Bukwabi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 3,352
- 1,148
Magufuli Kiboko Kigogo Akamatwa Kwa Tuhuma za Kuhusika na Unga
DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara maarufu jijini Dar ‘kigogo’, Daudi Yakubu Kanyau (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Makao Makuu Ufundi, Kilwa Road, Dar akihusishwa kwa namna moja au nyingine na biashara ya madawa hayo maarufu kwa jina la ‘unga’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mfanyabiashara huyo alikuwa akitafutwa na dola kwa kufuatilia nyendo zake siku nyingi baada ya kuwemo kwenye orodha ya watu wanaosadikiwa kuijua kiundani biashara
TAARIFA NDANI YA JESHI LA POLISI
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa Kanyau alikamatwa nyumbani kwake, Salasala jijini Dar wiki moja iliyopita kwa ushirikiano wa kikosi cha madawa ya kulevya na kikosi cha kupambana na utakatishaji fedha haramu (money laundering) ambao wao huchunguza utajiri wa mtu na uhalali wa kipato.
MALI ZAKE ZASHIKILIWA
Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi hilo zinadai kuwa polisi wanashikilia mali za Daudi kwa ajili ya uchunguzi wa namna alivyozipata pia kuchunguza misaada mbalimbali aliyokuwa akiitoa kwa jamii, kama vile kujenga nyumba za familia, ibada na mingine.
KWA NINI?
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutangaza vita dhidi ya wauzaji na watumiaji wa unga na kuagizwa kukamatwa mara moja.
DCI ANENA
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania, Diwani Athumani hivi karibuni aliliambia gazeti hili kuwa msako mkali umeanzishwa na watu wengi wamekamatwa, wakiwemo vigogo lakini hakuwa tayari kutaja majina yao hadharani kwa madai kwamba upelelezi bado unaendelea.