Kigogo2014 lazima awe mtu wa maana

Kigogo2014 lazima awe mtu wa maana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KIGOGO HUWEZA KUWA MTU YEYOTE WA MAANA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Leo katika pitapita zangu mtandaoni niliona Tangazo linalotoa fursa kwa yeyote atakayewezesha kupatikana kwa mtu ajiitaye Kigogo2014 au Kigogo Kigogo basi angepatiwa donge nono. Kufikia hapo macho yakanitoka, si unajua tena vijana hatuna ajira. Lakini nikaingizwa na mashaka kuhusu ukweli wa tangazo lile, maana siku hizi habari bandia ni nyingi kuliko habari halisi. Hata hivyo sikupata uhakika wa ukweli wa tangazo lile. Kuhusiana na huyu mtu Kigogo Kigogo sio mtu niliyekuwa namfuatilia sana tangu nimeanza kusikia jina lake miaka kadhaa iliyopita. Lakini mwaka huu 2021 mwezi wa kwanza mwishoni ndio kidogo nilianza kumzingatia na kumuona ni mtu asiye wa kawaida. Hata hivyo nilishawahi kuandika makala moja mwaka jana hapa Facebook ya kumuonya kwa baadhi ya lugha anazotumia.

Kigogo2014 kama nikiambiwa nichore picha yake, basi ningechora picha ya mwanaume mwenye umri wa makamo kati ya 42 - 49, mrefu wa futi tano na nusu, maji ya kunde, mwenye kunyoa kipara, mwenye ndevu za wastani. Kwa habari ya kuongea basi anaonekana ni mtu mwenye kuongea kwa taratibu, tofauti na jinsi inavyoonekana akiandika kwa kufoka au machepele. Sauti yake sio nzito wala sio nyepesi.

Kwa mujibu wa jinsi anavyoandika, hapana shaka Kigogo ni mwanaume mwenye elimu ya juu ya Masters. Kigogo kwa uandishi wake pia inaonyesha ni mtu ambaye anaexposure na dunia ilipotoka, ilipo na inapokwenda. Kigogo kwa uandishi wake, anaonekana ni mtu aliyesafiri nchi zaidi ya mbili, na ameshawahi kwenda nchi za ulimwengu wa kwanza. Kwa uandishi wake, Kigogo anaonekana ni mtu aliyewahi kufanya kazi kwenye vitengo nyeti vya serikali, ila kwa sasa hayupo serikalini.

Kwa tones anayoandika Kigogo, inaonekana kuna pesa anaidai serikali, aidha aliziiba zikataifishwa na serikali au hajaziiba lakini kuna namna serikali anaiona inadeni lake hivyo anataka stahiki zake. Kisaikolojia, Kigogo anaonyesha ni mtu aliyetulia, na anayejua kucheza na akili za mahasimu wake na watu wanaomshabikia na kumfuatilia. Anajua nini aseme wapi kwa muda gani. Pia Kigogo hutumia mbinu ya kutumia matusi ili kumkasirisha hasimu wake kwani kwa kufanya hivi huwafanya wale anaowatukana kukosa utulivu katika kumsaka. Kiteknolojia, Kigogo anaonyesha ni mtu anayejua masuala ya Tehama.

Hivyo ili umpate basi yakubidi uwe na teknolojia kama yeye au zaidi yake jambo ambalo mpaka sasa inaonekana wengi hawajamfikia. Kiimani, Kigogo anaonekana ni Mkristo wa madhehebu yanayoabudu siku ya jumapili. Kisiasa na kianaharakati, Kigogo ni mwanachama wa CCM na kama ameacha chama basi ni siku za hivi karibuni, Kigogo hajawahi kuwa mpinzani na hatakuja kuwa mpinzani. Kigogo sio mwanaharakati halisi au wakweli kwani mambo anayoyafanya ni kwa maslahi yake binafsi sio maslahi ya taifa au jamii. Ni kwamba kuna sehemu maslahi yake yamebanwa sasa anahasira na serikali. Kwa umri wa kigogo kama nilivyokisia kuwa atakuwa ana range 41 - 49 kama angekuwa mwanaharakati wa kweli, basi angeanza harakati zake tangu utawala wa Kikwete.

Kiusalama na Kiintelejensia, Kigogo anaonekana alishawahi kula mafunzo ya kijeshi au ya kiintelejensia, na kama sio hivyo basi yupo karibu na watu hao lakini watu hao wanafanana kitabia, kimaslahi na jinsi walivyoathiriwa.

Hati na maandishi, kwa jinsi hati na maandishi ya kigogo kwenye post zake, ni wazi muandishi ni mmoja, na kama wapo wawili basi wanafanana muandiko, lakini kuhusu mshikamano wa sentensi na aya, kuna utata kwani inaleta matokeo ya watu wawili tofauti lakini hati ni ile ile. Zipo posti zinazoonekana zimepostiwa na kijana wa umri kati ya 30 - 40, posti hizi zinakuwa ndefu na maelezo yenye aya tatu mpaka nne. Lakini posti zenye sentensi moja au mbili zinaonyesha zimeandikwa na mtu mwenye umri kati ya 41 - 49. Kwa mujibu wa maandishi, Kigogo inaonekana ni kijana wa mjini(Born town), na kama ni wakuja basi alikuja mjini miaka ya 90. Kinaponipa wasiwasi zaidi ni hata hati ya Tangazo inafanana kwa ukaribu zaidi na hati ya maandiko ya huyo Kigogo2014. Sijajua nani anaongoza hiyo page iliyotoa tangazo la donge nono.

Sauti ya Kigogo inaonekana ni Ile ya Kati ndogo ndogo yenye ukali kidogo.

Kwa jinsi anavyoandika, Kigogo inaonekana hayupo Tanzania, yupo nchi za nje. Jina lake, kama nikifikiria habari la jina la Kigogo, kwa nini ajiite hivyo, basi naweza kuwa na majibu yafuatayo;
1. Mtu hujiita jina kwa vile alivyo
2. Mtu hujiita jina kulingana na tamaa ya vile anavyotaka awe baadaye
3. Mtu hujiita jina kwa kuitwa na watu wengine kama wazazi, ndugu, rafiki na jamaa.
Sababu ya kwanza na ya pili ndio inanguvu kwa muktadha wa Kigogo. Lakini sababu ya kwanza ndio jibu halisi kwani kwa kiwango na mienendo ya Kigogo Kigogo ni wazi hawezi jiita jina hilo kwa matamanio kuwa siku zijazo atakuwa kigogo bali amejiita hivyo kwa kuwa tayari yeye ni kigogo.

Hivyo Taikon kwa muono wangu kupitia jina alilojiita, naweza sema hivi;
1. Kigogo anaweza kuwa miongoni mwa vigogo wakubwa waliohudumu katika nafasi za uongozi hapa nchini
2. Kigogo anaweza kuwa mtoto wa Kigogo ambaye haishi hapa Tanzania lakini anapewa taarifa na Baba yake aliyepo ndani ya nchi yetu. Huyo Baba yake huenda ni mstaafu au amegombana na serikali somewhere sasa anamtumia mtoto wake kuiadhibu serikali. Bila shaka huyo mtoto lazima awe vizuri kwenye masuala ya Tehama.
3. Kigogo inaweza kuwa kikundi fulani cha vigogo au watoto wa vigogo ndani ya serikali wenye nafasi nyeti waliotengwa na serikali. Kiufupi Kigogo lazima awe mtu wa maana, hawezi kuwa mtu wa hivi hivi. Nachelea kusema Kigogo Kigogo Hawezi kuwa hawa vijana wa upinzani au wanaharakati wa kawaida, labda hawa vijana kazi yao iwe kumuunga mkono huyo Kigogo.

KUMFUATILIA KIGOGO
Ni ngumu sana kumfuatilia kigogo kwani yeye sio mtu Back, isipokuwa inaonekana yupo kwenye system nyeti, hivyo hata wanaomtafuta isikute naye yumo humo humo, namaanisha informer wake, na hawa kitabia lazima wawe ni watu wanaojifanya wao ndio wanahasira na huyo huyo Kigogo kuwapumbaza wenye nia ya kweli. Mbinu rahisi ya kumkamata Kigogo ni kujifanya kama mmeachana naye wala hamshughuliki naye kumbe mnamlia timing. Pasiwe na kikao chochote kumjadili huyo kigogo kwani uwepo wa kikao ni kumualika Kigogo mwenyewe. Kuweka vikao ni kutengeza mazingira ya kumpa ushindi Kigogo na genge lake. Kisha kuwafitinisha ninyi kwa ninyi ilhali hamumjui adui yupo kona ipi. Ushauri wangu kwa Kigogo; Acha kutumia Lugha ya matusi isiyo ya staha na adabu. Nimesikitika sana ulivyokuwa unaudhalilisha msiba wa taifa na kutukana bila aibu. Kwa kweli mimi sijapendezwa na lazima nikukemee kwa tabia ile, najua wewe unaakili ya uovu na kujificha lakini hautaweza kujificha siku zote. Hivyo nakushauri uiombe familia ya Hayatti Magufuli msamaha kwa maneno ya aibu uliyoyatoa kipindi cha msiba. Nafahamu unahaki ya kumsema aliyekuwa Rais, Hayatti Magufuli lakini sio kwa maneno makali vile, ulipaswa kumkosoa na kumsema kwa lugha ya hekima lakini sio ule upumbavu wako. Kwa hili na wewe utagharamika, pengine ulikuwa na haki lakini umeipoteza haki yako kwa kuzidisha mdomo.

PONGEZI ZANGU KWA KIGOGO
Mbali na kukuonya, kukukemea na kukuonya, lakini nikupongeze kwa uwezo uliokuwa nao wa kuweza kujificha mbele ya mkono mrefu wa serikali. Kusema ukweli unaipa changamoto serikali na kuonyesha madhaifu ya serikali, hivyo serikali ijitathmini kuhusiana na ni vipi unaweza kufanya hayo uyafanyao na serikali ishindwe kukukamata. Serikali ichukue jambo hili kama changamoto. Pili, nikupongeze kwa ujasiri wa kufanya hayo pasipo kuogopa hatma yako. Kwa kweli ni watu wachache mfano wako
WITO:
Achana na masuala ya kutukana watu, kosoa ikiwa kuna haja lakini rekebisha lugha yako

WITO WANGU KWA SERIKALI,
Zingatieni mazuri awapayo Kigogo Kigogo kama vile asemavyo suala la haki na uhuru, lakini mumtafute huyu mtu ili mumuonyeshe kuwa ninyi ni watu wema, na kwa kudhihirisha jambo hili, mkimkamata msimfanye chochote. Na wale wote aliowatukana watoke hadharani waseme wamemsamehe.

Ulikuwa nami:
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Njombe
 
Wale wahuni wa FB wa sku mbili tatu hao ndo wameeleweka concept zao kuhusu Kigogo , unadai anadai pesa ?? Noo , yeye mwenyewe anadai jiwe ametumia zaidi ya 4.6 billion kumpata na kumshawishi lakni wapi...inavyoonekana ni kikundi ndani ya CCM chenye interest zao na kilikuwa bittery against JPM....anyway still bado Kigogo haelewek ye ni nani😀😋 Ni ghost mi sjui 😋😋 asije akayafunua mafaili yangu

Kama yupo juu hawezi funua mafaili ya mtu wa chini

Na kama upo chini huwezi funua faili la mtu aliyejuu. Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba mzee.

Habari zako azipate wapi?
 
Kumkamata kigogo tunatumia ile njia njia aliyotumia the Imp kipindi anataka kumuozesha mtoto wa cersei lannister movie got au iliyotumika na jaro kwenye kumkamata snitch wa crew movie inaitwa pod pikrite

Nataka nijifunze kitu mkuu
 
'Niliwahi kuandika hapa facebook'

This means mleta uzi kacopy ishu yake ya fb na kuipaste hapa bila proof reading. Also nakupa ujanja ili huko fb uzidi kuwateka.

Mfano unasema anaonekana anaidai serikali basi unainsert screenshots zinazoonyesha hivyo. Na sehemu unazoamini zinahitaji picha unaingizia.

Katika uwasilishaji makala, makala yenye picha inavutia kuliko ambayo ni mwendo wa neno kwa neno mpaka mwisho.

Anyway, uzito wa mdundo wa indi amka na denzi za Sancho,

Ni sawa na ubishi wa goli kutoka kwa mbishi pancho,

Mashughuli toka utoto toka time ya msoto, toka studio joto sahau kuhusu AC...
 
Back
Top Bottom