Kigwangalla na Bashe wamuomba Rais Samia kuanzisha mkoa mpya wa Nzega

Kigwangalla na Bashe wamuomba Rais Samia kuanzisha mkoa mpya wa Nzega

"Nimepokea maombi ya Bashe kuwa kabla sijaondoka 2030 Nzega iwe mkoa". Maswali yangu. 1. Wanadamu tunazuiliwa na mambo mengi. Mwenzetu anapatano na Mungu kuiona 2030? 2. 2025 kuna uchaguzi mkuu, je ana uhakika gani kuwa atashinda?. 3. Je, hakung'amua kuwa swali la Bashe limekaa kichonganishi kati ya mama na Mungu?

Kwa maana tunashauriwa kwamba tusiseme kuwa kesho nitafanya kile na kile na badala yake tuseme "MUNGU AKIPENDA kesho nitafanya kile na kile" 4. JE, wenzetu hawamtegemei Mungu ktk kuwaongoza wapiga kura kushinda uchaguzi kama yule mama marehemu alivyosemaga. 5. Je, ni madaraka ya kulevya kuanza kujitapa mambo ya kuondoka madarakani 2030 wakati bado tupo 2023 miaka kama 7 kabla.
Tanzania is Kingdom country!
Kwanini asishinde?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Ila siasa na Hawa wapuuzi ni kama mataahira,Sasa kama Hilo ni azimio la mkoa Toka Kitambo akilisemea mmja si inatosha Sasa kwani lazima Kila mtu aonekane amelisemea?

Pili nimeona facial impression ya Kigwangala Uso hauna Nuru kabisa sijui shida yake ni nini.

Kwamba ukitenguliwa kama yule Mpina ndio unachukia Rais au? 🤣🤣🤣🤣
Tatizo mh angesema naipa Nzega hadhi ya mkoa mmoja angetamba kuwa yeye kuomba mkoa so ikabidi msomali atibue kwa kumpa mama maneno kuwa mama tunaomba 2030 ukiondoka tuachie mkoa
 
Kigwangala anaomba Rais aipe Nzega hadhi ya mkoa baadaye anakuja Bashe anasema mama tunaomba unapoondoka 2030 basi wilaya ya Nzega iwe mkoa.

Anakuja Mh Rais anasema nimepokea maombi ya Mh. Bashe kuwa kabla sijaondoka 2030 Nzega iwe mkoa.

AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KIGWANGALA HUNA CHAK0 2025.

HUYO NDIO BASHE KASUKU WA SIASA AMBAYE VIDEO YAKE ANALIA ANATAKIWA KUTEKWA BUNGENI HAIPO POPOTE PALE MITANDAONI KAMA UNAYO, POST HAPA USAIDIE TAIFA.
Kwamba Rais anajibu "kabla sijaondoka 2030 Nzega itakuwa mkoa"?
Nani kamwambia kuwa 2025 Watanzania watamchagua yeye? Kwa nini anapenda kujidanganya? Au ni hizi sifa za mzaha wanazompa wapambe na chawa wake?
Ngoja atembelee wilayani kwetu atatukuta na mabango yenye ukweli;
"HALI NI NGUMU 2025 HATUKUCHAGUI KAPUMZIKE NA WAJUKUU"
 
Wabunge wa Nzega Hamis Kigwangala na Hussein Bashe walimenuomba Rais Samia kabla ya Kuondoka 2030 awape Mkoa Mpya wa Nzega.

Rais Samia amekubali Ombi Hilo hivyo Mkoa Mpya wa Nzega uko mbioni kuanzishwa.

----
Mbunge wa Nzega vijijini Hamisi Kigwangalla amemuomba Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwapatia wananchi wa Nzega Mkoa mpya kabla ya muhula wake kutamatika

Ombi hilo ni muendelezo wa ombi lililotolewa jana na Waziri wa kilimo ambaye pia ni Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe

Kigwangalla ametoa ombi hilo wakati wa Ziara ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipo simama kuwasalimia wananchi wa Puge Nzega mkoani Tabora.

Amesema wananchi wa Bukene wanapata tabu ya umbali mrefu kufika katika halmashauri yao kutokea eneo hilo la Puge ambapo ni umbali wa takribani kilometa 180 hivyo angeomba kabla ya ombi la Nzega kufanywa mkoa basi kupatikane Halmashauri ya wilaya ya Nzega pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Bukene.

''Bado tutabaki katika maombi yetu, ambayo jana pia tuliyasema kwamba tungependelea wakati unamalizia muda wako tafakuri yako ikupelekee kutupatia mkoa mpya wa Nzega '' Alisema Hamisi Kigwangalla

Chanzo: EATV

Maoni Yangu.
Naunga mkono kugawanywa Kwa Mkoa wa Tabora.

Sambamba na Tabora Serikali iugawe Mkoa wa Morogoro, Ruvuma, Lindi na Chato wasisahaulike.

20231015_162327.jpg
 
Ikiwezakana Tuwateke Burundi na Rwanda tudai ni maeneo yetu kama Israel inavyofanya Ili iwe mikoa mipya 🤪🤪

Bila kujitanua hatutoboi tutaanza kusumbuliwa na hivyo vinchi.
 
Wabunge wa Nzega Hamis Kigwangala na Hussein Bashe walimenuomba Rais Samia kabla ya Kuondoka 2030 awape Mkoa Mpya wa Nzega.

Rais Samia amekubali Ombi Hilo hivyo Mkoa Mpya wa Nzega uko mbioni kuanzishwa.

View: https://www.instagram.com/p/CyiWHsAKVBS/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Maoni Yangu.
Naunga mkono kugawanywa Kwa Mkoa wa Tabora.

Sambamba na Tabora Serikali iugawe Mkoa wa Morogoro,Ruvuma na Chato wasisahaulike.

Chato hapana, itoe hapo. Usilete ujinga wako wakati watu wana discuss mambo nyeti ya Taifa. Hilo la Chato kuwa mkoa limekufa na Dikteta wenu, na hatokuja tokea
 
Hahahaha.Wasomali ni wajanja mno. Nzega iwe mkoa jamani, watamega maeneo na mkoa wetu wa Shinyanga. Tumechoka Shinyanga na Mwanza yetu kumegwa.
Hii ni dalili ya uongozi ulioshindwa. Wanafikiri kuongoza mikoa mingi ndiyo kuleta maendeleo. Wanachotakiwa kufanya ni kurudisha madaraka kwa wananchi.
 
Tayari Kuna Majimbo 2 na wao ni wabunge.

Katiba haiombwi inapiganiwa.
Upo sahihi inapiganiwa, sasa kwa nini CCM haijishughulishi kuipigania? inavyoonekana ni kama vile wao haiwahusu - hebu tusaidie hapa.
 
Wabunge wa Nzega Hamis Kigwangala na Hussein Bashe walimenuomba Rais Samia kabla ya Kuondoka 2030 awape Mkoa Mpya wa Nzega.
Hii Mikoa nchi nzima inatakiwa uwe reviewed, kuna maeneo unatakiwa upite kwenye miji mingine ndipo ukafike kwenye makao makuu ya wilaya yako, kwa mfano wakazi wa Mlali, Mzumbe, Melela, Mangae Morogoro wanapita Morogoro mjini ili waende kwenye makao makuu ya wilaya yao Mvomero, Kuna wakazi wa Uvinza lazima wapite Tanganyika ndipo wafike makao yao ya wilaya Uvinza, kuna wakazi wa Kiteto lazima wapite Kondoa ndipo waende makao makuu Babati, wakazi wa MKIRU lazima wapite Dar ndipo wakamwone RC wao Kibaha
 
Ni shida ya kukosa Barabara tuu Wala sio mipaka.
 
Aisee 2030 ? Sijaelewa mkuu…huon kama psychologically wanaanda mindset za watu kujua kwamba atakuwepo na uchaguzi atashinda, mbona wameanza campaign mapema sana mkuu, unakumbuka ya magufuli kuongoza milele ? .
 
Back
Top Bottom