Kigoma JF users connect

Kigoma JF users connect

Jua huku unakuja kukutana na watu wabishi kuliko wote Tz nzima so usishangae .
December ntatia timu huko na machalii nije nihamie kabisaaa....nijiandaeje kisaikolojia labda mkuu kabla cjaja??
 
kigoma nimekaa enzi za aifola mwenda salama kule beach nyuma ya hospital ya mkoa Maweni na Mbunge wetu Aman Waldi Kabourou,,

enzi Haice zinaitwa hiyasi na umeme niwamgao generator kule Magereza,Nimekaa kigoma

enzi bwawa la katubuka tunavua samaki na kitimoto tunanunua kilo moja sh 400 kwa jamaa mmoja anaitwa sokolo pale katubuka ,

enzi hizo story kubwa ni za Bunjumbura na zaire ,

Enzi hizo nyimbo za kizairwa kama yondo sista shimita aalus mabele na kanda bongo man ndio habari ya mjini.

Enzi samaki huwezi kuuziwa kwa kilo ila kwa mafungu samaki watano sh 200 na nyongeza,

Kigoma ninayoijua mimi ni ile mitaa ya kilimahewa na mjimwema ni ya kishua sana hukatizi ovyo mbwa wakali kila kona.

kigoma ile ya Cine atras na Bahama Ujiji tunaenda kucheck video unatoa sh 20 unaangalia movie mbili ya Kihindi na ya kizungu plus trailor la mziki wa Wenge BDBG

kigoma Ni noma Bana napamiss sana nasikia saizi kumekua kama dar es salaam vurugu nyingi
Enzi hizo kujirusha ilikuwa ni kwa azim premji magorofani ,kwa wale wazee Wa wanzuki na kayoka wanakutana pale "mgatutu"
 
ok mimi siikumbuki kigoma ya magorofa naikumbuka kigoma ile pale stand ya community center ni sehemu tunacheck video na mikutano ya siasa na ya kidini na uwanja wa mpira.
[emoji4] [emoji4] we kama Mimi zile enzi hata ule mwembe toga haujakatwa bado

Enzi zile za mashineni kwa "bidyanguze". Pale sokoni mwanga
 
Back
Top Bottom