Kigwangalla na Bashe wamuomba Rais Samia kuanzisha mkoa mpya wa Nzega

Kigwangalla na Bashe wamuomba Rais Samia kuanzisha mkoa mpya wa Nzega

Aisee 2030 ? Sijaelewa mkuu…huon kama psychologically wanaanda mindset za watu kujua kwamba atakuwepo na uchaguzi atashinda, mbona wameanza campaign mapema sana mkuu, unakumbuka ya magufuli kuongoza milele ? .
Sasa kwani wewe unadhani nani atakuwa Rais baada ya 2025 tofauti na Samia? Cha kumzuia ni kifo au ugonjwa na sio vinginevyo
 
Kigwangwala ni "opportunists" kwani hili Bashe juzi nadhani kaliomba pale Igunga.
 
"Nimepokea maombi ya Bashe kuwa kabla sijaondoka 2030 Nzega iwe mkoa". Maswali yangu. 1. Wanadamu tunazuiliwa na mambo mengi. Mwenzetu anapatano na Mungu kuiona 2030? 2. 2025 kuna uchaguzi mkuu, je ana uhakika gani kuwa atashinda?. 3. Je, hakung'amua kuwa swali la Bashe limekaa kichonganishi kati ya mama na Mungu?

Kwa maana tunashauriwa kwamba tusiseme kuwa kesho nitafanya kile na kile na badala yake tuseme "MUNGU AKIPENDA kesho nitafanya kile na kile" 4. JE, wenzetu hawamtegemei Mungu ktk kuwaongoza wapiga kura kushinda uchaguzi kama yule mama marehemu alivyosemaga. 5. Je, ni madaraka ya kulevya kuanza kujitapa mambo ya kuondoka madarakani 2030 wakati bado tupo 2023 miaka kama 7 kabla.
Ameshaongea na DG wa DP World amlinde mpaka 2030 itakuwa
 
Hahahaha.Wasomali ni wajanja mno. Nzega iwe mkoa jamani, watamega maeneo na mkoa wetu wa Shinyanga. Tumechoka Shinyanga na Mwanza yetu kumegwa.
Kahama ilikua mkoa wa tabora,mkoa wa tabora ni mkubwa Sana,igunga,nzega,manonga,bukene zinatosha kuunda mkoa
 
Ndala ipo nzega,wilaya ya nzega kubwa Sana kieneo,zamani ikihusisha Hadi igunga
Kuna ndala ambayo ipo pia Mkoa wa shinyanga Mkuu inaenda mpaka ibinzamata (Stand ya mabasi kule) mpaka buhangija Huko Nimewahi kukaa shinyanga na Tabora so nafahamu mipka yao yote Boss
 
Yaani Shinyanga sijui wanataka iwe wilaya ?
Nzega huwa unapita tu stand kule nje ya mji siyo!?..miaka ya 90 kule usingepita,hapakua hata na njia ya kupitisha ng'ombe,wilaya ya nzega kubwa Sana,bukene ni sehemu yake,Sasa changanya bukene,igunga,nzega,puge,ndala,Hilo eneo dar inaingia Mara kadhaa
 
Wataimega kahama lazima hiyo..na huko singita, mpaka maeneo ya Ndala huko lazma wapachukue
Wilaya ya nzega ni zaidi ya nusu ya eneo la mkoa wa shinyanga,wamege kahama ya nini!?..nzega kua mkoa wataunga na igunga
 
Hii Mikoa nchi nzima inatakiwa uwe reviewed, kuna maeneo unatakiwa upite kwenye miji mingine ndipo ukafike kwenye makao makuu ya wilaya yako, kwa mfano wakazi wa Mlali, Mzumbe, Melela, Mangae Morogoro wanapita Morogoro mjini ili waende kwenye makao makuu ya wilaya yao Mvomero, Kuna wakazi wa Uvinza lazima wapite Tanganyika ndipo wafike makao yao ya wilaya Uvinza, kuna wakazi wa Kiteto lazima wapite Kondoa ndipo waende makao makuu Babati, wakazi wa MKIRU lazima wapite Dar ndipo wakamwone RC wao Kibaha
Point kubwa sana umeongea na hii inatokana na Kuwa na Vyuo vingi vya mipango Miji na vinavyotoa wanafunzi wengi ila cha ajabu ni kwamba Badala kumpa hizo kazi afanye aliyesoma mipango miji anapewa CHAWA fulani aliyesifia vizuri kuhusu kiongozi fulani unafikir Tutafika..

Watu wataendelea kufanya madudu lakini hakuna wa kuhoji...
Just Imagine kama Rais alifuta Hadhi ya Jiji kwa mkoa wa Dar es salaam bila kuhusisha wataalam we unafikiri nini changanoto zake
Mungu atusaidie tu tusiwe watumwa wa siasa milele
 
Point kubwa sana umeongea na hii inatokana na Kuwa na Vyuo vingi vya mipango Miji na vinavyotoa wanafunzi wengi ila cha ajabu ni kwamba Badala kumpa hizo kazi afanye aliyesoma mipango miji anapewa CHAWA fulani aliyesifia vizuri kuhusu kiongozi fulani unafikir Tutafika..

Watu wataendelea kufanya madudu lakini hakuna wa kuhoji...
Just Imagine kama Rais alifuta Hadhi ya Jiji kwa mkoa wa Dar es salaam bila kuhusisha wataalam we unafikiri nini changanoto zake
Mungu atusaidie tu tusiwe watumwa wa siasa milele
Thanks for compliments
 
Bukene Iko wapi?
Bukene iko nzega..Na kingine umewahi kufika shinyanga?
kwa sababu mimi nimefika Tabora karibu wilaya zote nilikuwa pale kwenye Research fulani nimeenda Nzega ,Nimeenda Igunga ,Nimeenda kaliua,Nimeenda urambo nimeenda tabora mjini wilaya zote nimeenda...
Kadhalika hata shinyanga nimeenda miaka y 2013 hiyi kabla hawajaimenya so naijua vizuri shy pamoja na tabora...

Wilaya kubwa mkoa mzima wa Tabora ni SIKONGE ikifuatiwa na KALIUA, Inakuja UYUI , Nzega na Igunga zinakaribia kulingana kwa ukubwa na kijigraphia then urambo na zinafuata zingine....
 
Hata Mimi sipendi kuliweka ila ukiangalia takwimu za idadi ya watu unaona kabisa Kuna vigezo tosha.

Pili tayari walishalimaliza Kwa ngazi zote ikiwemo kuweka miundombinu ya hadhi ya Mkoa

View: https://www.instagram.com/p/CyihAM5NC8i/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==View attachment 2785385View attachment 2785386View attachment 2785387

Miundombinu gani? Kwani miundombinu ndiyo kigezo cha kuwa mkoa? Alifanya makosa Mwendazake, kuufanya Chato uwe mkoa ni kuongeza chumvi kwenye kidonda
 
Kuongeza mikoa sio tija ,mkapa alipiga chini sera ya afya ya ccm ,akaichukua ya chadema mpaka anamaliza mihula yake miwili

Basi nanyi ccm kibalini nchi iongezwe kimajimbo ,kama chadema wanavyosema
 
Back
Top Bottom