Kigezo cha Rais bora hakipimwi na wanyonge, Wanyonge hawaelewi chochote kuhusu siasa wala uchumi

Ndio hao hao walikuwa wanawalaghai awamu iliyopita kwa kuwafanyia maigizo ya kula mahindi kwenye misafara ya Rais na eti kununua/ kupeana jogoo kutoka kwa wanyonge 😂😂😂..

Wenzao wanapiga pesa wao wanaambulia drama za kuitwa wanyonge,na wasivyo na akili wanashangilia 😬😬
 
Hoja yako ni ipi hapa dogo?
Hoja yangu Ni kwamba unachotaka kukipata Ni kitu kisichokiwepo, utahangaika mpaka kufa.

Hapo Kenya wana Tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya lakini mpaka Leo bado wanalilia Mabadiliko.

Sasa hivi, wanasiasa wanachofanya Ni kutengeneza magenge ya msimu wanayo yaita vyama kutafutia madaraka lakini watu Ni wale wale.
 
Labda kweli hawana wanachoelewa hawana maana yoyote lakini kura zao zina maana sana.
Ndio wanaoamua nani awe Raisi wa nchi.. nani awe Mbunge au Diwani...
Zina maana ndio ila kumbuka ukiwa na Taifa lililojaa hao watu huwezi pata maendeleo ya maana kwa sababu hao watu watawachagua wanasiasa waongo na walaghai wasiowaambia ukweli..

Ila ukiwa straight kama Samia wanakuchukia na huwezi pata kura.

Hao mburula hata mwalimu aliwapuuza kwenye kura ya Maoni Kuhusu vyama vingi.
 
Geita sio Chato, na kwenda huko haimaanishi kuwa ni route yenye faida.
Hakuna kitu kinaitwa Chatto (International Airport) ila Geita Airport na IATA Code yake ni GIT. Unajikuta mjuaji kumbe haujui chochote. 🚮
 
Ni wananchi wajinga wasiohoji lolote. Hao ndio waliambiwa uwanja wa ndege wa Chato unajengwa Tanzania, leo hii ATCL imesema haitapeleka ndege huko maana ni hasara, wako kimya hawajui hasara waliyoipata kwa kodi zao kutumika vibaya.
Ukisema uongo hakikisha unajua pia na ukweli wake😂😂😂. Natumia sana uwanja wa Chato na nimekuja Dar jumamosi narudi jumanne. Sijaona kufutwa kwa safari za ATCL kwenda Chato
 
Mataifa makubwa yana amani kwa sababu the national cake is shared equally, na hiyo inawezesha kiongozi yeyote kuja na kuongoza bila matatizo. Hizo fikra zako kama ndiyo mawazo ya na serikali ya awamu ya 6 mmeshapoteza uhalali wa kutawala.
 
Mataifa makubwa yana amani kwa sababu the national cake is shared equally, na hiyo inawezesha kiongozi yeyote kuja na kuongoza bila matatizo. Hizo fikra zako kama ndiyo mawazo ya na serikali ya awamu ya 6 mmeshapoteza uhalali wa kutawala.
Nafikiri hujaielewa .

Point sio kuwa wanyonge wakandamizwe, lakini ubora wa Rais haupimwi kwa kuwafurahisha wanyonge

Mfano akitokea Rais akasema wananchi wanaruhusiwa kuvamia hifadhi na misitu, wanyonge watafurahi sana, je huyo atakuwa rais bora?
 
Unaonaje tuweke sheria ili uweze kupiga kura uwe na degree umri kati ya 25 na 60 na kipato kianze 5000usd hapo tutaweza kuchagua viongozi bora
 
Unaonaje tuweke sheria ili uweze kupiga kura uwe na degree umri kati ya 25 na 60 na kipato kianze 5000usd hapo tutaweza kuchagua viongozi bora
Ni wazo zuri ila Tusifike huko,jambo la muhimu kwanza ni Katiba Bora bila shaka itapunguza role ya wajinga kwenye kufanya maamuzi ambayo mwisho wa siku inakuwa ni costful sio tuu kwao bali kwa Nchi..
 
Naam Naam, kweli asilimia mia mia moja, laiti ukweli huu ungekita kwenye vichwa vya watanzania
 
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, nadhani umeachia kiburi cha elimu ulichonacho kikutawale maishani mwako. That is wrong of you.
 
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, nadhani umeachia kiburi cha elimu ulichonacho kikutawale maishani mwako. That is wrong of you.
Hivi mkuu hao watawala wa zamani walikuwa wakichaguliwa na wanyonge?
Zilikuwa ni tawala za kiukoo na mabwanyenye na zilikubakika kwa Mungu

Point hapa sio kukandamiza wanyonge, ila kuna mambo mengine sio popular ila yana faida kwa muda mrefu na hapo huihitaji maoni ya wanyonge kuyatekeleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…