The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amesema kuwa licha ya Tanzania kukubali mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, bado wapo watu na baadhi ya vyama vinavyotumia demokrasia hiyo kama kichaka cha kufanya vurugu na kuchochea uasi ndani ya Taifa.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara Itigi, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida Januari 18, 2026 Amesema wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa, kulikuwa na chama kimoja CCM na bila chama hicho, huenda hata upinzani usingefika hatua ya kuwa na nguvu za kisiasa kama ilivyo leo.
Hata hivyo, amesema wapo watu kutoka katika Vyama hivyo vya upinzani walio tayari kutafuta madaraka kwa gharama ya kuumiza wananchi.
"Kuna watu wako tayari kuutafuta uongozi hata kwa kuumiza watu wengine… vyama hivyo vipo, na vinawaambia Watanzania fanyeni vurugu muidai haki. Kuna haki ya vurugu? Hatuna Taifa lingine zaidi ya Tanzania."
Ziara ya Mwenezi huyo inaendelea leo Mkoani Singida, katika maeneo ya Singida Mjini.