Kihoro kikubwa cha kuogofya cha mwanaume(Men's worst nightmare)

Kihoro kikubwa cha kuogofya cha mwanaume(Men's worst nightmare)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Jambo moja gumu sana kwa hii jinsia yetu. Jambo linalobeba maumivu yasiyosemeka na yenye kusononesha sana

mara nyingi likiakisi hofu za ndani kabisa za wanaume. Hofu hizi hugusa maeneo nyeti ya maisha yetu ikiwemo uwezo wa faragha, afya ya uzazi, heshima katika jamii, na usalama wa mahusiano yao.

Kiuhalisia, mambo haya yanabeba uzito mkubwa kwa sababu yanatazamiwa kama vipimo vikuu vya uanaume.

Katika upande wa afya na uwezo wa faragha, changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni mapema ndizo hofu kuu zinazowanyima wanaume wengi amani.

Wanaume wengi wanahofia kushindwa kuwaridhisha wenza wao au kuonekana hawana stamina ya kutosha.

Aidha, wasiwasi kuhusu udogo wa maumbile na hofu ya kugundulika kuwa na ugumba au kutoweza kuratibu vizazi, huchangia kwa kiasi kikubwa msongo wa mawazo na kupoteza kujiamini.

Kwenye mahusiano na maisha ya kijamii, hofu kubwa zaidi ni kufanyiwa udanganyifu wa kilezi, ambapo mwanamume analea mtoto akiamini ni wake kumbe si wake (paternity fraud).

USaliti kutoka kwa mwenzi, kufilisika kiuchumi kutokana na migogoro ya kifamilia, na kusambaziwa picha au video za faragha mtandaoni ni mambo yanayotishia kuharibu utu na heshima yao.

Vilevile, hofu ya kukabiliwa na kashfa za uongo ambazo zinaweza kupoteza kazi au kuwapeleka gerezani ni jambo linalowasumbua wengi.

Zaidu, kuna hofu za kisaikolojia zinazotokana na jinsi mwanamume anavyochukuliwa na mwenzi wake.

Wanaume wengi wanaogopa sana kufanqnishwa vibaya na wapenzi wa zamani wa wenza wao, au kukataliwa kwa dharau pale wanapoonyesha nia ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Kupoteza heshima na nafasi ya uongozi ndani ya nyumba huwatafuna wanaume wengi kiakili, kwani huhisi wamepoteza thamani yao kama nguzo ya familia.

Imagine inapofikia mahali mwenzako anahama chumba cha kulala ama anapotaka kubadili nguo anakuomba umpishe🥺🙇🏿‍♂😭
3c235e81-91c0-45a5-b00c-e1f6cdfd8924.jpeg
 
kama unabadili badili wanawake na umeshatumia pesa kwao ,ndo tatizo la kukamia na kutumia mkongo linamaliza nguvu. Lakini kiwastani wazee wetu walikuwa na wake 3 au 2 ili kutengeneza balance.Hili tatizo halikusikika zama hizo
 
nadhani hofu kuu ya kupambana ayo ni kutokuwa imara kiuchumi
mathalan uwe na uwezo wa kulala kitandani mwaka mzima na bado familia isione kama maisha ni magumu
Haya ya urefu wa dhakari ama muda wa kukojoa sijui mke kaliwa nje ama mtoto hafanani na mimi ni mamo madogo sana ambayo yanajirekebisha ikiwa uchumi ni imara
 
Maisha yamebadilika sana
 
Wanaume tunapambana sana kutafuta pesa ili tuwe vichwa vya familia, lakini ukishafikia hatua ya kufukuzwa chumbani, hiyo ego yako yote inaishia hapo.
Kufukuzwa chumbani na mke wako ni moja kati ya mambo yanayoumiza na kushusha ego ya mwanaume kuliko kitu chochote, hata kama una fedha kiasi gani.Hali hii inaleta picha kamili kwamba pesa pekee haitoshi kulinda heshima yako kwenye ndoa.

Wakati mwanaume anapambana nje kutafuta fedha ili atimize wajibu wake kama kichwa cha familia, mwanamke ndani ya nyumba mara nyingi anatafuta uhusiano wa kihisia (emotional connection), amani, na kusikilizwa.
 
nadhani hofu kuu ya kupambana ayo ni kutokuwa imara kiuchumi
mathalan uwe na uwezo wa kulala kitandani mwaka mzima na bado familia isione kama maisha ni magumu
Haya ya urefu wa dhakari ama muda wa kukojoa sijui mke kaliwa nje ama mtoto hafanani na mimi ni mamo madogo sana ambayo yanajirekebisha ikiwa uchumi ni imara
Hata hivyo, uchumi imara ni nguzo moja tu kati ya mbili kuu zinazoshikilia ndoa.
 
Kwa Afrika hakuna mwanaume anaekosa nguvu za kiume labda tokea anazaliwa au kwa ajali, japo nguvu hizo zinatofautiana. Shida kubwa ni kusikiliza stori za uongo vijiweni ambazo mtu hujilinganisha akajionanyeye kumbe hafai.
 
Si vema kulikimbia ama kulikwepa hili tatizo kwasababu kama hizo. Hili tatizo ni halisi na lipo tena kwa ukubwa wake
 
Uzi una uzuri na ubaya wake
Silaha ziko wazi kutumika isivyo hasa pale mnapohitilafiana na mwenza.
 
Eeh mkuu hii ni ngoma kweli, mzigo wa pesa na mahusiano unaua mtu. Wazee wetu walikuwa na wake wengi kwa sababu maisha yalikuwa rahisi, sasa hata mke mmoja anakula mtu mzima. Ni kama ukishindwa unaitwa mchochote na ukifaulu unasemekana unabadilisha wanawake. Nimekubali kabisa hapo, ila bado naona k
 
Back
Top Bottom