Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga

Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga

Ushauri wako ni Mzuri lakini ninacho shangaa Serikali Ya Tanzania kwa nini inaogopa Huo Uraia Pacha? Ungekuwa Uraia Pacha una madhara jirani zetu Wa-Kenya wasingekubali kuruhusu huo Uraia Pacha Bado sisi Wa-Tanzania tuko nyuma kila kitu ingelifaa tuige wenzetu majirani zetu Wa-Kenya walioruhusu Uraia Pacha.
Ungeainisha hayo madhara ya iraia pacha hoja yako igekuwa na uzito mkubwa, wengi tungeelimika
 
CCM inaogopa wenye exposure toka Kulikotakata wanaweza wakapata nafasi za Kisiasa na kuwazindua Wadanganyika waliolala, hiyo ndio hofu kuu waliyonayo. Mifano ni harakati za Wahindi wa Canada na serikali ya Waziri Mkuu wa India na sehemu nyingi duniani. Chama chakavu wanapenda kuabudiwa na Kondoo Wadanganyika. Mama mitano tena
 
Kwani kama tukiwapa hadhi maalum wale raia wa Tanzania waliochukua uraia wa nje kuna shida gani? Kwamba wanaweza kurudi nyumbani bila kuhitaji visa,wataruhusiwa kumiliki ardhi,wataruhusiwa kufungua makampuni kama wazawa n.k
Lakini wasiruhusiwe kugombea vyeo vya kisiasa,kupiga kura n.k,sasa huko kung'ang'ana na uraia pacha kunatoka wapi au mnaosukuma hoja hiyo mna agenda yenu ya siri? Hivi leo ukiruhusu uraia pacha kwamba Mnyarwanda,Mcongo,Msomali,na kote huko kwenye migogoro inayotokana na sababu mbalimbali nchi yetu itakuwaje? Tuache unafiki serikali imeanza kuandaa sheria ya kuwapa hadhi maalum Watanzania hao waliochukua uraia wa nchi nyingine kwa sababu mbalimbali.
 
Kwani hao diaspora wakitumia hela zao na kufanya maendeleo huko waliko watapungukiwa nini? Kwanini wanataka sana kuwekeza Tanzania ila hawataki kuwa watanzania by 100%? Ninaishauri serikali izidi kukataa huu upumbavu wa uraia pacha. Wanaoutaka wana tamaa na utajiri wa nchi ya Tanzania na sio kwamba wana uzalendo wowote. Hao Kenya, DRC, Zambia hawana lolote walilotuzidi pamoja na kuruhusu uraia pacha.
 
Nyie UWT sijui kama mtapata akili hata siku moja
 
Wawape tu uraia pachą kwanza itasaidia Tanzania kupata remittance, upande wa diaspora zaidi psychological (belonging).

Hizo nyumba wanazojenga nyie jipangeni akifa nani mrithi, 90% yao wanazikwa huko huko walipo.

Watu wana watoto wakubwa na wajukuu wengi wao Tanzania hawaijui kabisa ndio waje wazike wazazi wao Tanzania.

Kwetu tushazika dada yangu wa kwanza ulaya, alijenga nyumba yake mwenyewe mumewe alirudi sasa hivi anaishi na mke mpya. Maamuzi ya kuzika ulaya ilikuwa ni baada ya kikao cha familia, bado wengine wamekazana kujenga mijumba na wana wajukuu tayari ulaya. Wazimu mtupu.

Tushazika binamu yangu, badala ya kuletwa Tanzania wazazi wake ndio wamepanda ndege kuja mzika.

Huu mji ninaoishi kwenye siku 30 tushazika watu wazima wawili, watoto na wajukuu wametaka hivyo.

Toka nimeamia huu mji tushazika watu kama saba kijana mmoja wakihaya japo hakuwa na watoto ila ndugu zake wakasema azikwe huku. Mwingine mumewe japo anapiga trip za Africa sana kutokana na watoto akaamua mkewe azikwe huku.

Dual citizenship kwa diaspora ni psychological issue tu ya belonging bado wana mapenzi ya moyoni na Tanzania. Lakini uhalisia ina faida kwa ndugu na jamaa kwenye mirathi kuliko diaspora wenyewe. Wawape tu huo uraia pachą wajenge hizo nyumba na kuweka vitega uchumi kwa faida za ndugu zao wakifa.
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo 20/11/2024.
Pascal, nimesema mara nyingi sana humu JF, kwamba wanaopinga uraia pacha wana hizi sifa kubwa
  • hawajui maana halisi ya uraia pacha
  • hawaajui ni jinsi gani mtu anaweza ku-qualify kuwa raia pacha wakidhani mtu yeyeote wa nje anaweza kuchukua uraia pacha wa Tanzania
  • hawana nafasi ya wao wenyewe kuwa raia pacha hivyo wana silka ya ubinafsi (selfishness) ya "kama sipati mimi basi wote tukose"
  • wivu unawasukuma kuwazibia wengine kwa sababu hawapendi kuona watu wengine wamefanikiwa
  • wanawaogopa diaspora kuja nchini na mawazo mbadala ambayo yanaweza kuleta vuguvugu jipya la uongozi nchini (kama ambavyo askari wa Afrika walipoenda kupigana nje vita ya WW2, walirudi na mawazo ya kudai uhuru Afrika)
Na nimesema wazi, Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa na wazo la uraia pacha. Karibu 75% ya nchi za Afrika zinaruhusu uraia pacha. Na nimekuwa nikiwauliza wanapinga uraia pacha kwa Tanzania, ni hasara gani nchi zenye kuruhusu uraia pacha zimepata hadi sasa? Nchi kama Rwanda, Mauritius, Kenya, Burundi, Misri, South Africa, Burkina Faso, Cape Verde, Ghana, Guinea Bissau, Uganda, Mali, Niger, Nigeria nk, wamepata ubaya gani hadi leo kwa kuwa waliruhusu uraia pacha ili tuchukue yaliyowapata kama onyo? Hizi nchi zimekuwa na athari gani, za usalama kwa mfano, wanazosema Tanzania itapata? Kwa nini Tanzania ionekane kama ikiidhinisha uraia pacha wake itavuta mambo mabaya tofauti na hizi nchi?

Siku zote nitamlaumu Kikwete. Badala ya kutia sahihi mswaada wa uraia pacha akasema ni vema usipitishwe peke yake uje ujumuishwe kwenye Katiba mpya. Katiba mpya iko wapi? Hapo ndipo tulikosea.

Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:
 
Kwani kama tukiwapa hadhi maalum wale raia wa Tanzania waliochukua uraia wa nje kuna shida gani? Kwamba wanaweza kurudi nyumbani bila kuhitaji visa,wataruhusiwa kumiliki ardhi,wataruhusiwa kufungua makampuni kama wazawa n.k
Lakini wasiruhusiwe kugombea vyeo vya kisiasa,kupiga kura n.k,sasa huko kung'ang'ana na uraia pacha kunatoka wapi au mnaosukuma hoja hiyo mna agenda yenu ya siri? Hivi leo ukiruhusu uraia pacha kwamba Mnyarwanda,Mcongo,Msomali,na kote huko kwenye migogoro inayotokana na sababu mbalimbali nchi yetu itakuwaje? Tuache unafiki serikali imeanza kuandaa sheria ya kuwapa hadhi maalum Watanzania hao waliochukua uraia wa nchi nyingine kwa sababu mbalimbali.
Ukiwa raia bas unakuwa huru kufanya lolote lisilo kinyume na Sheria , je kwann tuwazuie kwenye siasa , Hawa wazalendo wenu ndo wamekuja Tanganyikq Kwa miaka 60 Leo tuna PANYA road , watoto wa mtaan wasio na makaz , watu wasiojulikana , magaidi ya kibiti , magaidi ya amboni , utekaji , Wazee wa 10% , wafanya Kaz hewa , mafisadi , wazee wa laki si pesa , Tozo zisizo nq tija , masoko na stend kubinafsishwa kienyeji ,Wazee wa mishahara 17 kwq mwezi mmoja , mikataba mibovu mf wa DP world , Trafik kukusanya hela barabarani Kila gari

Huku tumefikishwa na wazalendo wenye uraia mmoja tu
 
Pascal, nimesema mara nyingi sana humu JF, kwamba wanaopinga uraia pacha wana hizi sifa kubwa
  • hawajui maana halisi ya uraia pacha
  • hawaajui ni jinsi gani mtu anaweza ku-qualify kuwa raia pacha wakidhani mtu yeyeote wa nje anaweza kuchukua uraia pacha wa Tanzania
  • hawana nafasi ya wao wenyewe kuwa raia pacha hivyo wana silka ya ubinafsi (selfishness) ya "kama sipati mimi basi wote tukose"
  • wivu unawasukuma kuwazibia wengine kwa sababu hawapendi kuona watu wengine wamefanikiwa
  • wanawaogopa diaspora kuja nchini na mawazo mbadala ambayo yanaweza kuleta vuguvugu jipya la uongozi nchini (kama ambavyo askari wa Afrika walipoenda kupigana nje vita ya WW2, walirudi na mawazo ya kudai uhuru Afrika)
Na nimesema wazi, Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa na wazo la uraia pacha. Karibu 75% ya nchi za Afrika zinaruhusu uraia pacha. Na nimekuwa nikiwauliza wanapinga uraia pacha kwa Tanzania, ni hasara gani nchi zenye kuruhusu uraia pacha zimepata hadi sasa? Nchi kama Rwanda, Kenya, South Africa, Burkina Faso, Cape Verde, Ghana, Guinea Bissau, Uganda, Mali, Niger, Nigeria nk, wamepata ubaya gani hadi leo kwa kuwa waliruhusu uraia pacha ili tuchukue kama onyo? Hizi nchi zimekuwa na athari gani za usalama wanazosema Tanzania itapata? Kwa nini Tanzania ionekane kama ikiidhinisha uraia pacha wake itavuta mambo mabaya tofauti na hizi nchi?

Siku zote nitamlaumu Kikwete. Badala ya kutia sahihi mswaada wa uraia pacha akasema ni vema usipitishwe peke yake uje ujumuishwe kwenye Katiba Mpya. Hapo ndipo tulikosea.
Huyo JK mwenyewe wanaomjua binti yake huko uingereza wanadai toka atie mguu huko, ajatoka tena kukanyaga Tanzania almost 20 years. Hao wajukuu ni babu ndio anawapandia ndege kwenda kuwatazama.

Ni uoga tu dual citizenship inafaida kwa Tanzania, kuliko kwa diaspora.
 
Ukiwa raia bas unakuwa huru kufanya lolote lisilo kinyume na Sheria , je kwann tuwazuie kwenye siasa , Hawa wazalendo wenu ndo wamekuja Tanganyikq Kwa miaka 60 Leo tuna PANYA road , watoto wa mtaan wasio na makaz , watu wasiojulikana , magaidi ya kibiti , magaidi ya amboni , utekaji , Wazee wa 10% , wafanya Kaz hewa , mafisadi , wazee wa laki si pesa , Tozo zisizo nq tija , masoko na stend kubinafsishwa kienyeji ,Wazee wa mishahara 17 kwq mwezi mmoja , mikataba mibovu mf wa DP world , Trafik kukusanya hela barabarani Kila gari

Huku tumefikishwa na wazalendo wenye uraia mmoja tu
Kwani wao si waliukana wenyewe uraia wa Tanzania na kuamua kuwa raia wa hizo nchi nyingine? Huwezi kula keki yako halafu ukadai bado unayo!
Kupanga ni kuchagua na wao wamechagua kuwa raia wa huko walipo.
 
CCM inaogopa wenye exposure toka Kulikotakata wanaweza wakapata nafasi za Kisiasa na kuwazindua Wadanganyika waliolala, hiyo ndio hofu kuu waliyonayo. Mifano ni harakati za Wahindi wa Canada na serikali ya Waziri Mkuu wa India na sehemu nyingi duniani. Chama chakavu wanapenda kuabudiwa na Kondoo Wadanganyika. Mama mitano tena

Ni akili chakavu tu sasa mtu kama ana uraia wa Canada na Tanzania na anapenda siasa kwa nini asifanyie Canada kwa wenye akili aje kufanyia shitholeni?
 
Kwani wao si waliukana wenyewe uraia wa Tanzania na kuamua kuwa raia wa hizo nchi nyingine? Huwezi kula keki yako halafu ukadai bado unayo!
Kupanga ni kuchagua na wao wamechagua kuwa raia wa huko walipo.

Ukaririsho huoo, nani alikufundisha kuchukua uraia wa nchi nyingine ni kukana nchi ya baba na babu zako? Darasa la ngapi wewe?
 
Back
Top Bottom