Nimekuelewa lakini pointi yako ya kwanza inafanya kazi kwenye nadharia tu. Hakuna mwanaume anayeoa akijua huyu mwanamke atakuja kumkataa au kumletea nyodo baada ya miaka 10.
Wote huwa tunakuwa makini wakati wa kuchagua, lakini maisha yana tabia ya kumbadilisha mtu.
Point yako ni non sequitur logical fallacy.
Hakuna mtu anayejua kwa uhakika kuwa kesho atakuwapo, lakini hilo halituzuii kupanga maisha ya kesho.
Sijasema kwamba mwanamme anatakiwa kupanga kuwa na mwanamke ambaye ana uhakika 100% kuwa hawezi kumuacha.
Ila hilo halimaanishi kuwa mwanamme (au hata mwanamke for that matter) hawezi kuwa na chujio la kuchuja vicheche wa wazi kabisa ambao ukiwaangalia hapa unajua hamna kitu.
Objective si kutafuta mwanamke ambaye kamwe hatakuletea matatizo. That is against the laws of physics.
Objective ni risk minimization.
Wanaume wengi wanaangalia mwanamke mwenye makalio makubwa, mwenye sura nzuri, wengine mwenye pesa, kuliko kuangalia risk minimization katika mahusiano.
Yani kuna risk minimization fulani mwanamme ukishafanya, mfano ukishafikisha 98% ya vigezo, hiyo iliyobaki inakuwa sawa tu kuwapo, kwa sababu hakuna kitu kilicho 100%.
Ndiyo maana kwenye uchumi kukiwa na 5% unemployment wanahesabu hiyo ni full employment. Kwa sababu hiyo 5% inakuwa katika margin of error kui control ni kazi sana. Hawatafuti 100% employment ili waseme hapa kuna full employment.
Na mwanamke aliyefikisha vigezo 98%, hata mkishindwana mkaamua kuachana, hamtaachana kishamba kama kicheche ambaye hajafikisha hata 10% ya vigezo.
Point yangu si total control, that is against the laws of physics.
Point yangu ni risk minimization, kwenye levels mbili. Kwanza kupunguza saana saana uwezekano wa kuwa na mwanamke mnayeweza kuachana kirahisi, na pili, hata ikitokea hiyo 2% uliyobakisha ikawa mtu kabadilika, mkaachana, mnaachana vizuri kila mtu anaendelea na maisha yake.
Moja ya tatizo kubwa linalofanya hoja yangu kuwa ngumu ni utamaduni wa "all or nothing at all".
Yani ni kama tunaona mwanamme au hata mwanamke, kuwa kamili, kuwa ana sifa, ni kutoachana na mwanamke/mwanamme wake.
Suala la talaka, suala la kuachana, linaonekana kama kushindwa, kama upungufu. Na kuna masuala ya utamaduni na dini, yasiyo mazuri, yanachangia sana kwenye attitude hii.
Unaambiwa kwamba Mungu anachukia talaka. Unalazimishwa kwa pressure ya dini kukaa na mtu ambaye unaona kabisa hamuendani.
Wakati kuna sehemu kuachana ndiyo akili yenyewe. Mkikaa pamoja mnaweza kuongezeana matatizo mpaka mkauana.