lunatoc
JF-Expert Member
- Aug 16, 2017
- 2,911
- 5,479
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe akili yako ina dosari sehemu fulani.Zito Kabwe yuko kimya hasemi chochote kwa sababu analamba asali ya mama
Huu ni zaidi ya unyama, hawa washenzi wakipatikana wachukuliwe hatua kali.Watu sita wa familia moja wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili na Watu wasiojulikana katika Kijiji cha Kiganza wilayani Kigoma Mkoani Kigoma.
Familia hiyo ya Mussa Cheche kwa sasa waliobaki hai ni Mtoto mwenye umri wa miaka 4 ambaye amejuruhiwa na Mtoto mwingine mdogo wa miezi minne ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Kigoma Menrad Sindano amesema chanzo bado hakijafahamika.
Kamanda Sindano amesema “Hawa Watu wote wameuawa wakiwa wamelala kwenye vitanda vyao si mauaji ya Mtu mmoja au wawili na kuna vyumba vitatu na miili hiyo imekutwa kwenye vyumba hivyo, na inaonekana wauaji ni zaidi ya Mtu mmoja, uchunguzi bado unaendelea, msako mkali unafanyika kuhakikisha wale wote waliohusika na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria”
Chanzo: Millard Ayo
Akisema wauwaji watajisalimisha??Zito Kabwe yuko kimya hasemi chochote kwa sababu analamba asali ya mama
Zito ni mbunge?
Wanawake wa siku hizi hatari, ila mpaka mwanamke anachepuka ujue kuna shida ndani. Kuna ndoa nyingine ni manyanyaso jamani, mwanaume hatulii ndani, kazaa nje, vipigo ndani na matumizi ndio hivo hivo tu maana kashikiliwa huko mpaka kasahau mke na watoto. Sasa kupunguza stress mwanamke anajikuta kaangukia pabaya, hapo mume ndio atafanya yake. Kuna wanaoangukia kanisani yaani hao ni balaa pia maana anasema anaenda kusali kumbe anagongwa na wachungaji haya maisha haya mhmimi tatizo likitokea huwa naangalia chanzo.
Mume kaua mchepuko wa mkewe, amefanya unyama mbaya sana.
ila tuseme ukweli Dada zetu na Mama zetu wengi walioolewa ni wachafu sana siku hizi. Wanaume wengi hawana raha tena na ndoa zao. wanawake kuchepuka imekuwa fashion na sifa. hizi simu kubwa zina malimbukeni wengi wanawake.
Jamii iwafunde kinadada na kinamama watulie kwenye ndoa zao.
Aliyeua ni Mtanzania mwenye wivu imeshabainika.kigoma ni miongoni mwa Mikoa ambayo inamatukio ya Kijambazi/kihalifu, na hiyo inachangiwa zaidi na mwingiliano kati ya warundi na wakongo.
Ni Mkoa unao ongoza kuwa na wahamiaji haramu wengi ambao wanaishi kiholela bila kuwa na vibali, kuna warundi na wakongo wengi ambao wamefanya uhalifu ktk nchi zao na kukimbilia Kigoma, hivyo usalama wa wananchi wa Kigoma kuwa mashakani.
Vyombo vya ulinzi na usalama havina budi kufanya operesheni ya kusfisha kabisa wahamiaji haramu ktk Mkoa huo ambao wamekuwa tishio kwa usalama wa raia na mali zao.
sawa, lakini bado Mkoa wa Kigoma una changamoto za wahamiaji haramu wanao ishi kiholela kitu ambacho ni tishio la usalama wa Mkoa wa kigoma na Tanzania kwa ujumla.Aliyeua ni Mtanzania mwenye wivu imeshabainika.