Kigwangalla kushangaa UDART kushindwa kuendesha mwendokasi ni unafiki wa kiwango cha juu

Kigwangalla kushangaa UDART kushindwa kuendesha mwendokasi ni unafiki wa kiwango cha juu

Tatizo kubwa ni siasa. Udart inaendeshwa kisiasa na wakati mwingine kibabe. Unakumbuka wakati wa JPM walipelekwa Suma jkt kuiendesha? Ni vizuri serekali kujiondoa lakini ni ufinyu wa akili kuikabidhi kwa wageni kuindesha. Zipo kampuni za kizawa nyingi zenye uzoefu wa biashara ya kubeba abiria zinaweza kuendesha Udart kwa ufanisi mkubwa.
Suma JKT hawajawahi kuendesha Udart. Suma JKT ni walinzi tu Kama walivyokuwa wanalinda wale CT. Wenzetu huwa sijui mnachanganyaje haya mambo.
 
"Wanangu wote nimesomeni maoni wala hayatofautiani na yangu,hilo suala mara kadhaa nimemuagiza Kaka yangu Profesa Mbarawa alitizame na timu yake lakini hakuna lolote lilofanyika,nadhani katika ziara yangu ya Oman muliniona kwenye picha na Mjomba wangu,sasa yule ndiyo kampuni yake yaja kuendesha mradi wa DART,wala musiwe na shaka wala muhali,mambo yatakuwa mazuri"
 
Suma JKT hawajawahi kuendesha Udart. Suma JKT ni walinzi tu Kama walivyokuwa wanalinda wale CT. Wenzetu huwa sijui mnachanganyaje haya mambo.
Mkuu madereva, mafundi na makarani wa kiraia wengi waliondolewa wakaajiri Suma jkt.
 
Aibu ilioje 😂😂😂 yani barabara ya kwako binafsi, gari zako pekee, abiria wote wakwako kwa umbali usiozidi 15Km.
Kwa ninavyojua biashara ya usafirishaji ndani ya dar inalipa mno na hapo wasafirishaji binafsi wanakwamishwa na trafiki polisi,nachoshangaa udart wanashindwaje na huku trafiki awawaletei usumbufu wowote!
 
Aliyeuwa mwendokasi ni Magufuli na alifanya haya kigwangala akiwa Waziri. Alikuwa wapi kusema haya?

Mwendokasi ilianza vizuri chini ya kampuni ya Maxmalipo na kulikuwa na ticket za kadi unalipia na kutumia wiki nzima na mapato yalikuwa yapo vizuri sana

Akaja magufuli akaondoa ile kampuni na kuleta ushamba wake eti akaweka wanajeshi na kukawa kuna kukata ticket kama daladala ndo mwisho wake mwendokasi imekuwa hivi. Wakata ticket wanajenga nyumba huku mradi unakufa watu wanajazwa kama kuku kwenye magari

Kigwangala angeongea kipindi kile wakati magufuli alivyokuwa anaua mwendokasi sio kuleta ujinga saivi
ishu ya kumwaga wanajeshi pale nlishawahi kuiskia
 
Mkuu madereva, mafundi na makarani wa kiraia wengi waliondolewa wakaajiri Suma jkt.
Suma JKT?? Ndio maana nasema unachanganya mambo, Suma JKT walichopewa ni ulinzi kwenye mwendokasi. Uendeshaji na management ipo kwa DART hadi sasa.

Hata hivyo management ndio inayoendesha biashara. Wengi wanapenda kuwatumia Suma JKT wakiaminj ni waadilifu(inaweza isiwe hivyo).

Na hata sasa haijafeli Dart wamekuwa waliotengeneza faida kubwa tu na mapato yakiongezeka maradufu. Bali kilichotokea Sasa ni mabadiliko ya kisera ni Kama vile awamu ya mkapa alipoamua kubadili sera na kuruhusu ubinafsishaji
 
ishu ya kumwaga wanajeshi pale nlishawahi kuiskia
Hakuna mwanajeshi alimwaga, wenzetu mpo mkoa gani? Suala la ulinzi walikuwa CT, ndio wakapewa suma JKT. Suma JKT ni walinzi Kama walivyo KK security na wengine.

Udart ilikuwepo na ipo kwa walewale, Ila Sasa hivi Kuna mabadiliko ya kisera ndio maana wanakaa pembeni.
 
Unaamini sababu ya kumpa mwekezaji ni kufeli kwa uongozi wa ndani? Tanesco Kuna idara kapewa mwekezaji, unataka kusema Tanesco nayo imefeli?

Alafu sababu yako ya max malipo haipo tena?
Uongozi umeafail ndo maana anapewa ulishaonaga wapi mtu anafanya vizuri alafu anatolewa

Kwenye maisha ukifanya vizuri unangangania na sio kuwa replace kadanganye wajinga
 
Uongozi umeafail ndo maana anapewa ulishaonaga wapi mtu anafanya vizuri alafu anatolewa

Kwenye maisha ukifanya vizuri unangangania na sio kuwa replace kadanganye wajinga
Hayo ni madabiliko ya kisera. Awamu ya mkapa alibinafsisha mashirika na viwanda sio kwa sababu walikuwa walifanya vibaya bali kutokana na mabadiliko ya kisera yalimpasa kufanya hivyo bahati mbaya sana hali ikawa mbaya tofauti na mwanzo.

Tanzania tulikuwa na viwanda vinavyoongoza kea uzalishaji na vilifanya vizuri sana Ila mabadiliko ya kisera kwa wakati huo yalifanya vibinafsishwe.
 
Kigwa yupo sahihi kabisa. Acha awachambue CCM wenzake, c wamemnyima cheo? Acha awanyee
 
Kiongozi wa Ccm anaikandia shirika la Ccm lililowekwa na Ccm kulinda maslai ya Ccm kwel haya maajabu
 
Udart kushindwa kuendesha mwendokasi sio suala la kushangaa ni unafki sana kushangaa kama wameshindwa.
Kingwangala kama walivyo watanzania wengi anasumbuliwa na unafiki pale wanaposhangaa kuona udart wameshindwa mwendokasi.

Yani unajenga barabara unamuita Mchina aje kuweka mabus abebe faida. Sasa kati ya ujenzi wa zile barabara na magari kipi kina gharama? Kama urasimu ni mwingi kwanini watu hawawajibishwi wakiiba? Nchi inadumaa kisa kuogopana na kuchekeana.

Mfano, wale waliyokuwa wanahujumu kivuko cha Magogoni na Kigamboni kabla hajapewa Bakharesa wangetakiwa wawe na kesi ya kujibu.

Kuna miaka itakuja tutamani kutawaliwa na wazungu voluntary kwa ridhaa yetu sababu ni kama somo la Management limetushinda sisi Waafrika na hii inamprove Wright Botha katika ile speech yake aliyoitoa.
SoC 2022 - Agizo lolote linapotelewa, muongozo wa mbadala wake utolewe, ili kuepusha kukiukwa kwa agizo hilo Kaisomee hii utanishukuru baadae aisee
 
Udart kushindwa kuendesha mwendokasi sio suala la kushangaa ni unafki sana kushangaa kama wameshindwa.
Kingwangala kama walivyo watanzania wengi anasumbuliwa na unafiki pale wanaposhangaa kuona udart wameshindwa mwendokasi.

Yani unajenga barabara unamuita Mchina aje kuweka mabus abebe faida. Sasa kati ya ujenzi wa zile barabara na magari kipi kina gharama? Kama urasimu ni mwingi kwanini watu hawawajibishwi wakiiba? Nchi inadumaa kisa kuogopana na kuchekeana.

Mfano, wale waliyokuwa wanahujumu kivuko cha Magogoni na Kigamboni kabla hajapewa Bakharesa wangetakiwa wawe na kesi ya kujibu.

Kuna miaka itakuja tutamani kutawaliwa na wazungu voluntary kwa ridhaa yetu sababu ni kama somo la Management limetushinda sisi Waafrika na hii inamprove Wright Botha katika ile speech yake aliyoitoa.
mtoa mada kwanza rekebisha kichwa cha habari sio UDART ni DART

udart ni kampuni tu iliyopewa tenda na dart kwaajili ya kutoa huduma za mabasi kwenye mradi wa mabasi yaendayo haraka na inamilikiwa na msajili wa hazina kwa asilimia 85 na simon group 15

DART ni wakala wa serikali wa mabasi yaendayo haraka ndio wamiliki wa mwendokasi yenyewe kwa niaba ya serikali

swali la kujiuliza je hazina ambayo ndio wamiliki wa udart na ambao ndio wanawajibika kulipa deni la word bank la mwendokasi wanaweza kujitoa halafu DART wakampa mtoa huduma mwingne?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
mtoa mada kwanza rekebisha kichwa cha habari sio UDART ni DART

udart ni kampuni tu iliyopewa tenda na dart kwaajili ya kutoa huduma za mabasi kwenye mradi wa mabasi yaendayo haraka na inamilikiwa na msajili wa hazina kwa asilimia 85 na simon group 15

DART ni wakala wa serikali wa mabasi yaendayo haraka ndio wamiliki wa mwendokasi yenyewe kwa niaba ya serikali

swali la kujiuliza je hazina ambayo ndio wamili wa udart na ambao ndio wanawajibika kulipa deni la word bank la mwendokasi wanaweza kujitoa halafu DART wakampa mtoa huduma mwingne?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hayo yote anayajua? Hakuna anacholewa hata kimoja kuhusu mradi na changamoto zake.

Ogopa sana mtu mjinga akitoa maoni
 
Huyu kama Polepole tu, akiteuliwa tena atanyamaxa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom