Kigogo wa NRM Agro Limited na wenzie 10; Mahakamani kwa makosa ya dawa za kulevya

Kigogo wa NRM Agro Limited na wenzie 10; Mahakamani kwa makosa ya dawa za kulevya

Kwahiyo kuuza mbolea ni biashara ya kuzugia
Inaelekea kwenye uingizaji wa mbolea,huwa anachomekea mizigo....pia
Hawa watakuwa wamechomana..
Maana mzigo kama huo ukifika ICD lazima waje watu wa security ukaguzi,kontena linafunguliwa seal ...watu wanachkua chao seal inarudushiwa maisha yanaendelea

Ova
 
NRM Agro Limited na wenzake wanadaiwa kuingiza shehena ya madawa ya kulevya aina ya Mitragyna Specioza uzito wa kilo 11, 596

TOKA MAKTABA :
10 Julai 2025
Bandari Kavu
Temeke
Dar es Salaam, Tanzania

Kamishna Mkuu wa DCEA aongelea mzigo huu ktk kontena mubashara ulioandikishwa kama mbolea

View: https://m.youtube.com/watch?v=yIkmplFKN2M
lakini kubainika ni madawa ya kulevya aina ya Mitragyna Specioza uzito wa kilo 11, 596 bandari kavu Sokota Temeke jijini Dar es Salaam

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata shehena ya dawa mpya ya kulevya aina ya mitragyna speciosa mifuko 756 yenye uzito wa jumla ya kilogramu 18,485.6 sawa na tani 18.5 iliyokuwa ikiingizwa nchini kama mbolea.

Hayo yamesemwa leo Agosti 13,2025 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema kuwa, katika tukio hilo watuhumiwa saba (7) wamekamatwa, wakiwemo raia wawili wa nchi ya Sri - Lanka ambao ni Jagath Prasanna Madduma Wellalage (46) na Santhush Ruminda Hewage (25).

Amesema watanzania waliokamatwa ni Riziki Abdallah Shawej (40), Andrew Athanas Nyembe (34), Mariam Shaban Mgatila (40), Ramadhan Sanze Said (57) na Godwin Melchory Maffikiri (40).
 
Billnas huyo
Jamaa fala kweli kwenye nyimbo yake mpya hii kuna mistari anajisifia kabisa ku supply nilisikia hadi nikawaza huyu bwege anajiamini vp, hata dogo hamidu ngoma yake moja anasema.. wanao sniff na ku snore me ndo nawa control, pesa hua inampa mtu kiburi cha kijinga wanajisahau kabisa au labda wanafkiri wametumia tafsida watu hatuwezi elewa.
 
Wakamatwe tu!
 
Back
Top Bottom