Mkuu..
Majirani na hapo kwa mama mkwe wa Kanyau wameshakwenda sana Polisi wakaja kujua kumbe polisi wana mgao wao.
Wakaja wakaenda serikali za mitaa.. Kama unavyojua serikali za mitaa zetu, wakaishia kutofanya kitu.
Lakini alipoingia Kitwanga kama Waziri wa Mambo ya Ndani kuna majirani navyosikia walijilipua wakampelekea taarifa maana pamekuwa kero kubwa kwa mtaa.
Mateja mamia kwa mamia wanajazana hapo kwa mama SEDI kila siku.
Nimesikia sikia kwamba CHALE ambae ndie muuzaji mkuu hapo kwa mama yake yupo ndani.