia madarakani CHAUMA watu wengi kutoka vyama vingine hata CCM watahamia huko huko kwenye ulaji na wewe Happ HUNA CHA KUFANYA.

Kwani Mara ngapi wagombea wanakatwa CCM wanahamia vyama vingine.

Tumia Akili, punguza matarajio yasiyokuwepo. Punguza kutumika.
 
Sijasema mahitaji ama shida za wanyonge zipuuzwe
Ninachosema popularity ya Rais kwa hao wanyonge sio kigezo sahihi cha kupima ubora wa Rais
 
Yaani haya mambo yanapasua kichwa !! Ni sawa na kusema baniani mbaya lakini kiatu chake dawa !!
 

Hoja yako ni ipi hapa dogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…